Dhana ya majina ya sifa/ utambulisho

EMACHA

Senior Member
Jul 16, 2021
147
187
Hapa nazungumzia majina kama Mheshimiwa, Mstahiki, Daktari (Dr.), Mhandisi (Eng.) Wakili Msomi (Adv.), Mwalimu, Mkadiriaji majenzi (Arch.), Muhasibu (CPA), Mkemia; na mengine mengi kadiri yanavyoongezeka!

Tulipotoka huko zama za Ujamaa, Watanzania wote tuliitana "Ndugu", bila kujalisha wadhifa wa mtu.

Tulizoea kusikia Ndugu Rais, Ndugu Mwenyekiti, Ndugu Spika, Ndugu Waziri na hata Ndugu Mwananchi/Wananchi. Lakini pia Madaktari wa kutibu, wa PhD na wa-heshima walitumia 'tittle' hiyo ya Dr. (fulani).

Hoja yangu hapa ni kujadili kama kuna umuhimu wa utambulisho huo kwa viongozi, mfano: kwa nchi yetu hapa cheo/wadhifa wa juu kabisa kwa uongozi ni u-Rais; maana yake hapa Rais yupo juu ya viongozi wote na watu wote bila jujali taaluma zao.

Sasa ikitokea tukampata Rais, mfano amesomea uhandisi, halafu jina likasomeka Mh. Rais Mhandisi Mdendeule Magwega. (hapo vipi).

Kwa maoni yangu ingetosha kumuita Mh. Rais Mdendeule Magwega; maana wadhifa wa u-Rais upo juu sana ya huo Uhandisi aliosomea. Na kama tukiachana na dhana ya u-heshimiwa, ingetosha pia kumuita Rais Mdendeule Magwega.

Lakini pia wapo watu wanasoma vitu vingi, au wanapitia majukumu mengi kiasi kwamba utashindwa kumchagulia 'tittle' moja ya kumtambulisha. Mfano Jaji Mkuu mstaafu Augustino Ramadhani (RIP) alipata kuwa mwanajeshi, kawa Jaji na kisha Jaji Mkuu, na alipostaafu akawa mchungaji.

Huyu alipokuwa Jaji hakuwahi kujiasibu na cheo cha kijeshi (ingawa alifika ngazi ya Brigedia Jenerali); maana hapo angeitwa Mh. Jaji Mkuu Brigedia Jenerali Augustion Ramadhani (cheki mlolongo). Huwa inanichanganya kidogo kusikia Mkuu wa Mkoa CPA fulani, fulani.

Wanajopo, sipo hapa kubeza taaluma/elimu za watu, lakini tupunguze majina ya utambulisho/visifa hasa kwa viongozi, maana havina mnasaba na uongozi wake!

Napenda sana picha za Rais wetu (na hata waliopita), zile zinazobandikwa maofisini (Official Potrait),; tazama jina la Kiongozi wetu Mkuu lilivyoandikwa. Hakuna mbwembwe nyingi za majina.

RAIS SSH.jpg
 
Back
Top Bottom