Tuhuma za mauaji dhidi ya Dr. Mwakyembe na wenzake

Tatizo Polisi wenyewe ni sehemu ya uozo. Polisi wengi hasa wenye vyeo vikubwa ni vibaraka wa Viongozi kwa kulinda uovu wao kwa kuwa wanafaidika nao.
 
haya ngoja tuone
Wana JF, pamoja na kwamba ninafahamu kwamba Polisi hufanya kazi zao kwa kuangalia ratiba yao wenyewe na mara nyingi bila shinikizo, ninashawishika kuuliza hatma ya tuhuma zilizotolewa na Dr. Mwakyembe kuhusiana na njama za kumuua yeye pamoja na watanzania wengine sita. Tuhuma hizi zimekabidhiwa Polisi miezi kadhaa sasa lakini mpaka sasa hatupewi hata update kuhusiana na upelelezi ulipofikia na kama kuna ukweli wowote kuhusiana na tuhuma hizo. Basi kama ni za uzushi tuambiwe ili ifahamike kwamba habari hizo zilikuwa ni za kutungwa na ikiwezekana aliyetoa tuhuma achukuliwe hatua.

Kwa kweli kigugumizi hiki, hakitoi taswira nzuri sana kwa kutendaji na uadilifu wa jeshi letu la Polisi na inanikumbusha tuhuma zilizopata kutolewa na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP ambaye alishusha tuhuma nzito kuhusiana na njama za Polisi na mfanyabiashara mmoja kumuwekea mihadarati mtoto wa bwana Mengi ili akamatwe na Polisi. Hatujasikia chochote hadi sasa na wale waliotuhumiwa wanazidi kupeta na wengine wanaendelea kushikilia nyadhifa zao. Je ingekuwa tuhuma hizi zimetolewa na kigogo mkubwa serikalini au mfanyabiashara mwingine kama hawa wenye asili ya kiasia hali hii ingejitokeza? Hivi jeshi hili linaangalia usalama wa raia gani?
 
Back
Top Bottom