adriz
JF-Expert Member
- Sep 2, 2017
- 15,479
- 33,514
Akili kubwa , madini ya nguvu sanaView attachment 3514828
My people,
Tuchukulie kwa mfano ndege za Air Tanzania ni za kigogo mmoja wa Serikali, je hii itaathiri vipi maisha yako?
Tuchukulie kwamba mtoto mmoja wa namba one anamiliki matoy makali nyumbani kwake,je wewe mwananchi wa buza,mbagala,chanika au songwe huko unaathirika vipi kwa kipindi hiki
Halafu
Endapo kuna lockdown sasa hivi ya wiki moja au mbili,wewe mwananchi wa buza,mbagala,chanika au sogwe huko unaathirika vipi kwa kipindi hiki
Najua kwa wasio chukua muda kutafakari hawatanielewa kwa mifano hii nataka kueleza nini hapa.
Kabla sijaendelea unashauriwa kama una hasira za karibu au una mihemko ya karibu basi lililo bora kwako ama pita kushoto usisome nyuzi zangu au niignore hutaweza kuniona tena
Kwasababu mabandiko yangu yatawakera sana mpaka mwishoni mwa mwaka,na si kwamba natukana watu au naandika mambo yasiyo na maadili laa,bali natofautiana na wengi wenu kimtazamo
Mifano hapo juu inaonyesha kwamba ama Kiongozi wa serikali kumiliki ile midege au mtoto wa namba one kumiliki matoy kwenye yard yake,, haya mambo hayata kuathiri wewe moja kwa moja ,kwakuwa una amani na uhuru wa kufanya shughuli zako za uchumi na kupata mkate wako wa kila siku
Lakini kama yakatokea machafuko na serikali ikaweka lockdown basi mimi na wewe maisha yetu yatabadilika mara moja,shughuli za uchumi zitasimama,hakuna movement,hakuna kwenda hospitali wala sokoni wala wapi..
Je kati ya viwili hivyo kipi ni cha kupiganiwa zaidi? Na kulindwa kwa wivu mkubwa?
Majibu unayo wewe!
Amani yetu ndio tunu yetu basi tuilinde kwa wivu mkubwa sana, pinga harakati zote zinazo hatarisha amani ya nchi yetu
Na si kila mwenye kutuletea habari za uzushi na uongo mitandaoni tumkubali moja kwa moja,tujipe nafasi kujua ukweli wa habari hiyo kabla haijazua taharuki na kuleta madhara katika jamii
Tutaelewana mdogo mdogo
Ni hayo tu!