Tuhuma toka WikiLeaks: AL BAWARDY wajibu mapigo

Tuhuma toka WikiLeaks: AL BAWARDY wajibu mapigo

Unanchekesha! unaonesha hujui biashara na investments, hasara itaendelea maisha? si msingi walioweka lazima uoneshe hasra mpaka utaporudi? au ulifikiri wamewekeza shillingi kumi pale?

Hapo sijui nani atamsaidia mwenzake; sasa kama internal rate of return inaonyesha positive hiyo itaitwa hasara?
 
Wakuu kutokana na historia ya matukio ya bongo haswa katika sakata la Kagoda nnajikuta nna wasiwasi kwamba hii barua inayodaiwa kwamba jamaa wa Albwardy wamehit back inawezekana ikawa ya kuchonga:

1. Hiyo logo hapo juu ya hiyo barua ipo openly kwenye hii website (Hivyo basi kuichukua hapo na kuitengenezea barua kama hii wala si ishu) - Gonga hapa

2. Sahihi ya hii barua chini kabisa inaonekana ni kama vile ya kuunga unga!!!!!!!

3 Huyo Philip d'Abo anapo-refer cable na hata barua yake mwenyewe aliyoiwekea "best regards" kama memorundum inanipa wasiwasi kiasi flani.

4. Mtiririko wa majibu ya hii the so called "hitback" unafanana fanana na the recent press release! just a hint eti makubaliano ya ujenzi wa hoteli mbugani yalifanyika kipindi cha awamu ya tatu.

5. Huyu jamaa Philip d'Abo ni managing director lakini kwenye signature yake ameweka just director, well si ishu lakini kama umewahi kuwa a managing director u will now what I mean.

6. Source ya kwanza kabisa ya hii barua ni blog ya Dewji!!!!!!!! - Mohammed Dewji is in recordz humuhumu JF kuleta article ya tatizo la umeme na namna ya ufumbuzi wake. He pretended that article to be his up until he was shamed by one of JF member kwamba hiyo article alicopy na kupaste kama ilivyo kutoka The Economist. Alifanya hivi akiwa mbunge na one of the high profile businessman in Tz, that can hint how desperate this guy could be.

Anywayz ni wasiwasi wangu tu, labda tuelimishane kidogo kwa niliyoyaeleza hapo juu


e1.jpg



jkkss.jpg
 
Unanchekesha! unaonesha hujui biashara na investments, hasara itaendelea maisha? si msingi walioweka lazima uoneshe hasra mpaka utaporudi? au ulifikiri wamewekeza shillingi kumi pale?
<br><br>Hapo sijui nani atamsaidia mwenzake; sasa kama internal rate of return inaonyesha positive hiyo itaitwa hasara?
 
AL BAWARDY inaonekana nao ni amateurs when it comes to media tactics. These guys kama walivyo SALVA & PREMMY wamelala. they've forgotten that when a crisis hits, minutes are money. When your reputation and financial worth are tanking, speed should be NO 1 priority.

They (Salva & Co) should have been mindful, although in their eyes wanajiona the're moving fast, but they should have been more mindful of their every move. One would have thought by now Premmy, Barwady & Co should have understood the reason why a crisis is called a "defining moment" - and for this reason they should have 'thought' first, and 'do' second in this WIKILEAKS fall out.

And this guys who claims to have worked for Mr Ali Bawardy for over 30 years cant even spell SAVILE ROW...wao wameandika SAVILLE ROW tena mara kadhaa!

These guys should have learned from "NSSF war rooms" and where they understand that sometimes conventional PR is just not enough. Lightning-fast and ruthless in combat, NSSF understood that Tanzania's un regulated media and their mickey mouse journalists takes no prisoners when it really hits the fan. Strategic moves is their speciality and, with instinctive forward planning, their media team always guided them safely through the twists and turns of a media inquisition and now they can predict, counter and take advantage of upcoming developments while they are on their top game when it comes to taking control and managing the news agenda....contrary to our friends in Magogoni ambao wanasubiri Jamii Forum i set the agenda kisha wao wanafuata kama mbuzi vile. I mean what's so difficult kuanzisha website na wakapost hizi releases zao online so they sould spare our the embarrassment ya kukutana na hawa ma supermarket journalists tulionao?




london-savilerow4.jpg




This is the right spelling



wewe unaonekana uko arrogant sana

kila kitu lazima uingize NSSF?

unalipwa
 
OK. Angalau Mzungu Lisa Pile amekanusha kuelewa "hata neno moja la Kiswahili". Vinginevyo, hata maana halisi ya "flashy suits" nayo vilevile inaleta utata. Suti hiyohiyo ya Savile Row akivaa Prince Charles na Prince Harry, no problemo. Lakini akivaa JK au Chiluba (RIP), inakuwa mucho problemo; wakati ukweli ni kwamba wafadhali wa suti hizi za bei mbaya ni walipa kodi iwe UK, Zambia au Tanzania.

Tofauti ni kuwa wangereza hawaji kutuomba misaada kwa ajili ya maendeleo yao, sisi ndio tunaenda kuomba misaada kwao. Sasa lazima wajiridhishe kuwa unaomba msaada ina maana wewe ni maskinini, vipi mbona unavaa kitajiri, sio fedha za misaada yao zinatumika kununulia suti. Lazima tukubali wenzetu wako curious.
 
Hapana. Ana ndugu yake kule!


No wonder na mimi ananiudhi na hii arrogance yake ya kujidai ana jua englisha na kuwatukana wenzie

ndugu yake ndio yule mswahili au?

lakini hii arrogance wanaitoa wapi hawa waswahili?
 
ni watu wenye akili za kibangi bangi ndio wanaofanya hii habari kuwa dili, yani hii stori ya suti ndio mnaoitumia kutafuta umaarufu. kweli mlishafilisika ki mawazo.

Swali: yule muhindi alietoa pesa za kampeni chadema alimpakata nani? Milioni mia haziwezi toka kiulani tu, lazima kuna kitu kapewa.
Hapo kwenye bold,siku wikileaks wakileta habari za huyo muhindi aliyechangia chadema ujenge hoja
 
Jamani mi nimeimaindi sana wikileaks, hawa jamaa wameshawahi kuzilipua idara nyeti za FBI na CIA walifurukuta mwishowe wakaufyata sembuse hii serikali ya ****** na hawa makanjunju wake, naipenda sana slogan yao na ndiyo inayofanya kazi, sio magamba mara tumedhubutu, tumeweza na tunasonga mbele, ukiitafakari kwa kina unabaki na viulizo kibao, pumbavu!
 
Mwenye kuelewa sana haya mambo ni Mzee Mengi. Waliokaribu warongoshe kilichoyokea, kwani yeye mwenyewe alilalamika wakati ule

Usimuingize Mengi kwenye mjadala huu kwani naye tunamvutia pumzi ametuingiza mkenge kwenye Kampuni yao ya NICOL!! Malalamiko yake alitaka apewe Kilimanjaro hotel bure halafu awauzie wahindi kama alivyofanya kuuza kiwanja alichopewa na Mwinyi kujenga makao yake makuu akaenda kumuuzia FIDA!!
 
Yaani hata ukilta Jeans za Express kwa JK basi anakuuzia nchi
 
Guys,I think its high time to investigate the truth of this story and see how we can act upon irresponsible and corrupted leaders in our country.Mimi binafsi sioni sababu ya kuonyeshana kujua zaidi ya mwingine hasa kwa mjadala usioleta ufumbuzi wa issue iliopo mezani.Tatizo la watanzania tumekua watu wa ku Hit and Run,we dont take things more seriously thats why we discuss alot of things but we endup with unknown solution.We need to take action rather than being politicians....Mara Richmond,Kagoda,fisadi papa,Epa,Jailo,ngeleja na budget yake ya uongo,yote haya hayana majibu mpka sasa.Why the irresponsible leader dont resign as we witness in western countries?.....kweli dua la kuku hilmzui mwewe.What we are doing is like dua la kuku.......
 
Jinsi nchi inavyodhalilishwa na hawa wapuuzi waliokoo Ikulu,siwezi kuamini kwamba watu watakazana kusafishana hata bila kuwa na akili ya kutenganisha maneno aliyosema Salva na Prema hivi hawajui kuna watu wamesomea maswala ya utambuzi wa maudhui ya nyaraka na jumbe mbalimbali ,kwanza waraka unathibitisha Raisi huwa anavaa suti za duka hilo sasa kwa nini tusiamini alihongwa suti na mwanaume mwenzie, ,

mtu anasoma maelezo mambo ya kwenye waraka wa kwanza maudhui na ujumbe anaona uko sawasawa kabisa kama ujumbe unaofuata ,tofauti wamepindua mtiririko tuu, na kubadilisha baadhi ya maneno,mtu akituambia Lisa anakataa ,public itaprove vipi kwamba Lisa anasema kweli tupu, kwa nini wanajitetea chini ya masaa 24 baada ya taarifa ya IKULU yaani mwarabu LIsa wako karibu kiasi hicho na IKULU, yaani sinema inatisha yaani Lisa mara moja kajitokeza anataka apology hasemi kutoka wapi ,je ni kutoka weaklinks au ubalozi wa marekani au Ikulu,jamani ombwe hilo la uongozi hakuna hata mtu wa kureason hapo IKULU

baba Jakaya KIKwete kweli unauza Serengeti kwa suti pair tano umetutia aibu kubwa sana na kumbe huyu mwarabu ana nguvu sana nilimsikia Raisi Shein kwenye TV akisema Kempisinky itajengwa tuu Zanznibar hata wanahifadhi majumba ya kale wakisema hata wakalia alisema ni nyumba ya serikali wnaweza kufanya watakavyo ndivyo alivyo na nguvu achunguzwe naye usikute aliletewa na yeye hizo suti,ni upuuzi Raisi anapogeuza IKULU ni dangulo kwa kila mtu kufanya chochote atakacho shame
 
Usimuingize Mengi kwenye mjadala huu kwani naye tunamvutia pumzi ametuingiza mkenge kwenye Kampuni yao ya NICOL!! Malalamiko yake alitaka apewe Kilimanjaro hotel bure halafu awauzie wahindi kama alivyofanya kuuza kiwanja alichopewa na Mwinyi kujenga makao yake makuu akaenda kumuuzia FIDA!!

Ebu tujuze hili manake wengineo sisi tunamuheshimu mzee huyu,ukitupa keki yake tujue na kupata picha kamili ila usizushe kutuleta vitu ambavyo ni pumba.
 
Hii ni aibu sana kwa Taifa.

Kwa vijana mnaokua ambao siku zijazo mnaweza kuwa kwenye power, jifunzeni na jiozezeni sana kukataa vya bure kwani gharam zake ndizo hizi. Hawa wanaonadika barua za kukanusha, wanafanya hivyo kwa vile ama wameombwa au wametishiwa maslahi yao, na ukiosoma lugha zao kwa makini utagundua kuwa madai ya Wikileaks ama ni sahihi au yana ukweli, ila hawawezi kutamka hivyo kutokana na mazingira waliyonayo sasa.
 
MADAI ya zawadi za suti tano na dola 1,000 za Marekani kupewa Rais Jakaya Kikwete yamezidi kukanushwa, safari hii kauli ikitoka kwa waliodaiwa kuhusika na utoaji wa vitu hivyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosambazwa juzi kwa vyombo mbalimbali vya habari duniani kutoka kwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Albwardy Investment ya Dubai inayomiliki hoteli za Kempinski, madai ya WikiLeaks dhidi ya Kikwete ni uongo mtupu.

Mkurugenzi huyo Philip D’Abo, juzi aliandika kuwa katika maelezo yote yaliyomkariri Balozi wa zamani wa Marekani nchini Michel Retzer, ukweli pekee uliomo ni usahihi wa majina ya watu waliotajwa na hakuna mwingine zaidi ya huo.

“Nikiwa nimefanya kazi kwa zaidi ya miaka 30 na Ali Albwardy, na sasa nikiwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa kampuni zake, napenda kuweka sawa uongo huu uliopindukia na madai potofu dhidi ya Rais na bosi wangu.

“Kwanza, Lisa Pile, alikuwa Meneja Mauzo na Masoko wa hoteli ya Kilimanjaro, nimeongea naye na amekanusha katakata kuzungumza na Balozi chochote kama anavyodai na anathibitisha kuwa hawezi kutamka neno lolote la Kiswahili,” alisema D’Abo katika taarifa yake.

Alisema hata siku moja Rais Kikwete hakuwahi kuomba au kupewa rushwa na Albwardy na wala bosi wake huyo hakuwahi kumlipia Kikwete tiketi ya ndege kwenda London au kumnunulia hata suti moja katika duka la Saville Row.

“Huu ni utunzi na uzushi kama ilivyo katika madai ya kutoa dola milioni moja kwa CCM, kwani hakuna wakati hata mmoja kiongozi yeyote wa CCM aliomba fedha hizo kwa Albwardy,” alisema D’Abo.

Akizungumzia maombi ya bosi wake kuhusu ujenzi wa hoteli Zanzibar, D’Abo alisema wakati wa uzinduzi wa hoteli yake ya nyota tano, Albwardy yawezekana kweli aliomba eneo kwa ajili hiyo Mji Mkongwe, na baada ya miaka mitano ya majadiliano, alinunua eneo. Juu ya hoteli ya Serengeti, taarifa hiyo ilisema baada ya miaka mitano ya makubaliano kusainiwa, hatimaye bosi wake alijenga hoteli katika mbuga hizo – Bilila Kempinski.

“Hata hivyo hizo zilikuwa enzi za Waziri wa Utalii na Maliasili, Zakia Meghji, chini ya uongozi wa Awamu ya Tatu ya Rais Benjamin Mkapa … kwa eneo la Ngorongoro, hadi leo maombi hayajakubaliwa hata licha ya Rais Kikwete kuwa madarakani kwa zaidi ya miaka mitano sasa,” aliongeza D’Abo.

Alisisitiza, kuwa kutokana na Pile kutozungumza Kiswahili hakukuwa na uwezekano wowote wa kufanyika mawasiliano na mtu yeyote, na pia alikanusha kama ilivyo kwa menejimenti ya Kempinski, dhidi ya vyumba vya hoteli hiyo kutumiwa na viongozi wa Serikali.

D’Abo alisema kutokana na madai hayo, bosi wake anajisikia vibaya, kwamba uwekezaji wake katika nchi hii nzuri ya Tanzania, unaweza kuchafuliwa na uzushi kama huo kama ilivyo kwa Rais Kikwete ambaye naye anajisikia vibaya.

Wakati huo huo, Pile naye katika ujumbe wake kwa rafiki yake aliyetambuliwa kwa jina la Hasu Masrani, anaelezea kusikitishwa kwake na taarifa hizo, akisema huo ni uongo na ni uchafu na anajisikia kuchafuliwa hadhi yake.

“Sikuwahi kuzungumza Kiswahili na sikuwahi kuonana na Rais wa Tanzania wala Rais yeyote duniani. Naamini nastahili kuombwa radhi kwa kashfa hii kama mimi binafsi lakini pia taaluma yangu,” alisema Lisa.

Katika sehemu ya madai yake hayo, Balozi Retzer anakaririwa akisema “baadaye Oktoba 18, tukila chakula cha usiku (hotelini Kempinski), mtu mwenye asili ya kihindi au kiasia, aliyeelezewa kuwa mbia wa kibiashara wa Albwardy, alimchukua Lisa kutoka mezani kwake na kwenda kuteta naye kwa Kiswahili.

“Sina uhakika wa nini kilizungumzwa, lakini jina la Kikwete lilitamkwa mara nyingi na kisha akampa bahasha. Lisa aliniambia bahasha hiyo ilikuwa na dola 1,000 na zilikuwa ni kwa ajili ya kulipia mkutano wa Kikwete hotelini hapo baadaye mwezi huo.”

Ikulu ilikanusha madai hayo pia na kuelezea kusikitishwa kwake na kuziita kuwa kampeni hizo ni upuuzi na uzushi wenye lengo la kuchafua jina zuri la Rais katika hadhi ya kimataifa. Akifafanua kuhusu hilo, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salvatory Rweyemamu, alisema: “Tunasikitika kwa kuona jina la thamani la Balozi linahusishwa na ujinga kiasi hiki,” alisema Rweyemamu.

Alisema Rais Kikwete tangu akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, hakuwahi kupelekwa na mtu yeyote London, Uingereza, kama inavyodaiwa, kununuliwa suti tano.

SOURCE: HABARILEO
 
ohh kanunuliwa siti mara ohh sijui niini

mbona hapa hajavaa hiyo suti mnayompakazia?

GO9G6293.JPG



 
tumekuzoea wewe mama wa taarabu mwenye kutumia masaburi badala ya akili mazakafa


Unanchekesha! unaonesha hujui biashara na investments, hasara itaendelea maisha? si msingi walioweka lazima uoneshe hasra mpaka utaporudi? au ulifikiri wamewekeza shillingi kumi pale?
 
Back
Top Bottom