Ki Mun
JF-Expert Member
- Oct 6, 2014
- 3,442
- 4,393
Maneno kuwa Lowassa anatumia pesa sasa zinaonekana ni majungu tu ya watu waliochelewa kujipanga kiraslimali kushindana naye,sababu ni hizi:
1. Watia nia wote wanatumia pesa kulipia matangazo ya mikutano yao kwenye TV na Radio - tena wengine kama January Makamba wameenda mbali zaidi na kutumia karibu kila njia ya mawasiliano iliyopo duniani kwa sasa kujitangaza
2. Kwamba Lowassa alipeleka watu Arusha kuhudhuria mkutano wake - wachongaji haohao leo wamesafirisha watu kutoka pande zote za nchi kwenda kwenye mikutano yao Lindi na Mlimani City Dar es Salaam,tena wameenda mbali zaidi kwa kuchapisha mabango makubwa ya kampeni ( bila shaka CCM wameona hili) - Mabasi yao yamepambwa kwa picha kubwa zinazopamba basi zima.
3. Watu wamenunua mabasi maalum ya kifahari yenye vyumba vya kulala na ofisi - mi najiuliza haya mabasi hayauzwi wamepatiwa bure?au kwamba bei zake ni sawa na baiskeli?
Rasmi,tuhuma za matumizi ya pesa hazilipi tena wapinzani wa Lowassa ongezeni ubunifu kwenye mikakati yenu mtaweza kushindana kuliko kutumia siasa za majitaka mkitumaini kumshinda Lowassa - he is by far and large the pace-setter and the agenda-setter!