Jamani sasa Makamba amedhihirisha Ukombi wake,anavyojikomba kwa Kikwete leo kwenye TBC runinga akiongea na waandishi wa habari kujibu mashambulizi ya kina Qares amesema Kikwete ni maarufu kuliko CCM na anauzika ,hivi ni kweli?
Kama sikosei hao wana CCM waliwahi kutamka kuwa Chama ndio maarufu na sio mtu binafsi pale Dr Salmini alipotikisa kiberiti miaka ya nyuma pia Makamba amewaponda wasio nazo na kuwasifia matajiri kuwa ndio wanafanya chama kijiendesha ama kwa hakika nimeona sasa nambari wani wamewatupa mkono wale wananchi wa kawaida.
Makamba kakosa ubunifu wa kutafuta vyanzo vya mapato kwa chama chake ambacho kinahodhi miradi lukuki na kabaki kuwakumbatia matajiri ambao hufadhili huku akitegemea biashara zake hazitatozwa kodi ,atapata tenda za nguvu,kweli hao matajiri Makamba anauwezo wa kuwadhibiti pale wanapofanya madudu yao?
Si siri hao ndio wanaendesha nchi kwa jinsi wanavyotaka na ndio maana mzee Butiku amesema wafanyabiashara wamemfanya raisi wetu awe wao anashindwa kuwajibika kwa sababu wafanyabiashara wamemkamata anashindwa kujinasua, atajinasuaje wakati washauri wake ndio hao akina Makamba!!
Akina Kingunge ama kweli ndio maana Mwl Nyerere wakati mauti yanamkaribia alikaririwa akisema anasikitika kutuacha watanzania na atatuombea kwa Mungu.
Nani atajitoa muhanga kuwasaidia watanzania? Akina Warioba, Salim ni waoga ndio maana walikuwa wanataka mzee mwenzao Butiku asiseme yaliyojiri kwenye kikao cha kuwapitisha wagombea uraisi huko nyuma, wanaogopa ni wale wale, watu waoga hao wanaogopa kusema ili eti kulinda maslahi, sijui masilahi ya nini?