Tuhuma dhidi ya JK zaikoroga CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuhuma dhidi ya JK zaikoroga CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Che Kalizozele, Dec 4, 2009.

 1. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #1
  Dec 4, 2009
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  • MAKAMBA ADAI MAKADA WANALIPWA NA MAFISADI
  na Hellen Ngoromera

  MASHAMBULIZI ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) dhidi ya Rais Jakaya Kikwete kuhusu udhaifu wake wa uongozi, yameleta sokomoko katika chama hicho, na sasa Katibu Mkuu, Yusuf Makamba, ameibuka na kudai wanaomtuhumu rais wanalipwa na mafisadi.

  Akizungumza na Tanzania Daima kwa simu jana, Makamba alidai tuhuma dhidi ya Kikwete zinatolewa na watu wenye visasi, walioshindwa uchaguzi, na ambao wanafadhiliwa na matajiri wale wale wanaoitwa mafisadi wa CCM.

  “Unasema tumekumbatia mafisadi. Wanaosema CCM imekumbatia matajiri wako kwenye lisiti ya kulipwa mishahara na hao hao matajiri, kwani hili ni siri? Mbona tunayajua haya,” alisema.

  Aliwataja kwa majina baadhi ya makada wa CCM ambao aliwashutumu, wakiwamo Mateo Qares na Mussa Nkhangaa, ambao juzi walitoa kauli nzito wakitaka Rais Kikwete asigombee tena urais mwaka kesho kama atashindwa kuwashughulikia wafanyabiashara mafisadi waliomzunguka.

  Kauli zinazofanana na hii zilitolewa na makada wengine waandamizi katika CCM, wakiwamo Joseph Butiku, Joseph Warioba, Salim Ahmed Salim, Nape Nnauye, Dk. Harrison Mwakyembe, Fred Mpendazoe na wengine walioshiriki kongamano la siku tatu lililoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere mapema wiki hii, kujadili mustakabali wa taifa.

  Wakati Warioba na Dk. Salim wamewahi kunukuliwa wakisema nchi inapoteza mweleko kwa kukosa uongozi thabiti, kauli ambazo zimerudiwa wiki hii katika kongamano hilo, Butiku alisema rais amezungukwa na wezi, huku Qares akisema si lazima rais apewe mihula yote miwili kama ameshindwa kazi.

  Akijibu tuhuma hizo, Makamba alidai zimejengwa katika misingi ya chuki kwani wengi wa makada wa chama hicho waliokuwa wakizungumza katika kongamano hilo, ama wao wenyewe au wagombea wao waliangushwa katika harakati zao za kisiasa huko nyuma.

  Alisema Qaresi alikuwa mkuu wa mkoa na mgombea ubunge wa chama hicho, lakini sasa amepoteza hata nuru kwao baada ya kushindwa.

  “Qaresi alikuwa mkuu wa mkoa na alikuwa na mgombea wa chama hiki, wewe unamjua, amepoteza hata nuru kwao baada ya kushindwa katika ubunge.

  “Wako matajiri wangapi? Mbona aliposhindwa ukuu wa mkoa amekwenda kiwanda cha mbolea na kuajiriwa na tajiri?…Wanasema Kagoda, unawaeleza ni nani? Thibitisha. Ukisema makamba afumaniwa thibitisha.

  “Sisi ni watu wazima, tuna maeneo ya kujua. Kwa hiyo sishtuki wanaposema akina Nkhangaa na Qaresi. Kama umesoma taarifa ya Redet (Taasisi ya Utafiti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam) na ile taasisi nyingine (Synovate Tanzania) wameonyesha CCM na rais anakubalika.

  “Nkhangaa ameshindwa katika kura za maoni na (Mohammed) Dewji kule Singida mwaka 2005 na inajulikana hakumtaka Jakaya, alikuwa na mgombea wake katika nafasi ya urais. Mgombea wake alishindwa. Kwa hiyo maneno haya yote ni ya chuki,” alisema.

  Pamoja na mambo mengine, Makamba alisema CCM imeshinda katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwa 93% na katika ushindi huo hawakupigiwa kura na matajiri bali na watu wa ngazi ya chini.

  “Unaposema hivyo unakosea, ukishinda uchaguzi kwa asilimia 93 maana yake aliyekufanya ushinde ni chama na rais mwenyewe kama Redet anavyosema rais anakubalika kwa asilimia 83. Hiyo ndiyo indiketa ya mwaka 2010. Ni nani kama Jakaya? Hilo si la siri kila mtu anajua,” alisema Makamba.

  Pamoja na Makamba, Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz ambaye ni mmoja wa wafanyabiashara wanaohusishwa kwa ukaribu na Rais Kikwete, na ambaye amekuwa akihusishwa na kashfa nyingi, ameendelea kung’ang’ania hoja yake ya kutaka liundwe jopo la majaji kuchunguza kashfa ya Richmond anayohusishwa nayo.

  Alipinga kauli ya Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe aliyeshauri uwepo mjadala wa wazi katika vyombo vya habari na hukumu ya umma.

  “Inatia aibu na kushangaza kumuona Dk. Mwakyembe ambaye anapenda aonekane kuwa mwanasheria aliyebobea, leo hii anakataa pendekezo langu la kuwa na timu ya majaji wanaoheshimika, ili wabaini ukweli wa madai ya kamati iliyoongozwa na yeye,” alisema Rostam.

  Juzi, Dk. Mwakyembe alipendekeza wafanyabiashara wanaotuhumiwa wanunue muda katika vyombo vya habari, ufanyike mjadala wa kitaifa kati ya mafisadi na wapambanaji wa ufisadi, halafu baada ya hapo washiriki wote wapite mitaani kwa miguu kupima maoni ya umma.

  Rostam, mmoja wa watu walioguswa na sakata la Richmond, hakubaliani na pendekezo hilo, na anapinga maazimio ya Bunge linaloitaka serikali iwashughulikie watuhumiwa wote wa Richmond.
   
 2. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,145
  Likes Received: 1,238
  Trophy Points: 280
  crazy CCM, crazy Maka Mba
   
 3. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #3
  Dec 4, 2009
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Makamba makamba makamba, unazidi kuzeeka vibaya sana. angalia sana maneno yako yatakuhukumu. Redet inajulikana ni tawi la kikwete sema source nyingine. Utafikti wenyewe wa redet unafanyika kwenye vijiwe vya ccm sasa unategemea nini? mkuu wa redet ni mwanamtandao na ameshindwa kuiongoza udsm. Je ataweza kweli kufanya utafiti makini?
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Kzi ipo mwaka huu...JK will be among the weakest president this country has in its history
   
 5. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #5
  Dec 4, 2009
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,276
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  NOT the weakest in TZ...Think in africa, and he will not be, he is already...
   
 6. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #6
  Dec 4, 2009
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,276
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Makamba akawadanganye watoto kuhusu redet...Tunaijua vizuri A-Z na hata huyo boss wake alipewa ukuu wa mlimani wakati hata hakugombea, yani JK alifanya hivyo ili kumpliz mkandara.

  waliogombea walikua kina prof mshana, prof nkunya na prof idris wa pale ardhi lakini ghafla bin vuu mchakato ukabadilishwa akapewa yeye alafu akawapa madaraka wale wengine ili kuwatuliza, prof mshana akapewa mkwawa, prof nkunya ndo boss wa TCU(ile bodi ya vyuo vikuu) na Prof idris akapewa UDOM.

  so redet ni mwana mtandao wa JK full chai...
   
 7. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #7
  Dec 4, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Nakosa la kusema. Hivi hawa watu ambao wanajitokeza sasa na kusema hayo yote walikuwa wapi siku zote hizo tangia JK aingie madarakani mpaka sasa?
  Naona hawa pia walikuwa sehemu ya kusebabisha matatizo hayo yote, na sasa sijui wameitilafiana wapi tena mpaka imefikia hatua ya kuanikana hadharani.
  Yawezekana ni mbinu pia ya ccm kujipanga kwa 2010.
  "MADHAMBI YAO YANAWATAFUNA, WATATAJANA WOTE NA MAKOSA WALIYOTENDA KILA MMOJA" Tutaona na kusikia mengi kuelekea 2010
   
 8. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #8
  Dec 4, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Makamba hakibu hoja za kina Qures. Wanasema Kikwete kama hawezi kufanya maamuzi magumu kulinusuru taifa katika migogoro basi ateuliwe mgombea mbadala 2010 kugombea urais kwa tiketi ya CCM 2010. Makamba anasema Redet inasema JK anapendwa na wananchi kwa asilimia 83. My foot!!

  Kupendwa na kufanya maamuzi ni vitu viwili tofauti. In fact hulka ya binadamu umpenda mtu legelege asiyefanya maamuzi magumu.Na wazungu wanasema "spare the rod and you spoil the child" Yaani ukiona haya kutumia fimbo utamuaribu mtoto na utajuta baadae. Kuchapa mtoto ni maamuzi magumu lakini sio lazima uwe uamuzi mbaya. Queres na wenzake wanasema wakati umefika kwa JK kuwachapa kina Makamba, Rostam, Lowasa na wengine washike adabu yao. Yeye anasema Redet inasema JK anapendwa! Hivi Makamba aliwahi kuigia darasani?
   
 9. amanindoyella

  amanindoyella Senior Member

  #9
  Dec 4, 2009
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  We ZionTZ mbona data zako zinzelekea kwenye ukweli! Yu mkini na wewe ni rafiki/adui wa mkuu! Mwenye namba ya mkononi ya Jk tafadhali anipatie ili nijaribu kuongea nae!
   
 10. T

  Tata JF-Expert Member

  #10
  Dec 4, 2009
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,729
  Likes Received: 645
  Trophy Points: 280
  Wahenga walisema uzee dawa. Lakini ukifuatilia hoja na maneno ya baadhi ya wazee wetu kama Makamba unajiuliza kama kweli bado huu usemi wa wahenga unaendelea kuwa na maana iliyotarajiwa.
   
 11. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #11
  Dec 4, 2009
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,276
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Sio hivyo amanindoyella,


  Kila kitu kipo labda ww tu ndo hujui, ila mara nyingi tunayasema wanapojitokeza watu kupotosha ukweli.

  Hii serikali ishamshinda mkuu, akifwata ushauri wa wenzake kina quares na nkangaa itakua swala la msingi sana
   
 12. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #12
  Dec 4, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Siamini kama ni rais dhaifu Tanzania na Africa,hayo ni maono na fikra binafsi ambazo ni ruhusa mtu kutoa maoni kikatiba.

  Kam kunauthibithisho wa udhaifu wa Rais JK basi uelezwe ili tuone ukweli wa habari hizi.

  Hivi juzi Rais wa CUBA amekaririwa akimuomba Rais JK amsaidia kuishawishi Marekani kuondoa vizuizi iliyoiwekea CUBA.Sasa najiuliza hivi unawexza kwenda kumuomba usaidizi wowote ule kwa mtu aliyedhaifu?

  Uozo wote tunaouona sana sidhani kama umetokea kwa awamu hii ya nne pekee,kwa awamu zote zilizopita kulikuwa na mapungufu mengi sana.
   
 13. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #13
  Dec 4, 2009
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135

  Hivi kwanini tunaandikia mate wakati wino Upo, Makamba tunajua anazeeka vibaya kwani mimi namjua tokea tunaishi nae Tanga kule Amboni unajua zamani hakupitia Ujana mzee huyu sasa Huu ndo ujana wake yeye anajifanya kama Redet haijui akawadanganye malimbukeni sisi Watanzania Tupo juu tunajua nini tunafanya asitudanganye kama hana maneno ya kuongea akae kimya kwani Namkumbuka Philip Mangula alikuwa kimya kama hana point sasa huyu pumba nyingi alaa!! Stop!!!
   
 14. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #14
  Dec 4, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Makamba anatakiwa kuona aibu kusema siri za chama chake. Kwamba hadi leo bado makundi yaliyokuwepo kwenye uchaguzi wa 2005 bado yako hai na hakuna jitihada zilizofanywa kuweka utulivu ndani ya chama hicho. Yaani anathibitisha kabisa kuwa ndani ya chama ambacho yeye ni kiongozi mkubwa, kuna CHUKI? Sijui chuki iliyopo itawasaidia nini mwakani. Utegemezi wa report za REDET and SYNOVATE zinaweza kuwapa moyo kuwa bado mwenyekiti wao anapendwa na wananchi. Ila kura inapigwa kwa siri na haipigwi na hao REDET na SYNOVATE. Njia pekee ni kuweka utulivu ndani ya chama ili kila mwanachama afanye jitihada za kukitetea na kukifanya chama chake kishinde uchaguzi ujao.

  Nimesoma kuhusu mapendekezo ya Mwakyembe nikaona yanachekesha sana. Yaani wakitoka kwenye mdahalo wapite mitaani kuona kuwa wananchi wanaonaje kuhusiana na wote wawili? Kipimo gani hicho?
   
 15. W

  WildCard JF-Expert Member

  #15
  Dec 4, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kunya anye kuku tu, akinya bata kaharisha! Makamba katoa maoni yake. Anatetea kitumbua chake. Yuko pale kwa huruma na hisani ya JK. Hatutarajii azungumze kinyume na hayo.
  Msomeni vizuri Makamba. Anasema Quares alikuwa na mgombea wake, Sumaye. MNF walikuwa na mgombea wao, SAS. Makundi haya hayajawahi kuvunjwa. Yapo.
   
 16. nkawa

  nkawa Senior Member

  #16
  Dec 4, 2009
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 181
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lakini kwa huyu bwana yamezidi.....na kuombwa kuishawishi Marekani eti kuwaondolea vizuizi Cuba, nguvu hiyo hana....fuatilia uone...
   
 17. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #17
  Dec 4, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu, kauli zinazotolewa na viongozi kote duniani hufika kwenye audience wanazotarajia mapema sana. Kiongozi huyo wa CUBA alitumia nafasi hiyo kufikisha ujumbe wake kwa Rais wa Marekani. Vile vile, anaamini kuwa JK ana uhusiano mzuri tu na Rais Obama na hivyo anaweza kusaidia kufikisha ombi hilo kwa urahisi zaidi. Hii yote haimaanishi kuwa JK ni kiongozi mahiri, hodari au mwenye kuchukua hatua sahihi kwa ajili ya utawala alioomba watu wake.

  Unaweza kupendwa na mtu mwenye hadhi kubwa na akakusikiliza maombi yako kwa kuwa tu una udhaifu mkubwa na hivyo anakuonea huruma. Lakini pia tunajua interest za mataifa kama Marekani kwa nchi kama zetu huwa si zenye manufaa makubwa kwetu. Hivyo inawezekana kabisa kuwa Rais huyo wa CUBA anajua kuwa JK anaweza kutoa fadhila zaidi kwa Marekani na yeye akafaidika. Yote yanawezekana.

  Sijui unahitaji uthibitisho gani kuwa JK ameshindwa mara nyingi kufanya maamuzi magumu. Ila kuna taarifa za kutosha sana kuhusiana na hilo.
   
 18. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #18
  Dec 4, 2009
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Mwenye shibe atamjuaje mwenye njaa!!!! Makamba anadhani kila MTz anamfagilia boss wake na system yote hata kama anaboronga,Hao wote hawawezi kumsahihisha why???? wanabebembeleza kibarua
  Kila mwenye maoni tofauti ana chuki....sijui hii philosophy ya wapi??
  So Mzee endelea kuficha kichwa ardhini kama Mbuni
   
 19. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #19
  Dec 4, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  It is likely political game hapa hakuna kipya juu ya mambo haya
   
 20. w

  wasp JF-Expert Member

  #20
  Dec 4, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yusuf Makamba ni sawa na mpiga filimbi wa Amelin. Hata akijua Kikwete anaboronga yeye yuko radhi kumsifia. Mtu mweledi hawezi kuzikiliza pumba za Makamba maana zinatia kichefuchefu.
   
Loading...