TUHUMA: DED Karatu adaiwa kuwanyanyasa na kutamba kuwafanya chochote Watumishi bila kufanywa chochote

Mdaiwa-Sugu

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
284
910
Huyu ni DED wa wilaya ya Karatu. Anaitwa Waziri Morice.

Ananyanyasa sana watumishi wa Serikali katika wilaya yake na anavyowanyanyasa anatamba kuwa anaweza kuwafanya chochote na watumishi hao wasimfanye chochote wala kumpeleka popote.

Baadhi ya Mambo ambayo amekuwa akiyafanya:

1. Amekuwa akiwapiga baadhi ya watumishi hasa WALIMU makofi, ngumi, na wakati mwingine kwa kuvua mkanda na kuwatandika nao.

2. Amekuwa akiwadhalilisha WATUMISHI kwa lugha chafu hasa pale wanapodai maslahi yao.

3. Amekuwa akiwahamisha watumishi vituo vya kazi bila kuwalipa stahiki zao.

4. Amekuwa akiwafungia baadhi ya watumishi Mishahara kwa muda anaotaka bila kuzingatia
sheria za UTUMISHI WA UMMA. Imagine mtumishi anafanya kazi zaidi ya miezi mitano bila mshahara kisa mtu kaamua tu kumkomoa.

5. Amekuwa akiwanyima kwa makusudi watumishi wa Serikali kujiendeleza kielimu kwani hataki wawe na Elimu kumzidi lakini pia watumishi wengi wamekuwa wakitumia mwanya wa kwenda kusoma kuondoka na kutorudi WILAYA YA KARATU baada ya masomo kwa kukwepa manyanyaso ya DED. Kwa hivyo DED ameamua kuwakomesha kwa kuwanyima fursa za kujiendeleza kielimu.

6. Amekuwa akiwanyima watumishi UHAMISHO kutoka Karatu kwenda nje ya Karatu kwa makusudi hata kama wanastahili kuhama.

7. Amekuwa akitamba waziwazi kuwa amechakachua Uchaguzi MKUU wa 2020 na kulazimisha ushindi wa aliyekuwa mgombea wa CCM aitwaye DANIEL AWACK kwa kupora haki ya aliyekuwa mgombea wa CHADEMA aitwaye CESSILIA PARESSO.

10. Amewafungia wafanya biashara zaidi ya 300 MADUKA na biashara zingine kwa kigezo cha wafanyabiashara hao kushindwa kulipa kwa wakati KODI ya Tsh.50,000/=. Imagine mtu anafungiwa biashara ambayo ndio anategemea kulisha familia yake.

NB: Watumishi wengi wa UMMA na wafanyabiashara wa wilaya ya Karatu wamekata tamaa na wengine wanaacha kazi na kufunga biashara zao kwa sababu ya huyu DED na kwa bahati mbaya amekuwa akilalamikiwa lakini mamlaka husika hazijawahi kumchukulia hatua.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kama hajawapigia wake zenu muacheni tu. maana te rest ni tabia za UVCCM nchi nzima, walizoeshwa hivyo n baba yao.
 
Mkuu, hili suala la teuwa teuwa ndo chanzo Cha mambo yote, tuhuma za namna hii hyu jamaa si wa Kwanza, tumeona juzijuzi tu maDC na maDED wakifanya mambo design ya hayo hayo, Kuna haja ya Raisi kupunguziwa majukumu ya teuwa teuwa hizi, wengi wao huwa hawajui utawala Bora ukoje na wanawekwa kwenye mamlaka hizo kwa matakwa binafsi ya Raisi! Wengi wao hua ni vilaza. Natokeo yake ndo hayo!
 
Kuna Bw mmoja kaniambia kuwa majuzi wakiwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri, Mkurugenzi huyo alituhumiwa na Madiwani dhidi ya huo mwenendo wake ktk utendaji. Naye akawapa LIVE Madiwani wale kuwa aliyeshinda kihalali ni Diwani mmoja tu. Wengine wote niliwabeba mimi. Sasa endeleeni. Nasikia wote wakafyata na tuhuma zikawekwa kapuni.

Nakubaliana na mchangiaji mmoja aliyesema kuwa maeneo yote ambapo Upinzani ulikwa na nguvu, Walipelekwa Wakurugenzi na Ma DC kwa kazi maalum. Ndiyo maana wengi wao walijawa na viburi ujeuri na manyanyaso kwa Watumishi wengine.
 
Inamaana huyo DED analindwa kama Rais au Waziri mkuu?
Watumishi waache ujinga, dawa ya Moto ni Moto na si maji.
Wawakadi wanyantuzu wamtandike mshale wa sumu
Eti, au Zile panga zenye shingo pinda, zinatumika Sana Ntuzu kule ku wakata kata wachawi na vikongwe wenye macho mekundu
 
Ndio maana mzungu mmoja alisomba waafrika elfu na kuwaswaga kama mbuzi
Yaani karibia miaka 300 baadae bado mnachapwa mikanda na makofi

Sio wakurugenzi wakafundishwe utawala bora hapana ila nyie ndio mkafundishwe namna ya kujitawala
Bahati Nina Swaumu
 
mrembo hebu weka picha

Adjustments.jpg
 
Kuna watu ni wajinga duniani kweli.Yaani unipige kofi kisa KAZI??Bahati nzuri huyo mkurugenzi hayupo kwenye eneo langu la kazi angejua kama hajui.
 
Wamle kiboga huyo, kwanini mtu mmoja awasumbue wakati hana hata ulinzi wa kuaminika?!. Mleteni Mara kwa wakurya na wajita huku tumfunze adabu.
 
Back
Top Bottom