TUGHE: Zitto Kabwe ashtakiwe

TUGHE: Zitto Kabwe ashtakiwe

Status
Not open for further replies.

MTIMBICHI

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2013
Posts
946
Reaction score
214
CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya Nchini (TUGHE) kimetaka Zitto ashtakiwe kwa kutamka mshahara wa Rais na Waziri Mkuu hadharani.

========
HATUA ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kutaja hadharani mshahara wa Rais na Waziri Mkuu, imechukua sura mpya baada ya Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) kulaani hatua hiyo na kuomba Spika Anne Makinda kuchukua hatua kwa vile ni ukiukaji wa sheria.

Chama hicho kimeeleza kusikitishwa na kitendo hicho kufanywa na Mbunge aliyehusika na upitishaji wa sheria hiyo huku wabunge wenyewe wakiwa wakali pale wananchi na wadau mbalimbali wanapohoji mapato yao.

Katibu Mkuu wa Tughe Taifa, Ally Kiwenge alisema Dar es Salaam jana kwamba pamoja na hatua hiyo kukiuka sheria ya kazi na uhusiano kazini inayosema mshahara ni siri ya mwajiri na mwajiriwa, pia kitendo hicho si ajenda ya wafanyakazi hivi sasa.

Alisema ajenda ya wafanyakazi kwa sasa ni kuona wabunge wanapigana kufa kupona katika kuhakikisha kuwa mshahara wa mfanyakazi unaongezeka kukidhi mahitaji ya mwezi mzima na kuwaondolea mzigo wa mikopo inayowaandama.

"Huu si wakati wa wafanyakazi kutaka kujua mishahara ya Rais au Waziri Mkuu, ajenda yetu kwa sasa ni kuona wabunge wanapigana ili kuboresha mishahara ya wafanyakazi ili ukidhi mahitaji muhimu tofauti na sasa," alisema Kiwenge.

Alisema pamoja na hilo ni mkakati wa wafanyakazi sasa kuona wabunge wanatumia muda wao uliosalia kabla ya Bunge kuvunjwa kuhakikisha mambo makubwa mawili yanaingizwa katika Katiba mpya, moja ikiwa ni nafasi ya mfanyakazi kikatiba ikoje na pia kuona Katiba mpya inasema nini juu ya hatima ya maslahi ya wafanyakazi.

"Tunataka Katiba mpya itamke wazi juu ya mishahara ya wafanyakazi ili iwe ni ile inayokidhi haja," alisema.

Aeleza kuwa ni jambo la kusikitisha kuona wabunge wanaanza kutaja mishahara ya viongozi wa taifa hadharani kwa kudhani kuwa ndio njia sahihi ya kuwasaidia Watanzania bila kujua kuwa hatua hiyo itasababisha mgawanyiko wa matabaka na kuligawa Taifa, jambo ambalo ni la hatari.

"Sisi mishahara ya viongozi wote tunaifahamu na hata ya wabunge, lakini sheria inasemaje juu ya kutangaza mshahara wa mtu hadharani? Wafanyakazi wanaweza kuitaja lakini kwa vile wameandaliwa hawafanyi hivyo, wanazingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi.

"Naamini kama wafanyakazi wangekuwa ni watu wa kukusanyana na wangekuwa hawana maadili wangeweza kusema mengi ambayo yangeshangaza jamii lakini hawafanyi mambo kwa kukurupuka au kuutafuta umaarufu usio na msingi," alisema.

Katibu Mkuu huyo wa Tughe alisema kwa kufuata mfano wa wafanyakazi, viongozi wakiwemo wabunge watoe kauli za kujenga nchi na si zenye kuashiria matabaka na ubaguzi, jambo linaloweza kusababisha migogoro mikubwa na kuliingiza taifa katika machafuko yasiyo na tija," alisema.

Alisema wabunge wafahamu pia kwamba suala la mishahara litaendelea kubakia kuwa ni la mwajiri na mwajiriwa na ndio maana katika fomu au nyaraka nyingine zinazoelezea majukumu ya wabunge suala la mishahara na marupurupu yao haliwekwi wazi kwa vile ni siri kati yao na taasisi ya Bunge kisheria.
 
Rais aliomba kazi ya kutuongoza, nasi tulimpa kwa njia ya kura. Rais naye amewateua Mawaziri na Vigogo wengine ili wamsaidie kutuongoza vizuri. Sasa inakuwaje dhambi/siri kwa Mwajiri kutaka kujua mishahara wanayojipangia bila sisi wenye nchi kuhusishwa? Haiingii akilini hata siku moja kwa Mwajiri kutojua mshahara wa mtumishi wake aliyemwajiri, vinginevyo utakuwa Mwajiri fake!
 
yaani mburula kama wewe umwajiri Rais? kichekesho sana. binafsi namlaumu sana ZITTO kwa move aliyoianzisha tena kwa maslahi yake binafsi ndani ya chama.
 
Hivi, mwajili wako kujuwa mshahara wako ni dhambi..??? Kama wewe umeamua muajili wako awe hadhara, basi hadhara lazima ijuwe mshahara wako.....

NB: Raisi kaajiliwa na hadhara

kwani wananchi wote ndo wamemwajiri Rais? Ni wale tu waliopiga kura na kumchagua JK ndo wanapaswa kujua mshahara wake na si wananchi wote. yaani hata machadema nanyi mnajiita ni mwajiri wa JK?
 
Hao THUGHE ni wapuuzi watupu! wameshindwa kutetea maslahi ya wafanyakazi wanakimbilia kulinda mishahara ya wakubwa isitajwe! hivi kweli inaingia akilini JK alipwe milioni 34, Pinda milioni 26 kwa mwezi wakati mtumishi chini ya TUGHE analipwa 150,ooo/= kwa mwezi; na TUGHE wanona hilo sawa!!

Hivi TUGHE wanajua kwamba mshahara wa David Cameron au Barack Obama unaweza kuujua kutoka kwenye tovuti!? Hivi huko TUGHE kuna watu wa aina gani?! walevi au wavuvi tu?!
Let them shoot the first salvo!
 
Rais aliomba kazi ya kutuongoza, nasi tulimpa kwa njia ya kura. Rais naye amewateua Mawaziri na Vigogo wengine ili wamsaidie kutuongoza vizuri. Sasa inakuwaje dhambi/siri kwa Mwajiri kutaka kujua mishahara wanayojipangia bila sisi wenye nchi kuhusishwa? Haiingii akilini hata siku moja kwa Mwajiri kutojua mshahara wa mtumishi wake aliyemwajiri, vinginevyo utakuwa Mwajiri fake!
Mi pia nawashangaa sana hao wanaojiita waajiri, na wanaotaka kuambiwa mishahara ya waliowaajiri. Hivi inakuwaje unamwajiri mtumishi halafu unasubiri mtu mwingine akwambie mshahara wake. Kama mnajiita waajiri (ambayo ni kweli kwa namna moja ama nyingine), si mlipaswa kutamka kiasi gani atalipwa huyo mwajiriwa. Kwani hao vilaza mnaowapeleka bungeni si ndio wanaopitisha hiyo mishahara. Kwani wao si wanaipitisha kwa niaba yenu. Basi kwa hoja zenu maana yake wanaopaswa kuujua mshahara wa Rais na pm ni wale tu waliompigia kura maana hao ndio waliomwajiri. Karibuni na mitusi yenu, maana najua mishipa ya Shingo itawasimama na mapovu yatawatoka
 
Hao THUGHE ni wapuuzi watupu! wameshindwa kutetea maslahi ya wafanyakazi wanakimbilia kulinda mishahara ya wakubwa isitajwe! hivi kweli inaingia akilini JK alipwe milioni 34, Pinda milioni 26 kwa mwezi wakati mtumishi chini ya TUGHE analipwa 150,ooo/= kwa mwezi; na TUGHE wanona hilo sawa!! Hivi TUGHE wanajua kwamba mshahara wa David Cameron au Barack Obama unaweza kuujua kutoka kwenye tovuti!? Hivi huko TUGHE kuna watu wa aina gani?! walevi au wavuvi tu?!
Let them shoot the first salvo!

umeropoka sana wewe. Hivi unaweza kututajia hapo Kinondoni unalipwa kiasi gani?
 
Hivi, mwajili wako kujuwa mshahara wako ni dhambi..??? Kama wewe umeamua muajili wako awe hadhara, basi hadhara lazima ijuwe mshahara wako.....

NB: Raisi kaajiliwa na hadhara

wewe umemwajili nani sasa unadhani hayo mawazo yako yanamantiki sana.
 
Hivi, mwajili wako kujuwa mshahara wako ni dhambi..??? Kama wewe umeamua muajili wako awe hadhara, basi hadhara lazima ijuwe mshahara wako.....

NB: Raisi kaajiliwa na hadhara

Wanaopinga mishahara yao kujilikana ni wezi, awe rais, waziri mkuu au hata hao vibaraka TUGHE
 
Kwa hiyo THUGE wanalinda huu upuuzi? Mbona wafanyakazi wengine mishahara yao ni midogo sana? Je hili hawalioni?
 
kwani wananchi wote ndo wamemwajiri Rais? Ni wale tu waliopiga kura na kumchagua JK ndo wanapaswa kujua mshahara wake na si wananchi wote. yaani hata machadema nanyi mnajiita ni mwajiri wa JK?

Tatizo lako unaandika kwa ushabiki sana bila kuangalia facts!.
 
Khaa! Kumbe ukitaja mshahara wa raisi unashitakiwa! Hii nchi wazee wetu walilewa sifa wakat wanatunga sheria hizi. Hovyoo kabisa
 
Product ya mulugo wewe,yaani hata hujui dhamana ya madaraka ya rais inatoka wapi
yaani mburula kama wewe umwajiri Rais? kichekesho sana. binafsi namlaumu sana ZITTO kwa move aliyoianzisha tena kwa maslahi yake binafsi ndani ya chama.
 
TUGHE imetaka Zitto ashtakiwe kwa kutamka mshahara wa rais na waziri mkuu hadharani.

Nilipokuwa nasoma hizi habari Zitto akiropoka kujitafutia umaarufu zaidi ya alionao nilishangaa sana.

TUGHE watofautishe kati ya waajiriwa katika sekta ya umma na sekta binafsi, na wanasiasa ambao ni waajiriwa wa wananchi. TUGHE wangekuwa na malamka ya kumshitaki Zitto kama angekuwa ametaja hadharani mishahara ya watumishi katika sekta ya umma au binafsi, lakini sio kundi la wanasiasa ambao ni waajioriwa wa wananchi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom