Tufundishane namna ya kuombaTender | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tufundishane namna ya kuombaTender

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Masikini_Jeuri, Sep 3, 2010.

 1. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Wandugu ujasiliamali unakua na sio wote tunaweza kuhudhuria hayo madarasa na kozi mbalimbali ilimradi tunapigana pia kila kukicha kujikwamua; Maadam jukwaa hili ni la wajasiriamali natoa mwito kwa wenye uzoefu watufunze hatua kwa hatua ni namana gani tunaweza kuapply tenda mbalia mbali nitatole tu mfano mie niko kwenye nyanja ya huduma za teknohama.
  Nimeamua kujitosa kuomba tender na kampuni tayari ipo ila uzoefu huo sina kwani nimekuwa nikifanya kwa mkataba na watu walioshika tenda hizo.

  Nitashukuru
   
 2. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2010
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kama huko kwenye biashara ya TEKNOHAMA nafikiri kuna namna mbili kubwa unaweza kuzitumia kupata biashara hasa kwa mazingiria ya Tanzania.Moja ni kwa kutumia tender kama ulivyoandika na ya pili ni ku-pitch in kwa njia ya proposal na meetings.

  Kuhusu tender unatakiwa uangalie kwenye magazeti na uone matangazo juu ya services ambazo unaweza kutoa.Kisha unafuata taratibu za kupata tender documents.Mara nyingi ofisi nyingi utapaswa kuandika barua ya kuonesha interest ya kununua tender husika na utaenda nayo na kulipa kiasi cha pesa ambacho kimetajwa ili kupata hizi documents.

  Sasa uhandishi wa tender kwa kawaida si mgumu...unafuata utaratibu ambao umewekwa kwenye hizi tender documents.Na mara nyingi inategemea una-bid/tender kwa kitu gani maana inaweza kuwa unataka ku-offer goods,services au works kwa hiyo hizi aina zote hapa zina guidelines zake.

  Unaweza kupata nafikiri some documents kwenye website ya PPRA Welcome to the PPRA Website ingawa guidelines utakazopata hapa zitakuwa kwa upande wa tender za serikali.Makampuni binafsi yanaweza kuwa na taratibu zake binafsi na hayafungwi na sheria ya manunuzi/procurement act inayotumika kwa sasa.

  Njia ya pili hiyo ya kupata biashara nimesema ni ya kwenda kuuza idea juu ya product au some services ambazo kampuni yako inaweza kuzitoa.Hii mimi naiona ni nzuri zaidi hasa kama kampuni yako si kubwa na haijakuwa kwenye soko kwa muda mrefu.

  Kwa mfano kama kampuni yako inafanya biashara ya kutengeneza websites basi angalia makampuni,taasisi na watu binafsi ambao unafikiri watahitaji websites na ambao kwa sasa hawana.Unaandika ka-proposal ka-page mbili na barua ya kujitambulisha...ikiwezekana angalia uwezekano wa kupata appointment ya kumuona muhisika kwa mazungumzo zaidi.

  Kwenye hiyo proposal yako ndogo unaweza kuweka vitu kama taarifa juu ya kampuni yako na nini unaweza kufanya kwa mteja unayemkusudia...pia unaweza kuweka baadhi ya kazi ambazo umekwisha wahi kufanya.That way nafikiri utakuwa na nafasi ya kupata biashara mara nyingi...you just need to be more aggressive na bila kukata tamaa!Ni muhimu kuhakikisha unajifunza zaidi juu ya sales techniques.

  Soko la TEKNOHAMA Tanzania kwa sasa limejaa players wengi lakini wanaofanya biashara kweli ni wachache sana na opportunities bado ziko nyingi sana.Fikiria na jaribu kulete vitu vipya kwenye market hiyo ni sehemu ya kazi ya watu walio kwenye TEKNOHAMA.Siri kubwa ni kusoma trends kwenye TEKNOHAMA kwa sasa na that way unaweza kugundua sehemu gani ukitupa pesa unaweza kupata returns za maana kama kampuni

  Goodluck!
   
 3. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #3
  Sep 4, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Ubarikiwe Mpogoro! Samahani naweza kukutafuta kwa mashauriano zaidi........nitashukuru.
   
 4. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #4
  Sep 4, 2010
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Niandikie Private Message tu hapa JF na tutaangalia namna ya kubadilishana mawasiliano yetu.Siko Dar es salaam kwa sasa lakini niko tayari kushauriana na wewe katika namna mbalimbali ambazo zinaweza kukusaidia kufanikiwa katika shughuli za biashara unazofanya.
   
 5. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #5
  Nov 16, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mpogolo upo juu
   
 6. l

  laun Senior Member

  #6
  Nov 16, 2011
  Joined: Sep 5, 2011
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  To be honest kupata tender Serikalini andaa na malipo yanayofanyikia bar,hotel au kwenye gari bila risti,
   
 7. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #7
  Nov 16, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hiyo kweli kabisa haina ubishi.kufa kufaana
   
 8. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #8
  Nov 16, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  mhhhhhhhhh!
   
Loading...