Tufikirie juu ya miundombinu Ya chuo kikuu cha Dodoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tufikirie juu ya miundombinu Ya chuo kikuu cha Dodoma

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by fikirini, May 26, 2011.

 1. fikirini

  fikirini Senior Member

  #1
  May 26, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nikiwa mgeni kabisa katika safu hii ya jamii forum yenye kutoa fursa ya fikra pevu na zisizo za woga. leo naomba tufikirie pamoja nanyi katika hili! mapema wiki hii vyombo vya habari viliripoti na kuonesha hali ya hatari ya majengo na mitaro inayozunguka kampasi ya chuo kikuu cha Dodoma. uwepo wa nyufa katika majengo wanapolala watanzania na wasomi wenzetu ni hali hatarishi kwa rasilimali ya taifa. kuna vyuo kama udsm, sokoine ambavyo vimejengwa miongo mingi iliyopita lakini hadi sasa hakuna nyufa za ajabu kulinganisha na umri wa majengo hayo. kuna nini udom? kuanzishwa kwa udom kwa mbwembwe na majigambo ya viongozi wetu wa kitaifa ilikuwa ni jambo la dharula? Hatuna wakandarasi weledi ambao wangeweza kufanya kazi yenye tija? au ujenzi huu wa chuo kikubwa kama hicho ni mradi wa kumnufaisha mtu mmoja? na je si fedha za walipakodi wa nchi hii?. Hebu ndugu zangu naombeni mawazo yenu katika hili.
  Ni mimi Fikirini
   
 2. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Karibu jukwaani.

  Wanachuo walale kiainaaina huku wakijihami wasiangukiwa na matofali usiku.
   
 3. M

  MSEHWA Member

  #3
  May 26, 2011
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi hii UDOM itafikia hatua tuichoke. Kila anaeingia ni kutoa maada juu ya UDOM. Inashangaza kumuona huyo huyo akimuomba mdogo wake asiache kuchagua UDOM. Hivi JF niukumbi wa kuonyesha maovu tu? Tujifunze kuandika faida ya kitu na hasara za kitu ili wachangiaji tuwe na uwanja mpana.
   
 4. fikirini

  fikirini Senior Member

  #4
  May 26, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nakushukuru msehwa kwa mchango wako, ni kweli nina wadogo zangu watatu pale udom, na wengine ni ndugu zangu watanzania. ni kweli inabidi tuongelee faida pia pale inapobidi, lakini faida hizi haziwezi letwa na mazingira mabovu endapo tutayaacha kama vile hatuoni. ubovu wa miundombino ni sehemu tu ya udhaifu uliopo udom...na niliona tulimulike kwanza hilo. kwa sababu mimi nimeongelea upande wa pili wa shilingi isionekane nawakatisha tamaa wadau wa elimu ktk chuo cha udom, basi ni vyema wewe ukatoa tu kwa uhuru hizo faida za udom...ambazo kimsingi nna imani zitakuwa sahihi zaidi endapo miundombinu, rasilimali watu,uongozi bora vitatupiwa jicho la tatu kwa kuleta chachu ya matokeo mema ya kisima cha elimu kama udom.
   
 5. Chief-Mkwawa

  Chief-Mkwawa Platinum Member

  #5
  May 26, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 17,788
  Likes Received: 7,109
  Trophy Points: 280
  inajulikana wazi kua udom imejengwa eneo ambalo limepitiwa na bonde la ufa vitu kama nyufa ni kawaida tutegemee matengenezo ya mara kwa mara. Ninawashangaa wanaokiponda chuo manake without udom ndugu zetu wanaopata division three wangeponea wapi???
   
 6. B

  Bernard pius Member

  #6
  May 26, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watafaidi wanaosoma kabla majengo hayajakabidhiwa baada ya hapo ni matatizo tu
   
 7. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #7
  May 27, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  hlo nalo neno mkuu..
   
 8. Chief-Mkwawa

  Chief-Mkwawa Platinum Member

  #8
  May 28, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 17,788
  Likes Received: 7,109
  Trophy Points: 280
  mi sijui college nyengine but huku social hakuna ufa twalala kwa nafasi now twashkuru maji twapata block 1-5 ila kuna watanzania wana kasumba za kuponda, udom ina wanafunz 20,000 kati yao sidhan div 1 kama zafika hata 3000 wengi wetu ni div 2 na 3 za kumwagaaaa ambao hawa kama ni miaka 7 ilopita walikua hawapati chuo. Je tujiulize ni bora kusoma udom au kubaki home??????
   
Loading...