Kamanda
Senior Member
- Dec 5, 2007
- 150
- 176
Nimeona na kusikia. Nimesikitika sana baada ya wale wanaojiita watumishi wa Mungu kuibuka nao kuanza kumtetea Lowassa kwamba ni mtu safi, anaweza, mtendaji bora na mchapakazi mahiri. Hakika ni sifa nyingi zinazosambazwa sasa kama wanavyofanya waandishi wa habari waliolipwa ama na Lowassa mwenyewe au yule anayejiita mnyamwezi, mbunge wa huko ingawa ni Muiran, ambaye sisi tunamjua.
Sasa kwa kuchokoza tu hoja iliyo mbele yetu kwamba hata hao eti wachungaji wetu nao wamo. Nime-attach hapa kijisehemu cha ufisadi uliofanywa na KKKT kwenye baadhi ya miradi yake baada ya kupokea fedha za wafadhili na sadaka zetu kama ulivyofichuliwa na kampuni ya ukaguzi wa hesabu, ingawa hadi sasa wahusika, kama walivyo wa Richmond nao wanaendelea kutanua, tena mbaya zaidi wakiwa wamesimama kwenye madhabahu na kushika na kusoma Kitabu Kitakatifu- Biblia.
Endeleeni wana JF, mapambano ndiyo kwanza yameanza na sasa twaona njia bora ya kufikisha ujumbe ni hapa ndani ya nyumba, maana taarifa zingine vyombo vyetu vya habari vinaogopa.
Tuko pamoja. Nawaandalia ripoti kamili muda si muda, nachanja mbuga kuisaka na nyingine ya hivi karibuni kuhusu ufisadi ndani ya masinagogi yetu.