tufanye hivi kwa maliasili na urithi wote

Ngambo Ngali

JF-Expert Member
Apr 17, 2009
3,517
1,359
Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga (kushoto) akipokea kinyago cha kimakonde kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Ladislaus Komba. Kinyago hicho ambacho ni urithi wa sanaa ya nchi yetu kiliibwa na watu wasiojulikana katika ofisi za wizara ya Maliasili na Utalii na kuja kupatikana nchini Uswisi kwa msaada wa Polisi wa kimataifa (Interpol). Hafla hiyo imefanyika leo katika Makumbusho ya Taifa yaliyopo katika mtaa wa Shaban Robert jijini Dar

source: michuzi.blogspost.com

Wadau mnaonaje kama serikali ingekazana kurudisha maliasili zote zinazoibiwa na kupelekwa nje km dhahabu, almasi, uranium nk si tungekuwa mbali sana?????? Kwa nini tushupalie vitu symbolic na kuacha vitu material. Hii inaingia akilini kweli?
 
HII SASA AIBU! Hivi Kinyago hicho ambacho ni urithi wa sanaa ya nchi yetu ambacho kiliibwa na watu wasiojulikana katika ofisi za wizara ya Maliasili na Utalii na kuja kupatikana nchini Uswisi kwa msaada wa Polisi wa kimataifa (Interpol) Kilipitaje pitaje Air Port au Mipakani ?. Ina maana Hakuna Usalama wa taifa? Au usalama wa taifa ni kwa ajili ya kushulikia vyama vya upinzani tu?!
 
issue sio kilitokaje, kilitoka kama zinavyotoka almasi, dhahabu, mchanga wa dhahabu, wanyama wa loliondo etc Suala kubwa hapa ni kuwa wanahangaika na vitu ambavyo ni inconsequential kwa nini wasihangaikie urithi mwingine ambao ni tangible. Kama tukiweza kurudisha mali zetu zote zilizoibiwa bila shaka nchi hii itakuwa mbali na kima cha chini kitakuwa 500,000/=.
 
jana huyo mama akaniudhi sana eti hawawezi kurudisha ile mijusi yetu toka ujerumana

hao wajerumani waliipeleka mijusi hiyo kipindi cha mkoloni zamani kinyama leo hii sayansi na tech imejaa halafu anasema hawawezi
kuirejesha

kwa nini serikali isiwaamuru hao jamaa wakairudisha kwa gharam zao kwa kuwa imeshawaingizia pesa kibao

huyu mama mpuuzi sana
 
Hata mijusi ikirudi maisha ya mtanzania yatabadilika? Haitaongeza kilo ya nyama kwenye chungu cha mtanzania wa tandahimba au utete , wala haitaongeza mshahara wa mafanyakazi hata wa makumbusho sehemu ambapo mijusi na sanamu zinakaa. Hivyo vyote ni none issues mbona mali ya kweli inayotoroshwa hawachamgamkii wanachamgamkia vitu vya kipuuzi tu?
 
mnapokea vinyago tu na ile chenchi yetu ya rada tunitaka faster.nahao waliopeleka huko tunataka tuwaning'inize.tumechoka mali inapatikana mwizi haonekani tuwabne waswis watueleze si ndio tumewakuta na ngozi?
 
Back
Top Bottom