Tuepuke ajali za barabarani sambamba na ajali za mahusiano

Rationale

Member
Mar 13, 2021
24
98
Ukimpa mtu ufunguo wa gari, mtu asiyejua kuendesha gari na kisha umwambie aendeshe gari unadhani nini kitatokea? Ni dhahiri kwamba itatokea ajali, tena ajali mbaya, itakayomdhuru yeye mwenyewe na walio karibu na yeye na chombo chenyewe.

Mtu ambaye hajui kuendesha gari na anataka kuendesha gari anapaswa kufanya nini? Anapaswa kwenda shule kujifunza kuendesha gari au amtafute mtu (Mwalimu) ambaye atamfundisha kuendesha gari na kanuni zake, ili pamoja na mengineyo itamuepusha na ajali zisizo za lazima. Na bado hata akipata mafunzo hayo ya kuendesha gari, na hata akipata cheti, bado atahitaji mazoezi zaidi ili ajijengee uzoefu na umahiri wa kuwa barabarani.

Mahusiano ya kawaida ya kimapenzi hadi kufikia ndoa, ni sawasawa na mchakato wa kuendesha gari, kwamba ili uingie kwenye mahusiano LAZIMA upate aina fulani ya mafunzo ya msingi yatayokusaidia kumudu mahusiano yako, kwani sote kama tujuavyo kuna changamoto nyingi kwenye mahusiano ambazo bila mafunzo ni wazi kwamba tunakwenda kukumbana na ajali (ya kimahusiano).

Kuna watu, wako kwenye mahusiano, wanafurahia sana mahusiano yao kama vile wako peponi, lakini kuna wengine wako kwenye mahusiano lakini ni kama vile wako jehanamu, maana wanaishi na wenza wao kama maadui, na wanateseka hadi kupata msongo wa mawazo na vidonda vya tumbo, kwanini? ni kwasababu ya kukosa mafunzo na maarifa kuhusu mahusiano.

Mahusiano ya kawaida ya kimapenzi hadi kufikia ndoa ndio maisha yetu, hivyo tunaingiaje kwenye mahusiano KICHWAKICHWA, bila mafunzo!!? bila maarifa??!! ni wazi kabisa kwamba tunakwenda kukumbana na AJALI, tofauti ni kwamba haitakuwa ajali ya gari barabarani bali itakuwa ajali ya mahusiano.

Ili upate mafunzo bora kabisa ya mahusiano na uweze kukabiliana, kumudu, kuwa na amani, na hatimaye kufurahia mahusiano yako na mwenza wako, jipatie nakala yako ya kitabu cha Fungate ya Milele LEO, ni kitabu kitakachokupatia majibu yako yote kuhusu changamoto lukuki za mahusiano, ni kitabu kinachoainisha changamoto na ufumbuzi kuhusu mahusiano.

Kitabu kinapatikana kwa shilingi 20,000/= (Elfu ishirini) Kwa maelezo zaidi na jinsi ya kupata nakala yako wasiliana na mwandishi kwa nambari ya simu 0784 607524.

Hakika hutajutia uamuzi wako.
 
Back
Top Bottom