Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 15,338
- 9,766
Ndugu zangu watanzania zoezi la Sensa limeanza Leo na litaendelea katika wiki yote hii, Najuwa Kuna ambao hatujabahatika kufikiwa na makarani wa Sensa katika siku ya leo, ndugu zangu naomba tutambue kuwa sote tutafikiwa na kuhesabiwa bila kuachwa Wala kurukwa kaya yoyote Ile
Ndugu zangu pamoja na kuwa Mimi siyo kiongozi Wala karani wa Sensa lakini Kama kijana na mpenda nchi yangu napenda kuwasihi nanyi ndugu zangu kuwa Tuwe na Subira na tuhakikishe kuwa tunakuwepo au anakuwepo mtu atakaye toa ushirikiano wa taarifa kwa karani wa Sensa atakapo pita
Tukumbuke kuwa zoezi hili limetumia mfumo mpya, kwa Mara ya kwanza makarani wamepewa vishikwambi,hivyo changamoto za hapa na pale haziwezi kukosekana,
Mimi moyo wangu umewiwa kumsaidia mh Rais kuwaelemisha watu juu ya umuhimu wa Sensa hasa majirani zangu ambao tulikaa kusubiri makarani, nimefanya hivyo hata kabla ya zoezi hili kuanza siku ya leo,
Tuhesabiwe wote ili Tumpe picha mh Rais wetu ya uhalisia wa Taifa analoliongoza, ili ajuwe afanye Nini na wapi, ajuwe Ni wapi apeleke huduma zaidi, Ni wapi asogeze huduma kupunguza adha kwa wananchi, ajuwe Hali yetu ya kiuchumi Sisi watanzania, ajuwe Ni vipi kundi fulani lipewe kipaombele
Sisi vijana ndio tunatakiwa Tuwe msitari wa mbele kuhamasisha watu wahesabiwe ili mh Rais wetu ajuwe Ni vipi atunge Sera na Sheria za kutusaidia sisi vijana wake, Sote tunatambua adhima na dhamira ya mh Rais wetu ya kutaka kujenga Taifa na uchumi utakao mgusa kila mtu, niwajibu wetu kumuonyesha Hali ya vipato vyetu watanzania ili ajuwe afanye Nini kutusaidia sisi
Natamanii hata ningepita Tanzania nzima kaya kwa kaya kuhamasisha watu wahesabiwe lakini uwezo wangu hauniluhusu kufanya hivyo, ndio maana natumia jukwaa hili kuwaomba watanzania wenzangu tuhesabiwe
Mimi Lucas Mwashambwa nipo Tayari Kuhesabiwa, Nawe pia mtanzania mwenzangu jiandae kuhesabiwa ili keki ya Taifa igawanywe kwa usawa na kwa makundi yote na kwa maeneo yote bila kuachwa mtu nyuma au pembeni ya meza ya Taifa