TUCTA yawakataa CUF, NCCR | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TUCTA yawakataa CUF, NCCR

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 8, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 8, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  WAKATI Chama cha Wananchi (CUF) na NCCR -Mageuzi wakithibitisha kushiriki maandamano yaliyoandaliwa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) ya kupinga ongezeko la bei ya umeme Katibu Mkuu wa shirikisho hilo Nicholas Mgaya amewakana.

  Akizungumza katika kipindi cha asubuhi kinachorushwa na televisheni ya Chanel Ten alisema shirikisho hilo halina haja na kufanya maandamano na chama chochote cha siasa na kwamba TUCTA wenyewe wanajuana.

  Alisema hii hoja inawaumiza Watanzania wote lengo ni kuitaka serikali kusikiliza kilio cha watanzania kupitia wafanyakazi lakini halitakiwi kuwa la kisiasa zaidi kama vyama vinataka kuandamana basi viandae maandamano yao.

  “Sisi hatuhitaji maandamano yetu kushirikisha vyama vya siasa si CUF, CHADEMA, NCCR, TLP wala chama chochote hatukihitaji bali tunahitaji wanachama wa shirikisho hilo tu na kwamba wenyewe tunajuana,” alisema Mgaya.

  Mgaya alisema wao wanataka kufanya maandamano ya amani lengo likiwa ni kupinga kupanda kwa bei ya umeme ambayo itasababisha ugumu wa maisha uliopo sasa kutokana na hata wafanyakazi wenyewe kupata mshahara usio kidhi mahitaji yao.

  Alisema umeme unategemewa katika kukuza uchumi wa taifa na hata uchumi wa mtu binafsi hivyo ni lazima serikali ikafanya jitihada zozote za kutumia vyanzo mbalimbali vya maji ili kuweza kufanya upatikanaji wa umeme kuwa wa uraisi zaidi.

  Akizungumzia kuhusiana na kusikilizwa mahitajio yao ambayo kwa mwaka 2010 walidaiwa kupamba vyombo vya habari kwa maandamano kila kukicha alisema bado hayajatatuliwa ila wanaahidiwa ahadi nyingine mpya na serikali.

  Alisema kwa sasa ana imani kubwa na waziri aliyepo kwa kuwa ameonesha nia ya kuwasaidia kutokana na ziara zake mbalimbali alizozifanya na kukutana na viongozi kadhaa wa shirikisho hilo na kufanya mazungumzo nao.

  “Sisi tunapenda kufanya kazi na viongozi wanaojali watu wanaowatumikia kwa sasa waziri ameanza vizuri na mwaka huu hatutarajii yatokee yaliyotokea mwaka jana kwa kuwa tayari tumekaa na waziri pamoja tumezungumza naye hivyo mwaka huu tunatarajia kuona mafanikio kwetu ya tuliyokuwa tunaahidiwa tangu malalamiko yetu yapelekwe serikalini,” alisema Magaya.
   
 2. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2011
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  CUF,NCCR wamedandia trenj kwa mbele ha ha ha...safi sana Mgaya maana mngeacha bila kutia neno nina uhakika CCM kwa kutumia vyombo vyake(jeshi la polisi etc) ingekuja na taarifa za ki-intelegisia juu ya maandamao yenu...siku hizi ukitaka kusimamisha maandamano ni rahisi tu..."tumepata taarifa za ki-intelegisia"...ha ha ha..bongo tambarare!
   
 3. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Kwa iyo TUCTA yawakataa NCCR na CUF tu? vyama vingine wanavítaka? ebu tuambíe vizuri tujue..
   
 4. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #4
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Hawa watu Pumba sana, Sisi shida yetu ni kilio chetu kisikike.... hata wakiandamana na bata, paka na mbwa.... haya mambo ya kukataana hayana tija...... we dont care about the means so long as the end is reached.
   
 5. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #5
  Jan 9, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  kwakuwa wote wataathirika na ongezeko la umeme, kusiwe na watu flan kutaka kufanya maandamano hayo yakisiasa zaidi bali, yawe ya kijamii zaidi.
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Jan 9, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,812
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa vipi? Kwani watu wa CUF, NCCR au chama chochote kile cha siasa hawaathiriki na ongezeko kubwa la bei ya umeme? :faint2:
   
Loading...