TUCTA: Kiwango cha chini cha mshahara kiwe Tsh. 1,010,000

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Katika siku ya wafanyakazi duniani TUCTA wamesema mapendekezo yao mara nyingi yamekuwa hayakubaliki na serikali na hivyo kiwango cha chini kimekuwa duni kwa watumishi wa serikali na binafsi.

Mathalani kwa sasa kima cha chini cha mtumishi wa serikali ni Tsh. 315,000 kiasi ambacho hakiendani na maisha halisi hivyo inawafanya watumishi waishi maisha duni.

Katibu wa TUCTA amesema kiwango kinachopendekezwa ni Tsh. 1,010,000 kwa watumishi wa serikali ili waweze kumudu maisha

====
Wakiwasilisha hotuba yao katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi mbele ya Rais Samia Suhumu, TUCTA imependekeza kiwango hicho ili kiwezesha Wafanyakazi na wategemezi wao kuishi

Wamesema kima cha chini cha misharaha kimendelea kuwa duni licha ya gharama za maisha, mathalani kwa sekta binafsi kwa watumishi wa majumbani ni Tsh. 40,000/- hadi Tsh. 60,000/-. Kwa wafanyakazi wa Umma kima cha chini ni Tsh. 315,000/-

Wameeleza kuwa Wafanyakazi hawajaongezwa mishahara kwa miaka 9 kwa sekta binafsi na miaka 7 kwa sekta za Umma hali iliyosababisha kupungua hari ya kufanya kazi ka kupunguza ufanisi mahali pa Kazi

Wameomba hivyo kwa kuzingatia kuwa mishahara haijapanda kwa kipindi kirefu, wakati gharama za maisha zikiendelea kupanda na bei za bidhaa kama chakula na mahitaji mengine ya msingi sambamba na mfumuko wa bei
 
Ahahahah nimecheka, serikali hawawezi wapea iyo amount.

Sema hotuba yake yote imejaa kuomba mshahara, wanasahau kuomba pia mazingira bora ya kufanyia kazi.

Ukiingia ofisi za kiserikali miundo mbinu ni mibovu” office appliances”, karatasi zimejaa kila meza. Kikubwa tafrani
 
1.1 mil sidhani kama itapita kwa serikali hii kwa sasa bado sana
 
Matawi ya CCM hayo. Baada ya maadhimisho, wanakutana na viongozi wao wa CCM na kunywa mvinyo! Huku wafanyakazi wakiendelea kutaabika.
Umifika uchaguzi ,hao waganga wanapewa 20,000/ili wageuze matokeo.
Hii ndi ghalama wanayoilipa.
 
Kwa wafanyakazi hawa tulionao, ni upuuzi tu kwa serikali kuwapa hizo hela.

Unaenda ofisi ya mtu jambo dogo tu,utatumia wiki kadhaa kufuatilia.

Ukutr kuna ujio wa rais, basi kila mtu anakwambia wapo kwenye maandalizi ya upokezi wa rais.

Labda tutafute namna nzuri ya kuwatambua wafanyaji kazi bora na wewe recognized vizuri kuliko serikali kujipa gharama kubwa.
 
Katika siku ya wafanyakazi duniani TUCTA wamesema mapendekezo yao mara nyingi yamekuwa hayakubaliki na serikali na hivyo kiwango cha chini kimekuwa duni kwa watumishi wa serikali na binafsi.

Mathalani kwa sasa kima cha chini cha mtumishi wa serikali ni Tsh. 315,000 kiasi ambacho hakiendani na maisha halisi hivyo inawafanya watumishi waishi maisha duni.

Katibu wa TUCTA amesema kiwango kinachopendekezwa ni Tsh. 1,010,000 kwa watumishi wa serikali ili waweze kumudu maisha

====
Wakiwasilisha hotuba yao katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi mbele ya Rais Samia Suhumu, TUCTA imependekeza kiwango hicho ili kiwezesha Wafanyakazi na wategemezi wao kuishi

Wamesema kima cha chini cha misharaha kimendelea kuwa duni licha ya gharama za maisha, mathalani kwa sekta binafsi kwa watumishi wa majumbani ni Tsh. 40,000/- hadi Tsh. 60,000/-. Kwa wafanyakazi wa Umma kima cha chini ni Tsh. 300,000/-

Wameeleza kuwa Wafanyakazi hawajaongezwa mishahara kwa miaka 9 kwa sekta binafsi na miaka 7 kwa sekta za Umma hali iliyosababisha kupungua hari ya kufanya kazi ka kupunguza ufanisi mahali pa Kazi

Wameomba hivyo kwa kuzingatia kuwa mishahara haijapanda kwa kipindi kirefu, wakati gharama za maisha zikiendelea kupanda na bei za bidhaa kama chakula na mahitaji mengine ya msingi sambamba na mfumuko wa bei
Inawezekana kabisa.
 
Kwa wafanyakazi hawa tulionao, ni upuuzi tu kwa serikali kuwapa hizo hela.

Unaenda ofisi ya mtu jambo dogo tu,utatumia wiki kadhaa kufuatilia.

Ukutr kuna ujio wa rais, basi kila mtu anakwambia wapo kwenye maandalizi ya upokezi wa rais.

Labda tutafute namna nzuri ya kuwatambua wafanyaji kazi bora na wewe recognized vizuri kuliko serikali kujipa gharama kubwa.
Wivu humuua mtu mjinga!!
 
Wafanyakazi wa Tanzania wengi ni useless na zero brains tu !

Wengi wanalipwa kwa kuwa maeneo ya kazi na si kwa kazi wazifanyazo!

Kama ambavyo huwa anasema Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Anthony Mtaka,wengi siyo wabunifu na hawana chochote cha maana cha kuonyesha!

Utakuta watu wamezaja mavyeti hadi PhD lakini hakuna cha maana wanachoweza kukuonyesha zaidi ya umasikini wa Wananchi wanaowahudumia.

Mimi nadhani ajira siyo birth right kwao, kama wanaona mishahara haitoshi watafute shughuli zingine wakafanye!

Yaani Watanzania tujichange tupate Tshs.1.5 trilioni kwa mwezi halafu Tshs.1 trillion itumike kulipa mishahara kwa watu laki 4 ambao uzalishaji wao in doubtful?!
Hiyo itakuwa akili au matope?!
 
Back
Top Bottom