Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Katika siku ya wafanyakazi duniani TUCTA wamesema mapendekezo yao mara nyingi yamekuwa hayakubaliki na serikali na hivyo kiwango cha chini kimekuwa duni kwa watumishi wa serikali na binafsi.
Mathalani kwa sasa kima cha chini cha mtumishi wa serikali ni Tsh. 315,000 kiasi ambacho hakiendani na maisha halisi hivyo inawafanya watumishi waishi maisha duni.
Katibu wa TUCTA amesema kiwango kinachopendekezwa ni Tsh. 1,010,000 kwa watumishi wa serikali ili waweze kumudu maisha
====
Wakiwasilisha hotuba yao katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi mbele ya Rais Samia Suhumu, TUCTA imependekeza kiwango hicho ili kiwezesha Wafanyakazi na wategemezi wao kuishi
Wamesema kima cha chini cha misharaha kimendelea kuwa duni licha ya gharama za maisha, mathalani kwa sekta binafsi kwa watumishi wa majumbani ni Tsh. 40,000/- hadi Tsh. 60,000/-. Kwa wafanyakazi wa Umma kima cha chini ni Tsh. 315,000/-
Wameeleza kuwa Wafanyakazi hawajaongezwa mishahara kwa miaka 9 kwa sekta binafsi na miaka 7 kwa sekta za Umma hali iliyosababisha kupungua hari ya kufanya kazi ka kupunguza ufanisi mahali pa Kazi
Wameomba hivyo kwa kuzingatia kuwa mishahara haijapanda kwa kipindi kirefu, wakati gharama za maisha zikiendelea kupanda na bei za bidhaa kama chakula na mahitaji mengine ya msingi sambamba na mfumuko wa bei