TUCTA: Kima cha chini cha mshahara kiwe 970,000

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Kaimu Katibu Mkuu wa TUCTA amesema wamefanya tafiti kubaini kiwango cha mshahara ambacho kinaweza kumtosha mtumishi kuendesha maisha yake.

Kutokana na Tafiti yao wamependekeza kiwango cha chini mshahara kiwe Tsh. 970,000 kutokana na gharama za maisha za sasa.

Hayo yamesemwa siku ya maadhimisho ya siku ya wafanyakazi ambayo kitaifa yamefanyika katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

IMG_20210501_161120_020.jpg

Pia soma: LIVE - Mei Mosi Mwanza: Rais Samia ahutubia, aahidi kuongeza mishahara kuanzia mwakani
 
Kaimu Katibu Mkuu wa TUCTA amesema wamefanya tafiti kubaini kiwango cha mshahara ambacho kinaweza kumtosha mtumishi kuendesha maisha yake

Kutokana na Tafiti yao wamependekeza kiwango cha chini mshahara kiwe Tsh. 970,000 kutokana na gharama za maisha za sasa

Hayo yamesemwa siku ya maadhimisho ya siku ya wafanyakazi ambayo kitaifa yamefanyika katika ukumbi wa CCM Kirumba Mwanza

Mtumishi yupi?
 
Hii ni nchi TAJIRI. Kwhy kima cha chini cha mshahara (KCCM) kiwe sawa na mshahara wa mbunge mwenye elimu ya darasa la Saba kfn Kibajaji au Msukuma, 2m/- kwa mwezi.
 
Waliwahi kupambania sh 350,000 ndo iwe kima cha chini kwa miaka takribani yote ya Mkwere, wakashindwa. Ebu fikiria walishindwa kumshawishi mkwere kuidhinisha hiyo 350,000, kwa jiwe walipendekeza kweli? Ngapi?

970,000 kwa mtu wa idara gani sasa? Wakisema Tanesco, sitashangaa ila wa wizarani nitasita kidogo.

Waache kuwaibia wafanyakazi, watengeneze tu chama cha siasa
 
Watumishi wa umma wanajiona kama wapo wenyewe tu sijui hawajui ni 0.6% ya raia wote? Huu upuuzi wa kudai laki 9.7 ni Seriikali gani hii itakayolipa hyo pesa? Hv wanajua impact ya mshahara kupanda huku mitaani ?
 
Back
Top Bottom