Mrimi
JF-Expert Member
- Jul 18, 2011
- 1,691
- 635
Wanajamii siku zote ukombozi unaanza na watu wachache wenye nia thabiti. Si kawaida umma wote kuamka mara moja na kudai ukombozi.
Nimefikiria hili vuguvugu la ukombozi linaloanza taratibu linaweza likazimwa kirahisi tu endapo watawala wataamua kutumia kale kautaratibu kao ka siku zote kapropaganda. Sote tunajua silaha yao ni kutugawa kisha wanatutawala.
Tukumbuke sisi ambao tuna access ya information tuko wachache sana, wengi wetu tupo mijini. Lkn watanzania wengi wapo vijijini. Ukifanya utafiti wa uelewa wa watu hawa juu ya katiba hawana.Sasa mimi naona hali hiyo ni silaha tosha ya watawala ktk kushinda vita hii. Wakati umefika sasa lianzishwe vuguvugu litakalopenya hadi vijijini ili watu wetu wafahau haki zao na nafasi yao katika kuzipigania. Sote tunajua watu wanavyoteseka huko, wanahitaji ukombozi.
Kitu ninachoona hapa ni kwamba watawala watatema sumu yao ya propaganda kwa kusema vuguvugu hili ni uvunjaji wa amani kama ambavyo wamekuwa wakidhihaki maandano siku zote. Watawarubuni baadhi ya wanaharakati wenye njaa, wengine watakamatwa na hata wengine watauawa. Hii ikitokea wengine watavunjika moyo na ku give up. Watawala watakuwa wameshinda vita hii nasi tutabaki kuwa watu dhalili miaka yote.
Kimsingi tunahitaji watu wa vijijini. Hii ndiyo silaha pekee waliyobakinayo watawala hawa, sote tunaona Arusha, Mbeya, Mwanza, Moshi Kigoma,Dar.nk. zinavyowahangaisha, sasa tunatakiwa kuzama ndani kwenye mizizi. Kiukweli tusipopata support ya wanavijiji, mi naona bado vita hii kuishida ni vigumu.
Nawasilisha....