Tuambie jinsi ulivyompata mwenzi wako

Tuambie jinsi ulivyompata mwenzi wako

Incidents Kama hizi zipo. Lkn kwa hii yako umetudanganya.

14years? How come? May be ulitaka KUANDIKWA 4 years.

Actually ww Ni mtunzi Bora ukiacha uwongo
 
😂😂😂 hiyo miaka 14 nyuma wenzetu mlikuwa mnatumiana kwa Mpesa ipi jamani daaah chai ya mchana hii😂😂😂
 
Nimejikuta nacheka tu mkuu [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Keyboard hizi haziaminiki mkuu.... Unaweza kuta una miaka 10 ya ndoa na watoto 3 mkuu

Keyboard yangu haidanganyi namna hiyo.....acha niendeele kutuma application wewe unaoneka unaye.
 
Nawe pia usisahau kumuomba hakuna aijuaye kesho..huenda ukajileta mwenyewe PM ni kwangu.
Hahahaaaaha Amen mkuu by the way haya mambo hayatabiriki naheshimu kila eneo nililopo na kila aliyepo...

Si kwa ajili ya mahusiano tu hata maisha mengine mkuu, afya, kazi, ushauri n.k kwa hivyo usijali mkuu...
 
Km mna miaka 14 ni sawa kabisa coz nimeshangaa eti Kodi tabata 120000 ..nyumba yenye ( jiko seble na chumba ) afu iwe mpya ...kwa miaka hii hupati
Habari wanajamvi heri ya mwaka 2020

Kwa wale ealiona wenzi wenu tuambie ulipataje najua wangine walisota sana wengine kama walisuka mlevi shimoni na nk.

Mimi binafsi ilikuwa hivi, nilikuwa kwenye harakati za kutafuta nyumba maeneo ya Tabata baada ya kuchoka maisha ya sinza nilipata nyumba yenye sebule, kajiko kadogo , chumba na washing room kwa ilikuwa nyumba mpya haijawahi kukaliwa na mtu, mwenye nyumba alikuwa anataka 120,000 kwa mwezi nikasema poa ingawa bajeti yangu ilikuwa laki, mwenye nyumba alikuwa ni mama wa kichaga alikuwa anaishi Moshi tukakubaliana nimtumie hela kwenye simu yake tulikubaliana nilipe kodi ya miezi sita 720,000.

Kwenye harakati za kutuma hela nikakosea namba ya kutuma ikaenda kwa mtu mwingine nilipagawa hiyo siku ilikuwa mbaya sana kwangu nikawa nawapigia voda huku natetemeka hawapoke kipindi basi ikabidi nipige hiyo namba niliyokosea akapokea sauti ya Dada mmoja nikajieleza huku natia huruma nikimsihi sana anirudidishe, nilimueleza ilikuwa ni kodi ya nyumba tena niliikopa, dada alinijibu usijali nitakurudishia.

Mungu mkubwa alinirudishia hela yangu yote bila kujali makato ya ada ya kutuma kwakweli sikuamini nilimshukuru sana, baada ya hapo tukaanza kuwasiliana kwa ukaribu ilichukuwa miezi mnne tunawailiana tu kwa simu kila tukipanga kuonana nilikuwa na sita kwakuwa nilikuwa na mtu mwingine mkoani ingawa hatukuwa serious sana.

Siku moja walipata msiba wa baba wa mmoja wa staff mwenzao suku ya kuaga ndiyo ilikuwa siku pia tulipanga kuonana basi tukakubaliana tukutane mahali then nimsindikize kwenye msiba nikasema sawa, niseme tu siku hiyo nilikuwa na mchanganyiko wa feelings kama hofu, raha kimuhemuhe nk halahaula nilipo muona tu moyoni nilisema huyu ndiyo atakuwa mke wangu tulikumbatiana kwa hisia kali sana mpaka watu walitushangaa..basi tukaa kwa dakika chache then tukaenda msibani kuaga baada ya hapo tulienda kukaa mahali tukaongea sana kila mtu alikuwa yupo tayari kufunguka nilimtamkia siku hiyo kuwa wewe utakuwa mke wangu na akawa hivyo.

Sasa ni familia ya watoto wawili me na ke miaka 14 ya ndoa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom