Tuambie huko kwenu nafaka kama mahindi wanauza Tsh ngapi?

Sio dhamira yake kuu! Dhamira yake kuu ni kujua sehemu ulipo mazao hayo ni bei gani na kama mtu anaweza kununua anunue kutoka sehemu ambayo mazao hayo anaona yatamlipa!
Mkuu najua vizuri kabisa huu mjadala kulingana heading yake unaweza kutoa fursa nyingi za kibiashara lakini kwa hizo bei 2000 napata mashaka juu ya dhamira ya mtoa mada,,, anyway sio mbaya huku ulipo ni fursa nzuri kwa wafanya biashara was mahindi!!! Kanda ya ziwa utauza av. 8000
 
Hivi jiwe anafanya kazi ya kuwatetea wanyonge wa nchi gani? Mbona uti wa mgongo wa nchi unapuuzwa kibabe? Enzi za kikwete gunia la mahindi kwa bei ya chini ilikuwa 50000+tsh
 
Hivi jiwe anafanya kazi ya kuwatetea wanyonge wa nchi gani? Mbona uti wa mgongo wa nchi unapuuzwa kibabe? Enzi za kikwete gunia la mahindi kwa bei ya chini ilikuwa 50000+tsh
Labda tujue wanaofadika kwa bei ya mahindi kuwa chini (kupata chakula kwa urahisi) na wenye mahindi wapi wengi?

Na wapi ni wanyonge?

Mi naona wanyonge wametetewa, ungekumbuka kilo ya unga ilivofika 2300 wanyongewalivyopata tabu, wala usingeandika hii coment yako.
 
Daah 2000 haitoshi hata nusu ya nyama.
Mkulima ili ale kilo ya nyama inabidi auze debe 4 za Mahindi.
Hadi nasikia huruma, kulima panachosha sana na returns ndiyo kama hizi haziridhishi.
Sidhani kama ni kweli tusingekuwa tunanunua kilo ya sembe kwa tshs1200
 
Kaka sipo kisiasa
Nakukumbush wanyonge ndio wakulima wa mahindi na ndio wanaouziwa mbolea kwa bei aghali mno! Bei ya mbolea ingekuwa ipo chini kweli tungeafiki.......ila hali hii inakatisha tamaa juhudi za wanyonge kujikwamuA kwenye umasikini kwa kutumia kilimo.
Labda tujue wanaofadika kwa bei ya mahindi kuwa chini (kupata chakula kwa urahisi) na wenye mahindi wapi wengi?

Na wapi ni wanyonge?

Mi naona wanyonge wametetewa, ungekumbuka kilo ya unga ilivofika 2300 wanyongewalivyopata tabu, wala usingeandika hii coment yako.
 
Serikali mbona ilisha
Huku kwetu mahindi debe 1 ni Tsh 2000/=
Mchele super debe ni Tsh 25000/=

Serikali ifungue mipaka vinginevyo wakulima hata mitaji ya kununua mbolea itakuwa shida!
Au
Serikali ikimaliza kununua korosho inunue na nafaka hizo zingine.
Serikali mbona ilishafungua mipaka coz kuna ki-crip nilikiona cha waziri mwenye dhjamana na Kilimo akisema "serekeli" haijazuia kuuza mazao ya kilimo nje ya TiiZii..
N way Jembe halimtupi mkulima
 
Labda tujue wanaofadika kwa bei ya mahindi kuwa chini (kupata chakula kwa urahisi) na wenye mahindi wapi wengi?

Na wapi ni wanyonge?

Mi naona wanyonge wametetewa, ungekumbuka kilo ya unga ilivofika 2300 wanyongewalivyopata tabu, wala usingeandika hii coment yako.
Nilitegemea uje na point labda ya kushusha pembejeo za Kilimo ila kama pembejeo ziko Juu huku bei ya mazao ipo chini kiasi hicho sioni unafuu kwa maskini huu utawala.

Mbolea ya kupandia kg50 ni zaidi ya 50000tsh huku gunia la mahindi 20000, hapo bado other investment cost, kama kuandaa shamba, kulima, kununua mbegu, kupanda, kupalilia, kuvuna, kupiga, store alafu uuze gunia 20000au 18000. Hapo huoni shida ipoje Mkuu?

We bilashaka umezaliwa familia ya Mboga 7 hujui adha ya wakulima wanayopitia. Hongera kuzaliwa pema penye neema.
 
Unalinganisha bei ya gunia la mahindi na bei ya mfuko wa mbolea,
Unajua hizo kg 50 zinatosha kwa shamba ukubwa gani?
Na huo ukubwa unaweza kutoa wastani wa gunia ngapi?
 
Ndugu unaweza kunisaidia kujibu maswali haya:
1. Hiyo bei ya 18,000/= kwa gunia la kilo 100 inajumuisha na bei ya gunia au gunia mnunuzi unanunua kivyake? Na bei ya gunia tupu ni kiasi gani?
2. Gharama za chini kabisa za kusafirisha tani 50 (gunia 500 za kilo 100 kila moja) za mahindi kutoka Sumbawanga au Songea hadi Dar ni kama kiasi gani?
3. Gharama za kupakia na kupakua ni kama kiasi gani kwa gunia moja?
4. Muda ambao mahindi yanaweza kuhifadhiwa bila kuharibika.
5. Aina nzuri ya dawa ya kuweka kwenye mahindi ili yasiharibike ni ipi? Utaratibu wake wa kuwekwa kwenye mahindi ambayo yameshapakiwa kwenye magunia ni upi yaani iwekwe kila baada ya muda gani?
6. Kutoka Sumbawanga au Songea hadi Dar gari linatumia muda gani?
7. Mbali na Sumbawanga au Songea ni sehemu gani nyingine ya karibu na Dar ambako mahindi yanaweza kupatikana kwa urahisi na kwa bei kama hiyo ya Sumbawanga au Songea?
8. Ni gharama gani zingine zinazohusiana na usafirishaji wa mahindi kiasi hicho kutoka katika maeneo hayo niliyoyataja hadi Dar?

Nitashukuru nikipata jibu swali kwa swali
7-KIBAIGWA
 
Huku kwetu mahindi debe 1 ni Tsh 2000/=
Mchele super debe ni Tsh 25000/=

Serikali ifungue mipaka vinginevyo wakulima hata mitaji ya kununua mbolea itakuwa shida!
Au
Serikali ikimaliza kununua korosho inunue na nafaka hizo zingine.
Korosho hujasikia imeshindwa kununua sasa wanatisha wafanyabiashara wanunue kwa lazima.
 
Haya ndiyo manufaa ya upinzani, kwa pamoja mlipiga kelele kwamba kuna njaa.. JPM akawaambia Hakuna na Njaa.. na haipo kweli!
 
Huku kwetu mahindi debe 1 ni Tsh 2000/=
Mchele super debe ni Tsh 25000/=

Serikali ifungue mipaka vinginevyo wakulima hata mitaji ya kununua mbolea itakuwa shida!
Au
Serikali ikimaliza kununua korosho inunue na nafaka hizo zingine.
kwenu sh ngapi?
 
Back
Top Bottom