Tuambie huko kwenu nafaka kama mahindi wanauza Tsh ngapi?

Daah 2000 haitoshi hata nusu ya nyama.
Mkulima ili ale kilo ya nyama inabidi auze debe 4 za Mahindi.
Hadi nasikia huruma, kulima panachosha sana na returns ndiyo kama hizi haziridhishi.
 
Daah 2000 haitoshi hata nusu ya nyama.
Mkulima ili ale kilo ya nyama inabidi auze debe 4 za Mahindi.
Hadi nasikia huruma, kulima panachosha sana na returns ndiyo kama hizi haziridhishi.
Panachosha mno aisee
Ili upate mfuko wa mbolea mmoja inabidi uuze debe zisizopungua 30 za mahindi ndio utapata mbolea.
 
Huku kwetu mahindi debe 1 ni Tsh 2000/=
Mchele super debe ni Tsh 25000/=

Serikali ifungue mipaka vinginevyo wakulima hata mitaji ya kununua mbolea itakuwa shida!
Au
Serikali ikimaliza kununua korosho inunue na nafaka hizo zingine.
Wapi huko mkuu
 
Gunia la kg 100,kwenye Soko la mahindi,SODECO,mjini songea ni sh.18,000/
 
Huku ni 8500/=, tulime mazao ya biashara kama tunalenga kukuza uchumi, mahindi na nafaka zingne zibaki kwa matumizi ya chakula, mimi kama mlaji hiyo bei iko vizuri
 
Gunia la kg 100,kwenye Soko la mahindi,SODECO,mjini songea ni sh.18,000/
Ndugu unaweza kunisaidia kujibu maswali haya:
1. Hiyo bei ya 18,000/= kwa gunia la kilo 100 inajumuisha na bei ya gunia au gunia mnunuzi unanunua kivyake? Na bei ya gunia tupu ni kiasi gani?
2. Gharama za chini kabisa za kusafirisha tani 50 (gunia 500 za kilo 100 kila moja) za mahindi kutoka Sumbawanga au Songea hadi Dar ni kama kiasi gani?
3. Gharama za kupakia na kupakua ni kama kiasi gani kwa gunia moja?
4. Muda ambao mahindi yanaweza kuhifadhiwa bila kuharibika.
5. Aina nzuri ya dawa ya kuweka kwenye mahindi ili yasiharibike ni ipi? Utaratibu wake wa kuwekwa kwenye mahindi ambayo yameshapakiwa kwenye magunia ni upi yaani iwekwe kila baada ya muda gani?
6. Kutoka Sumbawanga au Songea hadi Dar gari linatumia muda gani?
7. Mbali na Sumbawanga au Songea ni sehemu gani nyingine ya karibu na Dar ambako mahindi yanaweza kupatikana kwa urahisi na kwa bei kama hiyo ya Sumbawanga au Songea?
8. Ni gharama gani zingine zinazohusiana na usafirishaji wa mahindi kiasi hicho kutoka katika maeneo hayo niliyoyataja hadi Dar?

Nitashukuru nikipata jibu swali kwa swali
 
Wapi huko?
Je mazao ya biashara ni yapi ambayo yapo juu?
Huku ni 8500/=, tulime mazao ya biashara kama tunalenga kukuza uchumi, mahindi na nafaka zingne zibaki kwa matumizi ya chakula, mimi kama mlaji hiyo bei iko vizuri
 
Huu Uzi una kila dalili ya uchonganishi/uchokozi/kukatishana tamaa,,,,
MWISHO!
Sio dhamira yake kuu! Dhamira yake kuu ni kujua sehemu ulipo mazao hayo ni bei gani na kama mtu anaweza kununua anunue kutoka sehemu ambayo mazao hayo anaona yatamlipa!
 
Back
Top Bottom