#COVID19 Tuache upotoshaji kuhusu chanjo ya Corona

Gift mzalendo

JF-Expert Member
Dec 13, 2019
1,006
1,170
Kuna "misconceptions" nyingi kuhusu chanjo ya Covid19. Baadhi za kitabibu na nyingine za elimu ya tabia. Zile za kitabibu nawaachia madaktari na wataalamu wa afya wazijibie. Mimi najibu hizi ambazo ni Socio-Cultural infuenced.

1. Chanjo ya Corona ni mpango wa wazungu kutuua?

JIBU: Wazungu wangetaka kutuua wana njia nyingi za kutumia. 90% ya madawa na vifaa tiba tunavyotumia vimetoka nje. Kuanzia MRI na CT scan ya Muhimbili, hadi dawa ya panadol pale zahanati ya Nanjilinji vimetoka kwa mabeberu. Kwanini wasitumie njia hizo ambazo ni rahisi zaidi kutumaliza badala ya chanjo ya Corona?

Hata hivyo kuna chanjo nyingi sana tunazitumia kutoka kwa hao tunaowaita mabeberu. Mtoto akizaliwa hadi anapofikisha umri wa miaka mitano anachomwa jumla ya chanjo 13 za aina tofauti. Na hakuna hata moja tunayotengeneza sisi. Zote tunapewa msaada na mabeberu. Je wangekua na nia ya kutumaliza si wangesubiri chanjo ya Corona?

2. Kwanini chanjo ya Corona inatolewa bure?

JIBU: Ni chanjo ipi inatolewa hapa nchini kwa kulipiwa? Mbona hujahoji kwanini chanjo ya pepopunda, polio, tetekuwanga, homa ya ini zinatolewa bure, badala yake unahoji chanjo ya Corona tu? Halafu pia kwanini hauulizi mbona ARVs zinatolewa bure?

Je ungetakiwa kulipia ungeweza? Au serikali yako ingeweza kukununulia? Kwa mfano dozi ya mwezi ya ARVs ni kati ya $170 hadi $220 yani kati ya shilingi laki 4 hadi laki 5. Kwahiyo kama umeathirika na VVU kila unapoenda CTC kuchukua dawa kuna "mabeberu" wamekulipia laki 4 kila mwezi. Je serikali ya Tanzania ingeambiwa ikulipie ingeweza? Same applies to Corona vaccine.

3. Kwanini tusitengeneze chanjo yetu?

JIBU: Hata mimi natamani hivyo, lakini hatuwezi kwa sababu zilezile za History ya Form 2B. Poor technology, lack of capital, poor government support etc. Kama toothpick na toilet papers tunaagiza China, je tunaweza kutengeneza chanjo ya Corona?

Serikali haijawa na nia ya dhati ya kufanya uwekezaji wa wataalamu, teknolojia, na fedha. Tukiamua tunaweza. Lakini kabla ya kufikiria kutengeneza chanjo ya Corona tujiulize nini kimetushinda kutengeneza chanjo zingine kama ya polio, tetekuwanga, homa ya ini etc? Jibu utakalolipata lihamishie kwenye Corona.

4. Chanjo ya Corona imetumia muda mfupi kupatikana kwa hiyo ni feki.

JIBU: Muda wa chanjo kupatikana sio kigezo pekee cha ubora wa chanjo. Zipo chanjo nyingi zilizopatikana kwa muda mfupi na zikaonesha ufanisi mkubwa. Chanjo ya Corona imetumia miaka miwili, lakini chanjo ya matumbwitumbwi (mumps) ilitumia miezi 11 na mpaka leo inatumika.

5. Chanjo zinazotumika Ulaya sio hizi tunazoletewa Afrika.

JIBU: Sio chanjo ya Corona tu, hata ARVs tunazotumia Afrika sio zinazotumika Ulaya. Hata Toyota unayoendesha Afrika sio Toyota inayouzwa Ulaya. Kwahiyo kama unadoubt chanjo basi doubt na ARVs unazomeza. Hata malaria kuna wanaotibiwa kwa Mseto na wengine Decotexin. Muhimu ni kuzingatia ubora na usalama wa hizo chanjo na si kulinganisha za Ulaya na hapa.

6. Kwanini tunalazimishwa tuchanje?

JIBU: Hakuna aliyelazimishwa. Chanjo ni hiyari. Wewe kama hutaki basi usimuandame aliyeamua kuchanjwa, kama ambavyo yeye hakuandami wewe uliyegoma. Muhimu tafuta taarifa za kutosha kabla hujafanya maamuzi ya kuchanjwa au kutochanjwa.

7. Chanjo zina madhara.

JIBU: Hakina dawa isiyo na madhara. Hata tangawizi na malimao ya mwendazake vina madhara. Lakini mara nyingi madhara ya dawa ni madogo kulinganisha na faida itokanayo na dawa yenyewe (unless for the very rare cases kunaweza kutokea madhara makubwa).

8. Kwanini serikali haiheshimu hisia zetu sisi tuliokataa chanjo?

JIBU: Imeheshimu ndio maana hamjalazimishwa kuchanjwa. Lakini na nyie heshimuni hisia za wale waliokubali kuchanjwa. Uhuru wako usiingilie uhuru wa mwenzako.

9. Kwanini chanjo ya Corona imekua ya kwanza kupingwa, nyingine hazikupingwa?

JIBU: Si kweli kwamba chanjo ya Corona ndio ya kwanza kupingwa. Hakuna chanjo yoyote imewahi kubuniwa ikaacha kupata upinzani. Anti Vaxxers wamekuwepo tangu enzi na enzi na hawataisha hadi Yesu arudi.

Ugonjwa wa ndui (smallpox) ulipokua tishio Edward Jenner alitengeneza chanjo mwaka 1721 wakati ambapo maelfu ya watu walikufa kwa ndui. Lakini jamii ilimpinga sana. Mchungaji Cotton Mather aliikubali chanjo hiyo na kuwashauri waumini wake waitumie. Akapata upinzani mkali na kupoteza robo tatu ya waumini wake, wakimhusisha na dhana ya Mpinga Kristo.

Lakini miaka mingi baadae dunia nzima ilikubali chanjo hiyo, na kila mtu alichomwa chanjo ya ndui. Kwahiyo hakuna jipya kwa hawa Anti Vaxxers wa Corona.
 
Kwann hii inaonekana ipo kibiashara zaidi tofauti na chanjo zingine.?
Sasa hivi tunasikia watu fulani wamepata utajiri kiasi fulani kutokana na chanjo ya corona lakini hatujawahi kusikia watu fulani wamepata utajiri kutokana na ARV
 
Ulitaka wapate umasikini kama wa kwako? Kweli wivu ukizidi ni zaidi ya uchawi.
 
Ugunduzi wowote ukishafanyika unakuwa biashara , maana ni gharama kubwa inatumika kwenye tafiti
Lakini baada ya hapo Kuna taasisi zinaamua kufadhili ili watu maskini wapate kwa bei nafuu au bure
 
Tamko la kijinga kabisa limekwepa maswali ya msingi
1. Afrika ni nchi ipi iliyofanikiwa baada ya kuchanja?

2. Ni kwa nini tupewe chanjo na wazungu waliokufa sana na corona wakati sisi hatujaarithiriwa kihivyo ?
Tuanze sisi kufanikiwa
Ni ujinga kusubiri uathirike ndo uchanjwe
 
Corona ni fumbo kubwa.

Chanjo imesababisha wananchi kukosa iman na kiongozi wao.

Mutations zikianza ndio tutaelewana vizuri. Kitanuka!
Baadhi ya watu wameamua kuwa fumba watu, Kama ndo chanzo ya Kwanza kutolewa duniani
 
Ulitaka wapate umasikini kama wa kwako? Kweli wivu ukizidi ni zaidi ya uchawi.
Wewe jamaa 👆 unawaona wenzako Wenye akili timamu na kusoma comments kwa kutumia akili wanavojibu comments 👇
Ugunduzi wowote ukishafanyika unakuwa biashara , maana ni gharama kubwa inatumika kwenye tafiti
Lakini baada ya hapo Kuna taasisi zinaamua kufadhili ili watu maskini wapate kwa bei nafuu au bure
 
Gift Nzarendo. Waliokuja na hii hoja wamechanganya Elimu ya Neno la Mungu na yanayo endelea duniani kwa sasa. Jua hilo kwanza. Neno la Mungu linasema kuna majira na nyakati katika kila kusudi la Mungu chini ya nchi.

Hayo yote uliyo ya ongelea haya kutokea maana majira na nyakati zilikuwa bado. Chanjo hii inatupeleka katika zoezi la maandalizi ya kupigwa chapa ya mpinga Kristo. Ziko chanjo zimetumiwa kuleta ugumba, kuthibiti ukuaji wa population. Nasema uongo jamani?

Nitakupa changamoto utafakari. JJ inayolalamikiwa imechanja 2.4% ya Wamarekani na inawezekana ikawa ndio lengo lao kupunguza population yao kwa 2.4%. Na ikitokea ikiwa hivyo sisi Tanzania tutapunguza yetu kwa ngapi kutumia JJ.

Hizi chanjo za kupewa tujiulize kwa nini sio buffet ya chanjo zinazotumika USA tuletewe JJ tu? Tumezoea nguo za misaada utakuta jeans ke/me, gagulo vivyo hivyo. Sasa chanjo imekuja JJ tu. Uko walakini flani hapa.
 
Kwann hii inaonekana ipo kibiashara zaidi tofauti na chanjo zingine.?
Sasa hivi tunasikia watu fulani wamepata utajiri kiasi fulani kutokana na chanjo ya corona lakini hatujawahi kusikia watu fulani wamepata utajiri kutokana na ARV
Acha ujinga. Kama wewe hujasikia kitu, je inamaanisha hakipo???
Jielimishe kidogo kuhusu faida kubwa za madawa ya ARV:
 
Gift Nzarendo. Waliokuja na hii hoja wamechanganya Elimu ya Neno la Mungu na yanayo endelea duniani kwa sasa. Jua hilo kwanza. Neno la Mungu linasema kuna majira na nyakati katika kila kusudi la Mungu chini ya nchi.

Hayo yote uliyo ya ongelea haya kutokea maana majira na nyakati zilikuwa bado. Chanjo hii inatupeleka katika zoezi la maandalizi ya kupigwa chapa ya mpinga Kristo. Ziko chanjo zimetumiwa kuleta ugumba, kuthibiti ukuaji wa population. Nasema uongo jamani?

Nitakupa changamoto utafakari. JJ inayolalamikiwa imechanja 2.4% ya Wamarekani na inawezekana ikawa ndio lengo lao kupunguza population yao kwa 2.4%. Na ikitokea ikiwa hivyo sisi Tanzania tutapunguza yetu kwa ngapi kutumia JJ.

Hizi chanjo za kupewa tujiulize kwa nini sio buffet ya chanjo zinazotumika USA tuletewe JJ tu? Tumezoea nguo za misaada utakuta jeans ke/me, gagulo vivyo hivyo. Sasa chanjo imekuja JJ tu. Uko walakini flani hapa.
Ndiyo!!! (uliuliza "Nasema uongo jamani?"). Chanjo ipi imetumiwa kuleta ugumba??? Wachina walipunguza idadi ya watoto kuliko kila nchi duniani lakini hawakutumia chanjo. Hakuna chanjo ya kuzuia watoto.
Marekani hawana shabaha kupunguza idadi ya watu wao 2.4% (wala %% yoyote). Kinyume wanaendelea kupokea wahamiaji kutoka nchi nyingine ili kujenga uchumi wao.
Kama sasa wameleta chanjo ya Johnson - kwa sababu walibaki nayo baada ya kuchanja watu wengi wengi tayari, na kwa sababu ile chanjo ya JJ ilichelewa kufika sokoni. Hapo sababu ya kufikia watu wachache huko. Lakini wamechanja mamilioni ya watu wao , na bila shaka SI KWA KUSUDI KUWAUA.
Kwa Astra Zeneca kama huko Kenya TZ imechelewa shauri ya kiburi cha mwenda zake. Itarudi baadaye.
 
Ugunduzi wowote ukishafanyika unakuwa biashara , maana ni gharama kubwa inatumika kwenye tafiti
Lakini baada ya hapo Kuna taasisi zinaamua kufadhili ili watu maskini wapate kwa bei nafuu au bure
Wanachosahau baadhi ya watu ni kwamba wako wenzao wanaojitolea hadi kujinyima usingizi wakitafiti namna ya kuwaepusha binadamu wenzao na athari za milipuko ya magonjwa hatari kama hii ya corona.

Katika kundi hilo wapo Watanzania ambao hawajawahi kugundua chochote kuboresha maisha au kuwaokoa binadamu wenzao na majanga kama hayo lakini ndio wa kwanza kuwakejeli watu kama hao.

Baadhi ya Watanzania wenzetu unaweza hata kutilia shaka ubinadamu wao kwa namna wanavyouchukulia kama joho linaloweza kuvaliwa na kuvuliwa kulingana imani yao na hali zao katika nyakati hizo.

Fikiria mtu na akili zake timamu anadai Tanzania iko kwenye vita ya kiuchumi na taifa kubwa kama Marekani! Anatoa dai kama hilo la kijinga jukwaani na kushangiliwa kwa vifijo na nderemo kama mkombozi!

Naam, hivyo ndivyo tulivyo ingawa si wote...masikini Tanzania!
 
Hulazimishiwi kupiga chanjo tafadhali acha acheni makelele,kila mtu atabeba mzigo wake,ukiumwa usihangaishe madaktari waliokwambia chanjo ndio kila kitu.
 
Gift Nzarendo. Waliokuja na hii hoja wamechanganya Elimu ya Neno la Mungu na yanayo endelea duniani kwa sasa. Jua hilo kwanza. Neno la Mungu linasema kuna majira na nyakati katika kila kusudi la Mungu chini ya nchi.

Hayo yote uliyo ya ongelea haya kutokea maana majira na nyakati zilikuwa bado. Chanjo hii inatupeleka katika zoezi la maandalizi ya kupigwa chapa ya mpinga Kristo. Ziko chanjo zimetumiwa kuleta ugumba, kuthibiti ukuaji wa population. Nasema uongo jamani?

Nitakupa changamoto utafakari. JJ inayolalamikiwa imechanja 2.4% ya Wamarekani na inawezekana ikawa ndio lengo lao kupunguza population yao kwa 2.4%. Na ikitokea ikiwa hivyo sisi Tanzania tutapunguza yetu kwa ngapi kutumia JJ.

Hizi chanjo za kupewa tujiulize kwa nini sio buffet ya chanjo zinazotumika USA tuletewe JJ tu? Tumezoea nguo za misaada utakuta jeans ke/me, gagulo vivyo hivyo. Sasa chanjo imekuja JJ tu. Uko walakini flani hapa.
Mkuu samahani, ila wewe una mtindio wa ubongo
 
Ndiyo!!! (uliuliza "Nasema uongo jamani?"). Chanjo ipi imetumiwa kuleta ugumba??? Wachina walipunguza idadi ya watoto kuliko kila nchi duniani lakini hawakutumia chanjo. Hakuna chanjo ya kuzuia watoto.
Marekani hawana shabaha kupunguza idadi ya watu wao 2.4% (wala %% yoyote). Kinyume wanaendelea kupokea wahamiaji kutoka nchi nyingine ili kujenga uchumi wao.
Kama sasa wameleta chanjo ya Johnson - kwa sababu walibaki nayo baada ya kuchanja watu wengi wengi tayari, na kwa sababu ile chanjo ya JJ ilichelewa kufika sokoni. Hapo sababu ya kufikia watu wachache huko. Lakini wamechanja mamilioni ya watu wao , na bila shaka SI KWA KUSUDI KUWAUA.
Kwa Astra Zeneca kama huko Kenya TZ imechelewa shauri ya kiburi cha mwenda zake. Itarudi baadaye.

Maneno mengi. Moja ya madhara ya chanjo za kabla ya hii ya corona ziko zilizolalamikiwa kusababisha ugumba. Tafuta hapa ni jF sio kila kitu ni spoon feeding.
 
Njano imeleta taaruki wazazi wameandamana wamejaa shule za msingi kipawa dar es salaam kisa Mzungu kaonekana shuleni.Kuna shule Mzungu anafundisha kaja kutembelewa na rafiki yake Mzungu wanafunzi wamekimbia wazazi wamejaa watoto wetu awachomwi.Afrika bado Sana yaani Mzungu kaja kutembelewa na Mzungu mwenzake wanafunzi nduki.Hili la chanjo muitikio bado serikalini ifanywe Sana elimu ya kutosha maana wanasiasa sio watu.
 
Back
Top Bottom