Tuache siasa tuwekeze katika hisabati | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuache siasa tuwekeze katika hisabati

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sabi Sanda, Dec 11, 2009.

 1. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #1
  Dec 11, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wakuu,

  Natumaini wengi wetu tumepata taarifa kuhusu matokeo ya darasa la Saba. Inatia aibu na kusikitisha sana kuona kuwa Hisabati ndiyo somo linaloongoza kwa wanafunzi kufeli. Zaidi ya asilimia 79 wamefeli. Ukienda ngazi ya sekondari hali haina tofauti kwani wastani wa wanafunzi wanaopata "F" katika Hisabati ni zaidi ya asilimia 75.

  Nafikiri ni muhimu sana tukakubali udhaifu wetu na kufanya kile tunachopaswa kufanya kama taifa. Tuwekeze ipasavyo katika Hisabati na sayansi kama taifa. Tembeleeni vyuo vyetu vya ualimu muone hali ilivyo. Hivi kweli tuko makini kweli na ubora wa elimu katika nchi yetu????

  Kuhusu somo la Kingereza takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 64.6 wamefeli. Moja ya njia inayoweza kutusaidia ni kufundisha Watanzania kwa angalau saa 2 kila siku kupitia Televisheni la Redio (hasa TBC). Tukiwekeza angalau shilingi bilioni 20 kila mwaka pale TBC kwa ajili ya kutoa elimu kwa taifa kwa kushirikiana na vyuo vyetu mbalimbali, baada ya miaka 10 tutakuwa taifa tofauti.
   
 2. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #2
  Dec 11, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ni watanzania wangapi wana utamaduni za kusikiliza redio? Ni watanzania wangapi wana uwezo wa kuwa na Television?
   
 3. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #3
  Dec 11, 2009
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kiongozi kuna utafiti wowote umefanya ukagundua kua njia hii ina ufanisi zaidi ya njia nyingine zote?? Je ni watanzania wangapi wenye TV sets nyumbani? Je ni wangapi wanaangalia vipindi vya elimu kama si ze komedi na mambo mengine??
   
 4. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #4
  Dec 11, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  TV na Redio hazijapendekezwa kama njia mbadala. Bali njia ambazo zinaweza kusaidia pamoja na njia nyingine kutufikisha huko tunakotaka kwenda. Kama tunaamini kuwa baadhi ya vipindi katika TV vimechangia sana kuwaharibu Watanzania, naamini pia tunaweza kutumia TV pia kuwarudisha katika mstari mnyoofu.

  Ni kweli kuwa si watanzania wengi ambao wana TV. Suluhisho ambalo linaweza kusaidia katika hili ni kuweka Umeme Jua katika shule zetu na kujenga Community Centres katika vijiji vyetu na kuzipatia Umeme Jua. Kama Watanzana tulivyojenga shule za kata hatuwezi kushindwa kujenga Community Centres katika kila kijiji kwa ajili ya elimu hasa katika Stadi za Maisha.
   
 5. Companero

  Companero Platinum Member

  #5
  Dec 11, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Everything is political. You need politics to invest in mathematics. Thats why someone said politics is too important to be left to politicians. Lets invest in politics. Thats the only way we can be able to make political decision such as that of investing in mathematics.
   
 6. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #6
  Dec 11, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hata hesabu ni siasa, watu walianza kuandika namba kwa sababu wafalme wa Babeli walikuwa wanataka kukusanya kodi, hivyo ilibidi wajue ukubwa wa mashamba na wingi wa mazao.

  Tunatumia numerali za kiarabu (1,2,3,4...) kwa sababu wazungu walipoenda kupigana vita vya crusades (siasa) walichukua vitabu vilivyokuwa na nambari za kiarabu zinazofanya kazi vizuri kuliko numerali za kirumi.

  Kwa hiyo kama unataka kuweka mkazo katika hisabati, sema hivyo.Ukitaka kui slight siasa, unaweza kusoma hesabu unavyotaka, halafu wanasiasa wakakwambia hesabu zako hazina mpango.

  Hakuna sababu kwa nini watu wasijue vyote, siasa na hesabu.
   
 7. Companero

  Companero Platinum Member

  #7
  Dec 11, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Bajeti ni hesabu. Na bajeti ndio inaamua fungu gani linaenda kuwekeza wapi. Hatuwezi kuwaachia wanasiasa wa majukwaani (platform politicians) watupangie bajeti!
   
 8. C

  Chuma JF-Expert Member

  #8
  Dec 11, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ilibidi marehem Prof.Shayo wa hesabu nae awekeze ktk SIASA...baada ya kuona watu hawapo ready ku-invest ktk "Hesabu"

  Kimsingi ukiona mtu anapewa Uongozi kwa asie na Elimu tegemea hilo Jambo kuharibika
   
 9. epigenetics

  epigenetics JF-Expert Member

  #9
  Dec 12, 2009
  Joined: May 25, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  hesabu ngumu, jameni doh!
  ila this shows us that bado hatupo serious ktk swala la elimu. inabidi hao laki 5 waliofeli wafanyiwe mpango kuendelea na elimu ya vitendo ktk fani mbali mbali. at least huko mbeleni wawe na qualification ya aina yoyote, sio tu mtu ukifeli la saba ndio mwisho wa dunia kwako. hiyo VETA ianzie form 1.
   
 10. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #10
  Dec 17, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Epigenetics na wengine,

  Bahati mbaya sana hakuna anayejali kuwa kuna vijana zaidi ya laki tano ambao wamefeli mtihani wa darasa la saba na kuja na mpango wa kuwapatia ujuzi katika fani mbalimbali ili waweze kuwa wazalishaji bora na kumudu maisha yao.
   
 11. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #11
  Dec 17, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  ugonjwa wa taifa huu mkuu!kujua hisabati ni KIPAJI kutoka kwa ALLAH!
  asilimia karibu 85 ya waafrika NI WAOGA WA MATHE!
   
 12. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #12
  Dec 17, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Perception ya vijana wengi ni kuwa masomo ya Science hayana deal maana scientist wengi wanalost mtaani. Ila ni mtazamo finyu maana mambo yanabadilika haraka. Kuna vitu vingi ambavyo bila kuwa na wasomi wa science itakuwa ndoto kuviendesha. Mfano ni kukua kwa construction industry, mining industry, mambo ya ICT etc
  Kama mchangiaji mmoja alivyosema leadership is everything. Kama leaders hawataweka umuhimu kwenye elimu basi itaonekana kana kwamba haina umuhimu. If we train well competent scientist leo, tunaweza kukuta tunauza raslimali watu pia in the world where knowledge has become so powerful.
  Vision ya kuwapa vijana iwe wazi kwamba waiiangalie dunia kwa jicho pana sio kwa kuangalia jinsi ajira zilivyokuwa miaka mitatu iliyopita tukajikuta kundi kubwa limefocus kwenye trend hiyo tu na kusahau the whole idea of promising future.
   
 13. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #13
  Dec 17, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Mbona mnashindwa kusema ukweli. Matatizo ya elimu yaliopo sasa ni matunda ya mipango sahihi ya elimu ya Dr. Kambarage Nyerere.
   
 14. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #14
  Dec 17, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Hesabu....... hisabati, magazijuto magazijoto aljebra ah kichina kitupu.

  Hivi unategemea nini kutoka kwa mwalimu alieecha chuoni baada ya kupata ziro ktk O level au A level?? Dawa ni kuwa na programu inayoeleweka kwa kila somo halafu wizara iache kuwachanganya wanafunzi kwa kuwaletea mabadiliko ya masomo kila mhula.
   
 15. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #15
  Dec 18, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  duu mwana vitu vingine tunavyoongea inabidi tuwe makini inamaa wote hao laki tano waliofeli ALLAH hajawapa vipaji vya hisabati, bac kama ndio hivyo Allah ana mpango wake inabidi tusubiri tuone

  tatizo kubwa la sasa Tanzania ni siasa, hili Tazizo limekuwa kubwa kiasi sasa linafikia kuathiri maendeleo ya taifa, maana kwa kila kitu ambacho kinaweza kutatuliwa kwa njia ya kawaida ni lazima siasa ndio ichukue mkondo wake kwanza, na ule ushauri mzuri wa wataalamu unafuata baadae kama ukipata nafasi, (issue ya relwe, richmond, epa na zinginezo, ushauri wa kitaalamu ulipuuzwa na ule wa wanasiasa ndio ukachukua nafasi)

  sasa kwa hili la hisababti tatizo nadhani moja kwa moja linaanzia serikalini, uwezi kuwalaumu wanafunzi wakati ujawapa walimu wanaofahamu hilo somo, kama serikali imewaajili walimu wabovu unategemea nini, mbona kipindi cha nyuma ufaulu ulikuwa ni mkubwa katiak hayo masomo,

  sasa hebu angalia wanataka kuua technical collage zote ziwe universities, sidhani kama unaweza kuwa na product nzuri bila kuwa na artisanz na mafundi michundo, hivi mainjinia wote wakiwa na gdegree nani atakuwa technician, lakini uhamuzi huo upo kisiasa zaidi ili ionekane huyu raisi amecha vyuo vikuu kadhaa
  nchi kama India, China, na Scandinavian wanabase sana kwenye technicianz level na ndio maana hawa jamaa wa FINIDA na DANIDA Walijaribu kuwekeza sana kwenye VETA.

  NCHI YENYE MAENDELEO SIASA HUWA ZINAANZA NA ZINAISHIA WAKATI WA UCHAGUZI, BAADA YA HAPO WATU WANAPIGA KAZI 2
   
 16. Companero

  Companero Platinum Member

  #16
  Dec 18, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mwalimu Nyerere ndiye aliyewatungia Sera ya Elimu ya 1995 na hii mnayoiandaa ya 2009?
   
 17. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #17
  Dec 18, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mimi nadhani ualimu unaanzia nyumbani. kama wazazi (walezi) wanapata muda wa kuongea na watoto wao na kujua matatizo yao ni rahisi kwa watoto husika kueleza wapi wanahitaji msaada. hakuna mtu anayezaliwa na uwezo wa kufahamu kila kitu. ukifundishwa utajua tu. wazazi/walezi hima tafadhari tuwafundishe watoto wetu kuanzia nyumbani, mjengee mtoto mazingira ya kusoma tangu akiwa mdogo. hisabati na kiingereza ni masomo marahisi kwakweli lakini ukweli ni kwamba wanafunzi wengi wanafulia sana hapo.

  nakumbuka miaka ya nyuma kidogo watu wengi walikuwa nanakimbilia kufanya kazi za kiofisi zaidi kwasababu 'ualimu' ulikuwa haulipi kabisa. Hivyo 'sirikali' iliamua kuziba mapengo ya waalimu kwa kuanzisha mpango wa UPE, waalimu hawa wengi wao walikuwa ni wale wahitimu wa darasa la saba waliofeli. sio siri inauma sana.

  mimi mwenyewe nilisomeshwa na waalimu hao, yaani nilipofika kidato cha 4 na ndio nikaona baadhi ya waalimu husika wa UPE wanajisomesha jioni na kufanya mitihani ya kidato cha 4 kwakuwa serikali imewawekea ngumu!

  sasa madhara au sumu iliyopandikizwa na waalimu hao wa UPE bado ipo haijaisha na madhara yake inaendelea kutafuna kizazi cha sasa. wanafunzi hawaelewi kabisa...

  Naiomba 'sirikali' kupitia watu wake waliopo humu JF wasaidie kuwapa motisha waalimu ili watu wengi waipende kazi hiyo na kuiona ni ya muhimu kwa maendeleo ya taifa. vitu vinavyoweza kufanywa na 'sirikali' ni kama kuwapa mishahara mizuri, marupurupu na kuwajengea nyumba nzuri, ofisi nzuri n.k

  Embu angalia waalimu wa UPE, inawezekana vipi mwalimu mwenye elimu ya darasa la saba amfundishe mwanafunzi wa darasa la saba? hapo 'sirikali' ilifulia sana sio siri.

  kitu kingine watanzania tuondoe mawazo ya kwamba eti hisabati, sayansi ni ngumu...hayo mawazo sio mazuri kabisa...

  Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Africa...
   
Loading...