kabila01
JF-Expert Member
- Apr 21, 2009
- 4,235
- 4,950
Mimi sio mchumi ila Wachumi hebu tusaidieni kutuelimisha, kuna dhambi gani kufungua FD ili hizo kiduchu ulizopewa zizaliane angalau kukidhi mahitaji ukilinganisha na kuzihifadhi tuu BOT ambako hazizalishi hata sentí moja?!.
Kwa uzoefu wangu mara zote pesa zinazoombwa hua haziji zote, tumeshuhudia MSD katika robo ya kwanza wamepata fedha chini ya 50% kwa zile walizoomba pamoja na sekta nyingi tu za serikali. Kwa Mantiki hiyo kila idara, mkurugenzi na mkuu wa kitengo ambaye atapokea fedha za serikali kutoka katika bajeti ya serikali ambayo imepitishwa na Bunge basi ajiongeze kwa kuziweka kwenye FD ili aweze kukamilisha shughuli.