Asanteni kwa kuanzisha mada hii. Ninaungana na wote waliotoa msimamo wao kuhusu mijadala ya dini ambayo haitufikishi popote zaidi ya kupoteza wakati na kututenganisha. Ni ukweli wa kikatiba kuwa Tz haina dini ingawa wa TZ wanazo dini zao. INATOSHA. Kila mtu abakie na imani yake moyoni, hadharani tujadili mambo ya kumkomboa Mtanzania.
Tuna masuala kama katiba, umeme, maji, barabara mbovu, ajira, mishahara mibovu, pensheni, elimu duni (kuanzia chekechea hadi vyuo, uhaba wa madarasa, samani, walimu, vifaa vya maabara, nobe hata chaki hatuna sisemi sayansi na teknolojia), afya, usafiri na miundombinu, rushwa, wizi na ubadhirifu wa mali za umma, mikataba mibovu, uongozi bora... Orodha haiishii hapa. Kwa nini tunayawacha haya tunajadili dini na dini ya mtu.
Tuamkeni Watanzania. JF ni mahala muafaka pa kuanzisha mijadala ya kujenga, ya kumkomboa Mtanzania na wala sio dini. I-N-A-T-O-S-H-A.