Tuache mfumo Dume, Samia Suluhu Hassan ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tumpe ushirikiano!

Alex Fredrick

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
680
1,338
Rais wa sasa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Mh Samia Suluhu Hassan...

Mh Samia amepokea kijiti baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Magufuli kilichotea tarehe 17 March mwaka huu

Toka Mh Rais Samia Suluhu amepokea kijiti tunaona kwa nafasi yake kama Rais wa awamu ya sita anakuja kutibu majeraha ya serikali zote ambazo zimetangulia...

Kila Rais ambaye amepita kwa nafsi yake alikuwa na mifumo yake pamoja na taratibu zake

Kwahiyo Mh Rais Samia Suluhu Hassan nae anakuja na mifumo yake na taratibu zake ili mwisho wa siku aje ahukumiwe yeye kama yeye na sio mwingine

Ameanza na kurudisha Diplomasia ya nchi hii ambayo siku za nyuma ilikuwa imeyumba kidogo

Pili tunaona anarudisha" Sector Binafsi ambayo 80% ya watanzania wote...

Kingine ameanza kupandisha madaraja wafanyakazi ambao walikaaa zaidi ya miaka 6 pasi na kupandishwa madaraja

Poa ameanza kulipa wazabuni na makandarasi malimbikizo ya muda mrefu

Yako mambo mengi ikiwamo kurudisha mifumo ianze kufanya kazi ndani ya serikali na taasisi zake..

Hoja yangu ya msingi tumpe Ushirikiano Mh Rais Samia Suluhu Hassan kama Kiongozi wetu pasi na mashaka ili kwa nafsi yake aweze kutimiza maono yake katika kipindi hichi ambacho anahudumu

Alex fredrick
 
Raia tunampa. Wasaidizi wake na wanasiasa wenzake ndio hati hati.

Tunamwambia gesi ipo. Madini yapo. Maliasili na rasilimali zipo. Watu wapo. Maji chini ya ardhi yapo. Jua lipo. Upepo upo. Ardhi yenye rutuba ipo. Vina vya bandari ndio usiseme. Madaraka anayo.

Sasa anahangaika huko nje ya nini wakati unahitajika usimamizi tu?
 
Unakosea unaposema majeraha. Hivi kipindi Dkt Magufuli anarithi hii nchi ilikuwa imefikia hatua gani? Hukumbuki ufisadi, uzembe, madawa vilikuwa vimetamalaki???? Hivi hujui wapiga dili walijipanga kuuza nchi?

Mnapa kichwa Mama kwa kumsemea eti anaponya majeraha. Yeye angekuwa makini Mama angesimamia yake ambayo serikali ya Dkt Magufuli iliyaanzisha bila kuanza kuyabadilisha kama vile yeye hakuwa sehemu ya hiyo serikali.

Sasa hivi anaonekana kituko mtaani. Mfano tozo walizileta akina Mwigulu ili kumharibia na yeye Mama kakubali kichwa kichwa, yaani vitu vingi wanamdanganya hawa wanasiasa njaa anakubali.

Yeye afuate ushauri wa vijana wa kitengo atakuwa na Amani mno kwa sababu wao ndiyo wanajua wananchi wanahitaji nini. Ila kama aliwaondoa hao boda boda, chinga mhhh ni kazi
 
Raia tunampa. Wasaidizi wake na wanasiasa wenzake ndio hati hati.
Tunamwambia gesi ipo. Madini yapo. Maliasili na rasilimali zipo. Watu wapo. Maji chini ya ardhi yapo. Jua lipo. Upepo upo. Ardhi yenye rutuba ipo. Vina vya bandari ndio usiseme. Madaraka anayo.
Sasa anahangaika huko nje ya nini wakati unahitajika usimamizi tu??????!!!!!!
Nikupe na ya Bi.Tozo umtumie huu ujumbe?
 
Unakosea unaposema majeraha. Hivi kipindi Dkt Magufuli anarithi hii nchi ilikuwa imefikia hatua gani? Hukumbuki ufisadi, uzembe, madawa vilikuwa vimetamalaki???? Hivi hujui wapiga dili walijipanga kuuza nchi????? Mnapa kichwa Mama kwa kumsemea eti anaponya majeraha. Yeye angekuwa makini Mama angesimamia yake ambayo serikali ya Dkt Magufuli iliyaanzisha bila kuanza kuyabadilisha kama vile yeye hakuwa sehemu ya hiyo serikali. Sasa hivi anaonekana kituko mtaani. Mfano tozo walizileta akina Mwigulu ili kumharibia na yeye Mama kakubali kichwa kichwa, yaani vitu vingi wanamdanganya hawa wanasiasa njaa anakubali. Yeye afuate ushauri wa vijana wa kitengo atakuwa na Amani mno kwa sababu wao ndiyo wanajua wananchi wanahitaji nini. Ila kama aliwaondoa hao boda boda, chinga mhhh ni kazi
Ficha upumbavu wako. Hizi tozo mnazoongea kila siku mlitaka Samia aje na fedha za urithi kutoka kwao Ili aendeshe nchi? Au mlitaka aingie kwenye akauti za watu apore hela zao Ili awajengee madarasa? Tulilipa tozo hadi za baiskeli hapa enzi za Mwinyi na Mkapa na tulilipa kodi za kichwa enzi za Nyerere na Mwinyi. Private sekta almost ilikufa kabisa. Ajira huko zilipungua ndio maana mtangulizi wake alijikita kupata hela kutoka njia za kibabe. Was that sustainable? Kuna miradi mikubwa umeacha na mtangulizi wake, na wananchi tumekomaa aimalizie, ataimalizaje kama hatakusanya fedha kutoka kwa wananchi? Acheni unafiki, acheni udumedume. Samia ndio Rais wenu.
 
Tumpe nafasi ipi tena, kama amepewa urais wenye mamlaka yote ya kiungu mtu na bado anashindwa kuleta maendeleo na kutenda haki?

Mfumo dume unakujaje hapo kama yeye mwenyewe kila siku anarudia kusema yeye ni rais wa kike na kuhakikisha anabakia madarakani kwa kuwa yeye ni mwanamke?

Ni mama huyu huyu aliyetuletea hadithi za ugaidi, tozo, manyanyaso ya wapinzani, aliyewaondoa wamachinga mitaani, aliyehusika kusaini mradi hewa wa ujenzi wa meli mpya, kupanda kwa bei ya mafuta, gesi na vyakula, mgao wa umeme na maji, kuingilia mhimili wa mahakamani nk.

Mleta mada unataka sisi tufanyeje sasa kama mtu hawezi, hajitambui na hajiamini?
 
Chief Hangaya alikuwa msaidizi wa huyu shetani ambae unadai kuwa aliua sector binafsi pamoja na diplomasia ya nchi ambae kwa sasa yupo kuzimu kama anavyoonekana hapa👇
628693.jpg

Ukweli mchungu ni kwamba msaidizi wa Shetani hawezi kuwa Malaika.
 
Unakosea unaposema majeraha. Hivi kipindi Dkt Magufuli anarithi hii nchi ilikuwa imefikia hatua gani? Hukumbuki ufisadi, uzembe, madawa vilikuwa vimetamalaki???? Hivi hujui wapiga dili walijipanga kuuza nchi????? Mnapa kichwa Mama kwa kumsemea eti anaponya majeraha. Yeye angekuwa makini Mama angesimamia yake ambayo serikali ya Dkt Magufuli iliyaanzisha bila kuanza kuyabadilisha kama vile yeye hakuwa sehemu ya hiyo serikali. Sasa hivi anaonekana kituko mtaani. Mfano tozo walizileta akina Mwigulu ili kumharibia na yeye Mama kakubali kichwa kichwa, yaani vitu vingi wanamdanganya hawa wanasiasa njaa anakubali. Yeye afuate ushauri wa vijana wa kitengo atakuwa na Amani mno kwa sababu wao ndiyo wanajua wananchi wanahitaji nini. Ila kama aliwaondoa hao boda boda, chinga mhhh ni kazi
Hata kama uko sahihi lakini siyo kiviiiiiile! Unamtaka Mama afuate ushauri wa kitengo afanye yafuatayo;
1.Aamuru watu wapigwe risasi hadharani?
2.Aamuru watu watekwe na kupotezwa?
3.Àamuru wanaompinga wakamatwe na kubambikiwa kesi za ugaidi?
KWAMBA hayo ndo yatampa Amani ya moyo? Amani unaipata huku unaona Fulani anateswa bila hatia? Nafsi itakubali kabisa na Mungu ataruhusu nafsi yake itulie?
LABDA kuhusu kudanganywa na kina Mwingulu nakuunga mkono, Mwigulu ni Chawa, hajawahi kusema ukweli zaidi ya kujipendekeza.
 
Usisumbuke na hawa wapuuzi wachache sukuma gang ambae mpuuzi mwenzao marehemu alitumia wajinga wenzake kina Gwajima kusema eti wao ndo wengi na wanaweza kuweka Rais.

Wanaompinga Samia wote wako kwenye hiki kichaka cha ukabila na ni wajinga na washamba tu.

Wametufundisha sasa kuwa wasahau kushika madaraka ya nchi hii tena!
 
Tumpe nafasi ipi tena, kama amepewa urais wenye mamlaka yote ya kiungu mtu na bado anashindwa kuleta maendeleo na kutenda haki?

Mfumo dume unakujaje hapo kama yeye mwenyewe kila siku anarudia kusema yeye ni rais wa kike na kuhakikisha anabakia madarakani kwa kuwa yeye ni mwanamke?

Ni mama huyu huyu aliyetuletea hadithi za ugaidi, tozo, manyanyaso ya wapinzani, aliyewaondoa wamachinga mitaani, aliyehusika kusaini mradi hewa wa ujenzi wa meli mpya, kupanda kwa bei ya mafuta, gesi na vyakula, mgao wa umeme na maji, kuingilia mhimili wa mahakamani nk.

Mleta mada unataka sisi tufanyeje sasa kama mtu hawezi, hajitambui na hajiamini?
Kwa iyo unata machinga waendelee kuziba barabara?

Hutaki kulipa kodi wakati unataka maendeleo?? Mpuuzi kabisa wewe
 
Unakosea unaposema majeraha. Hivi kipindi Dkt Magufuli anarithi hii nchi ilikuwa imefikia hatua gani? Hukumbuki ufisadi, uzembe, madawa vilikuwa vimetamalaki???? Hivi hujui wapiga dili walijipanga kuuza nchi????? Mnapa kichwa Mama kwa kumsemea eti anaponya majeraha. Yeye angekuwa makini Mama angesimamia yake ambayo serikali ya Dkt Magufuli iliyaanzisha bila kuanza kuyabadilisha kama vile yeye hakuwa sehemu ya hiyo serikali. Sasa hivi anaonekana kituko mtaani. Mfano tozo walizileta akina Mwigulu ili kumharibia na yeye Mama kakubali kichwa kichwa, yaani vitu vingi wanamdanganya hawa wanasiasa njaa anakubali. Yeye afuate ushauri wa vijana wa kitengo atakuwa na Amani mno kwa sababu wao ndiyo wanajua wananchi wanahitaji nini. Ila kama aliwaondoa hao boda boda, chinga mhhh ni kazi
Ukigundua kuwa huo ukabila wako hautakufikisha popote utafika mbali sana!

Hakuna nchi isiyofuata taratibu! Unataka watu wapange bidhaaa hadi barabarani na waachwe tu? We ni mpuuzi tu
 
Unakosea unaposema majeraha. Hivi kipindi Dkt Magufuli anarithi hii nchi ilikuwa imefikia hatua gani? Hukumbuki ufisadi, uzembe, madawa vilikuwa vimetamalaki???? Hivi hujui wapiga dili walijipanga kuuza nchi????? Mnapa kichwa Mama kwa kumsemea eti anaponya majeraha. Yeye angekuwa makini Mama angesimamia yake ambayo serikali ya Dkt Magufuli iliyaanzisha bila kuanza kuyabadilisha kama vile yeye hakuwa sehemu ya hiyo serikali. Sasa hivi anaonekana kituko mtaani. Mfano tozo walizileta akina Mwigulu ili kumharibia na yeye Mama kakubali kichwa kichwa, yaani vitu vingi wanamdanganya hawa wanasiasa njaa anakubali. Yeye afuate ushauri wa vijana wa kitengo atakuwa na Amani mno kwa sababu wao ndiyo wanajua wananchi wanahitaji nini. Ila kama aliwaondoa hao boda boda, chinga mhhh ni kazi
Wizi wa Trilion 1.5 ulitokea Awamu gani hadi CAG alipohoji akafutwa kazi?

Uwanja wa ndege wa chato ulijengwa kwa tender ipi? Na kampuni ipi? Ilikuwa Awamu gani?
 
Raia tunampa. Wasaidizi wake na wanasiasa wenzake ndio hati hati.
Tunamwambia gesi ipo. Madini yapo. Maliasili na rasilimali zipo. Watu wapo. Maji chini ya ardhi yapo. Jua lipo. Upepo upo. Ardhi yenye rutuba ipo. Vina vya bandari ndio usiseme. Madaraka anayo.
Sasa anahangaika huko nje ya nini wakati unahitajika usimamizi tu??????!!!!!!
Mtu anakuja kuchukua 70b kimasihari kwa kuweka just software ya tensco .sijui tumerogwa wapi
 
Kuingiza mambo ya kijinsia ni kukwepa uwajibikaji.

Yeye ni Rais, na kwa Katiba yetu ilivyo ana absolute power ya kufanya chochote, aache kulialia.

Ukweli ni anawajibika moja kwa moja kwa kila uamuzi na matendo yanayotendwa na serikali yake. Period.

Msianze kutafuta huruma ya wananchi hapa.
 
Ficha upumbavu wako. Hizi tozo mnazoongea kila siku mlitaka Samia aje na fedha za urithi kutoka kwao Ili aendeshe nchi? Au mlitaka aingie kwenye akauti za watu apore hela zao Ili awajengee madarasa? Tulilipa tozo hadi za baiskeli hapa enzi za Mwinyi na Mkapa na tulilipa kodi za kichwa enzi za Nyerere na Mwinyi. Private sekta almost ilikufa kabisa. Ajira huko zilipungua ndio maana mtangulizi wake alijikita kupata hela kutoka njia za kibabe. Was that sustainable? Kuna miradi mikubwa umeacha na mtangulizi wake, na wananchi tumekomaa aimalizie, ataimalizaje kama hatakusanya fedha kutoka kwa wananchi? Acheni unafiki, acheni udumedume. Samia ndio Rais wenu.
Ndo kupeleka 30usd nje ya nchi kwa ERP software ya tenesco .wew unaona ni sawa
 
Ubarikiwe sana,umeelezea vizuri,lazima wewe utakuwa kama sio mhadhiri wa chuo kikuu,utakuwa ni mwalimu katika nyanja tofauti.Umeelezea vizuri,na umeweleweka,atakaye kupinga,ni kuwa uwelewa wake ni mdogo,lakini usichoke,kumuelezea,ataelewa tu.
 
Kuna mtu .

Back
Top Bottom