Tuache kujibagaza, tukitaka kuwa wazalendo wa kweli tutafute suluhu ya kudumu dhidi ya mkulima Steyn

Tatizo ni ubabe wa watendaji serikalini kutotaka kulipa madeni sio tu ya nje bali hata ya ndani. Mfano Katibu Mkuu Kiongozi alimuandikia barua Katibu Mkuu Wizara Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano tarehe 22/01/2019 akimuamuru alipe madai ya wastaafu ATCL ya PSSSF ( PPF) lakini hadi hi Novemba, 2019 hakuna alicholipa. Hii inadhihirisha umwamba wa viongozi serikalini wa kutotii mamlaka na kufanya yao au kwa kufuata maelekezo ya mkuu wa kaya.
Kama wastaafu ATCL wangekuwa wanaishi nje ya nchi naona nao wangepeleka suala hili mahakama za huko nje ili ndege zikamatwe kwani kuhusu suala hili shirika la PPF waliipeleka ATCL mahakamani hapa nchini na kuamriwa kukamata mali za ATCL na kuzinadi hali iliyopelekea Katibu mkuu Uchuku, Ujenzi na mawasiliano kuingilia kati na kuahidi kulipa kitu ambacho haja tekeleza hadi leo. Huu ndio ubabe wa wenye dhamana serikalini na ndio unaleta haya matatizo.
 
TAHADHARI: Kama huna akili timamu usisome.!
__________________________________
Kuhusu kuzuiliwa kwa ndege yetu huko Canada, swali la msingi la kujiuliza ndege zetu zitaendelea kuzuiliwa hata lini? Hii ni ndege ya 3 tangu zimeanza kuzuiliwa.

Ya kwanza ilizuiwa Canada kufuatia kesi iliyofunguliwa na kampuni ya ukandarasi ya Sterling Construction and Engineering Ltd (SCEL), nyingine ilizuiliwa Afrika Kusini kufuatia kesi iliyofunguliwa na mkukima Hermanus Steyn, na huyohuyo ndiye amezuia tena ndege hii ya sasa.

Tukitaka kuwa WAZALENDO wa kweli tutafute suluhu ya kudumu ya tatizo hili. Nimemsikiliza Prof.Kabudi akiongea na Rais JPM kwa kujibagaza kama kawaida yake. Akijitutumua na kuongea kwa tashwishwi na tamathali nyingi za semi, lakini hajatoa suluhisho la kudumu, badala yake ameishia kumpotosha Rais.

Kabudi ameongea kana kwamba tatizo la msingi ni Canada, na amefanikiwa kushawishi watanzania waamini hivyo. Akafika mbali na kusema alimuita Balozi wa Canada na kumwambia eti serikali imekasirika sana (hii kauli ya kifutuhi tuipuuze. Tuhesabu tu kwamba Kabudi alitaka kufurahisha umati kama kawaida yake).

Lakini je tatizo ni Canada. Jibu ni HAPANA. Tatizo si Canada, si Afrika kusini, wala si Chato. Tatizo la msingi ni kesi zilizofunguliwa dhidi ya serikali na serikali kuangukia pua. Kwa hiyo badala ya kudeal na Canada tudeal na kesi hizo. Unless otherwise ndege zetu zinaweza kukamatiwa hata Burundi.

Kwa mfano kesi iliyoshikilia ndege kwa sasa ni ya mkulima Hermanus Steyn. Huyu alikua mlowezi aliyemiliki mashamba makubwa sana ya kilimo mkoani Arusha. Mwaka 1982 serikali ya Nyerere ikataifisha mashamba yake, magari yake 250, ndege ndogo 12, mifugo na majengo.

Akafungua kesi mahakamani hapahapa nchini akidai fidia ya $36M. Mahakama kuu ya Tanzania ikampa ushindi na kumgrant "tuzo" hiyo ya $36M. Serikali ikasema haiwezi kumlipa pesa zote hizo. Ikaunda kamati maalumu ya kufanya tathmini ya mali zilizotaifishwa. Kamati hiyo iliongozwa na Mzee Chenge na Mkulo, ikapendekeza alipwe $20M kinyume na "tuzo" aliyopewa na mahakama ya $36M.

Serikali ya Rais Mwinyi ikamlipa $20M kama ilivyopendekezwa na kamati ya akina Chenge. Wakati huo sarafu yetu bado ilikua na nguvu. $20M zilikua kama TZS 44M hivi kwa wakati huo. Mkulima Steyn akapewa lakini hakuridhika. Akaendelea kudai kiasi kilichobakia. Na amekua akidai tangu wakati huo hadi sasa bila kulipwa. Kiasi kilichobakia kilikua $16M lakini kutokana na kukaa kwa muda mrefu pamoja na riba kimefika $33M, sawa na TZS 70 Bilioni kwa sasa.

Serikali ya Tanzania ilipoona anasumbua sana kudai fedha hizo ikampiga marufuku kukanyaga ardhi ya Tanzania. Steyn akaona atapoteza haki yake. Akachukua hukumu ya mahakama kuu ya Tanzania iliyompa ushindi na kwenda kusajili tuzo yake katika Mahakama ya Afrika kusini. The Arbitration act, cap.15 inamruhusu kufanya hivyo.

Akaomba mali za serikali ya Tanzania zilizopo Afrika kusini zikamatwe ili kufidia deni lake. Kifungu cha 30 cha sheria hiyo kinatoa masharti ya kufanya hivyo (conditions for enforcement of foreign awards). Na ndipo ndege yetu aina ya Airbus A220-300 ilipozuiwa nchini humo.

Lakini ikaachiwa baada ya mahakama ya Guateng kujiridhisha kuwa Hermanus alikosea kusajili "tuzo" yake mahakamani hapo (procedural irregularities). Sasa mkulima huyo amesajili "tuzo" hiyo nchini Canada, na ndio maana ndege yetu nyingine imekamatwa.

Jambo ambalo Kabudi anapotosha kwa makusudi ni kusema kuwa tulimshinda mkulima Hermanus Steyn on merit. Uongo mtupu. Kama tulishinda on merit why the matter is not res judicata?

Hatukumshinda Steyn on merit. Yani hatukumshinda katika kesi ya msingi ya kutaka alipwe fedha anazotudai. Tulimshinda kwa "technicalities" za kisheria (procedural irregularities) baada ya yeye kukosea kusajili tuzo hiyo kwenye mahakama ya Guateng.

Kwa lugha rahisi ni kwamba Hukumu ya mahakama kuu ya Tanzania iliyompa Hermanus tuzo ya $36M bado haijabatilishwa. Na Hermanus anaweza kuisajili tuzo hiyo katika nchi yoyote ya Jumuiya ya madola. Kwahiyo hata ndege ikiachiwa Canada, anaweza kusajili tuzo yake India, Kenya, Zambia, Australia, au nchi yoyote yenye mali za Tanzania zinazoweza kufikia thamani ya tuzo hiyo, na mali hizo kukamatwa.

Kwahiyo Kabudi anapoishangaa Canada, ni kukosa umakini tu. Ameongea kama "layman" ambaye hajui sheria kabisa. Vijana wa LLB1 pale UDSM, Mzumbe au SAUT wanamshangaa.

Mali zetu zimekamatwa zaidi Canada kwa sababu ndio nchi yenye mali nyingi za Tanzania kwa sasa (ndege zote za Bombadier zinatengenezwa huko). Hata Brazil ambapo Kabudi anashauri tukanunue ndege, zinaweza kukamatwa pia kama Steyn akiamua kwenda kusajili tuzo yake kwenye mahakama za huko.

Hivyo basi tunahitaji kupata suluhisho la kudumu badala ya kupiga 'ngonjera' kwamba kuna watanzania wanatumiwa na mabeberu kutuhujumu. Hakuna cha "beberu" wala "mbuzi jike" anayetuhujumu, ni makosa yetu wenyewe. Tutafute mbinu za kuyatatua badala ya kujificha kwenye visingizio vya mabeberu. Na tusimpotoshe Mheshimiwa Rais.

Nini kifanyike?
1. Serikali imuondolee mkukima Hermanus Steyn marufuku iliyompiga ya kuingia nchini. Ikumbukwe anahangaika huko nje kwa sababu amezuiwa kuja nchini. Kabla hajapigwa marufuku ya kuja Tanzania alikua anakuja kudai haki yake hapa. Alipozuiwa ndipo akaamua kuichukua "tuzo" yake mahakama kuu na kwenda kuisajili huko nje.

2. Kamati ya Chenge na Mkulo iitwe na kuulizwa msingi wa kupendekeza Steyn alipwe kiasi kidogo tofauti na "tuzo" aliyopewa na mahakama kuu. Kama sababu hizo zitakua na mashiko, zitumiwe kumshawishi Steyn akubali kiasi alicholipwa na kufuta shauri hilo mahakamani.

3. Kama serikali haikubaliani na option hizo mbili hapo juu, basi ikate rufaa au iombe "judicial review" kupinga hukumu iliyotolewa na mahakama kuu ya kumpa Steyn tuzo ya $36M. Na maamuzi yatakayotolewa kwenye rufaa hiyo yaheshimiwe na pande zote mbili.

Vinginevyo tutaishia kuwalaumu "mabeberu", kesho tutawalaumu "majogoo", keshokutwa tutawalaumu "mitetea" pasi na sababu zozote za msingi. Kama mkulima huyu kudai haki yake ni ubeberu basi Mahakamu kuu ya Tanzania ndio beberu kuu maana ndiyo iliyompa ushindi wa tuzo hiyo. Tuache porojo. Tudeal na msingi wa tatizo.

Tuanzie na sababu za Nyerere kutaifisha mali za Steyn, kisha twende kwenye hukumu iliyotolewa na mahakama kuu na kumpa ushindi. Then tumalizie na ripoti ya kamati ya akina Chenge. Halafu tumuite Steyn tukae nae mezani tuyamalize. Tuache kurukaruka kama maharage yaliyokosa maji.!

Malisa GJ
Nakumbuka enzi za Muammar Ghaddafi ni Libya pekee ndiyo ilikuwa haidaiwi. Sasa sikujua kama tumebaki watanzania pekee wenye madeni!!
 
Hili sakata la ndege yetu Kule Canada kukamatwa ni picha kali ambayo Uwenda ina chezeshwa na big secret agency aka mabeberu.

Hii picha nikama picha ya utani na picha ya mchezo wa kitoto ila mwisho wake inamadhara makubwa kwa uchumi wetu na taifa.

Hii picha imetengenezwa na watu wenye akili nyingi dhidi ya utawala wetu wenye watu wachache wanamshauri vibaya Rais au anajishauri vibaya.

Nipicha yamzaha kama ule mzaa wa Mr Ben ila mwisho unalia while unacheza. Hapa Usije Penda kuokotwa majalalani nakuwekwa na wakuu ule ila mwisho historia ikakuadhibu ukasema bora ningebaki jalalani.

Sisi waangaliaji wa huu mpira tunaona vile tutafungwa goli la masihara na refa kusema ni goli. Watu tutalia nakulia ila goli halitofutwa.

Upo msemo una tahadharisha juu yakupenda kupigiwa Makofi pia uwe tayari kuzomewa haya mataifa beberu wanajianda kuwa kituko watanzania na kuvuruga uchumi wetu na nisiwafiche wamesubiri siku chache baada ya uchaguz wa serikal za mitaa kuchezewa Rafu.

Kiukweli kama vile serikal yangu tukufu ulivyo cheza mchezo wa masihara nakuwa Acha wengi wakilia ndio hivyo hivyo hawa jamaa watakuchezea mchezo ule ule.

Hawasemi lolote kuhusu uchaguzi ila nao wanataka kutubana na vijisent tunajivunia nakutukata miguu mwisho tukafie mbele.

Taarifa za chini ya carpet tujiandae kisaikolojia maana watatucheze mchezo ule ule vyama vya siasa tumewachezea. Nimwendo wa mahakaman na kupigwa big fine mwisho kama asset zetu.

Mungu likumbuke Taifa letu Tanzania.
 
Unapoleta madai nyeti kama haya inabidi ubalance pande zote. Tunajua mawakili wake huyu mzungu na wanaoleta ukimbelembele wa madai haya ni hawa wenye majina ya akina MALISA.
Kwanza tuambie huyo mzungu hayo malaki ya maekari aliyapataje? Ni mzawa?

Alipora hiyo ardhi ya umma kwa unyonyaji wa kikoloni ndo maana Nyerere akaitaifisha. Hata hivyo kwavile baadhi ya ardhi alikuwa ameishaiendeleza na Mali zinazohamishika kama magari, ndege ndogo za tours, n.k. ndo maana Nyerere akamuachia kiasi fulani cha ekari (nyingi tu) kama fidia ya mali zinazohamishika na Huyo mzungu akutaka kuendelea na mgogoro na serikali ya Tanzania akakubali yaishe.

Nyie akina Malisa wapiga deal kwavile mnajua mna 10% ndo mnalianzisha ili mpige hela. Sasa sikia, kwa serikali hii kama kulipa italipa lakini sio rahisi kihivyo. Tunajua mnakopa hela nyingi tena kwa riba kufungua kesi ugenini mkidhani mtalipwa kirahisi na kurejesha mkopo.

Hiyo hela ina mawili kulipwa au kutolipwa: Kwanza huyo mzungu alishalipwa dola mil.20 na mwinyi ni zaidi ya miaka 35 hivi. Pili huyo mzungu aliachiwa hekari kibao na bado anazo anaendelea kuzimiliki. Sasa nyie mnataka cash kusudi mpate 10% lakini huyo mzungu anajua itakula kwake maana atanyanganywa ardhi ndo maana alikubali yaishe. Endelea kupima joto la serikali hii mkidhani mtapata hela ya bure. Why now?

Kwani nchi haina mali nje ya nchi miaka hiyo yoote mbona hazijawahi kuzuiwa? ATCL haikuwa na International routes kabla ya kufilisika mbona hatukusikia hawamu ya Mkapa, na Kikwete ndege zetu zikikamatwa?

Baadhi ya balozi zetu nje ya nchi hayo majengo tumejenga wenyewe ni mali zetu mbano hayajawahi kiwekewa kofuli kufidia? Nchi ina gold deposits kwenye benki ya dunia kureflect paper/coin money mbona hazijawahi kushikiliwa?

Ukweli ni kwamba myanya yooote ya wizi wa mali za umma na utakatishaji wa hela chafu na madawa ya kulevya, huo mtandao JPM kausambaratisha! Endeleeni kukopa hela kuendesha kesi mtaangukia pua! Shwaini!
Tusikimbilia kutafuta visingizio vya kisiasa. Hoja hii inatakiwa itazamwe kisheria na kiuhalisia.

Unasema, aliachiwa ardhi nyingine. Kama ndivyo, ataitumiaje hiyo ardhi wakati ana marufuku ya kuingia nchini?

Umeuliza kwa nini haikutokea huko nyuma wakati wa awamu nyingine, ingetokeaje wakati alikuwa anaruhusiwa kuishi nchini na kufanya shughuli zake? Ingetokeaje wakati serikali za awamu zilizopita, walikuwa wakimlipa kidogo kidogo kwa makubaliano waliyokuwa wamefanya?

Tusiwe wendawazimu wa kuamini kuwa kila anayebeba kinyume na tunavyotaka au tulivyotarajia, basi huyo anatumiwa au haupendi utawala uliopo. Tuzingatie hoja. Na tutende kwa kufuata sheria na siyo nguvu. Pundamilia au nyati wana nguvu kuliko simba kwa vile tegemeo lao ni nguvu na siyo akili, kila siku wanaliwa na simba ambaye uzito wake haufikii hata nusu ya uzito wa nyati.

Awamu hii imezidi mno kutumia nguvu na ubabe kuliko werevu na ujuzi.
 
Kwa namna ulivyojibu ni wazi nawe huna credibility ya kucomment nilichoandika, namanisha akili yako ni ndogo Sana kuelewa nilichoandika, kakojoe ulale.
Huyo nyani hapo kwenye avatar yako anaakili kuliko wewe.
 
Kwani nchi haina mali nje ya nchi miaka hiyo yoote mbona hazijawahi kuzuiwa? ATCL haikuwa na International routes kabla ya kufilisika mbona hatukusikia hawamu ya Mkapa, na Kikwete ndege zetu zikikamatwa?

JIBU NI: Walikuwa wanamlipa kwa awamu, huyu wa awamu hii alikata umeme na kumfukuza ndio sababu ya haya yanayoendelea
 
Unapoleta madai nyeti kama haya inabidi ubalance pande zote. Tunajua mawakili wake huyu mzungu na wanaoleta ukimbelembele wa madai haya ni hawa wenye majina ya akina MALISA.
Kwanza tuambie huyo mzungu hayo malaki ya maekari aliyapataje? Ni mzawa?

Alipora hiyo ardhi ya umma kwa unyonyaji wa kikoloni ndo maana Nyerere akaitaifisha. Hata hivyo kwavile baadhi ya ardhi alikuwa ameishaiendeleza na Mali zinazohamishika kama magari, ndege ndogo za tours, n.k. ndo maana Nyerere akamuachia kiasi fulani cha ekari (nyingi tu) kama fidia ya mali zinazohamishika na Huyo mzungu akutaka kuendelea na mgogoro na serikali ya Tanzania akakubali yaishe.

Nyie akina Malisa wapiga deal kwavile mnajua mna 10% ndo mnalianzisha ili mpige hela. Sasa sikia, kwa serikali hii kama kulipa italipa lakini sio rahisi kihivyo. Tunajua mnakopa hela nyingi tena kwa riba kufungua kesi ugenini mkidhani mtalipwa kirahisi na kurejesha mkopo.

Hiyo hela ina mawili kulipwa au kutolipwa: Kwanza huyo mzungu alishalipwa dola mil.20 na mwinyi ni zaidi ya miaka 35 hivi. Pili huyo mzungu aliachiwa hekari kibao na bado anazo anaendelea kuzimiliki. Sasa nyie mnataka cash kusudi mpate 10% lakini huyo mzungu anajua itakula kwake maana atanyanganywa ardhi ndo maana alikubali yaishe. Endelea kupima joto la serikali hii mkidhani mtapata hela ya bure. Why now?

Kwani nchi haina mali nje ya nchi miaka hiyo yoote mbona hazijawahi kuzuiwa? ATCL haikuwa na International routes kabla ya kufilisika mbona hatukusikia hawamu ya Mkapa, na Kikwete ndege zetu zikikamatwa?

Baadhi ya balozi zetu nje ya nchi hayo majengo tumejenga wenyewe ni mali zetu mbano hayajawahi kiwekewa kofuli kufidia? Nchi ina gold deposits kwenye benki ya dunia kureflect paper/coin money mbona hazijawahi kushikiliwa?

Ukweli ni kwamba myanya yooote ya wizi wa mali za umma na utakatishaji wa hela chafu na madawa ya kulevya, huo mtandao JPM kausambaratisha! Endeleeni kukopa hela kuendesha kesi mtaangukia pua! Shwaini!
Maraisi waliopita pita kila mtu kwa awamu yake walilipa kwa sehemu deni halikwisha na lina riba awamu ya tano imemfukuza asikanyage TZ hukumu ya mahakama IKO PALE PALE ..mahakamani huulizwi hayo ya gold deposit majengo ya balozi huko nje yeye ameamua ndege ndio chaguo lake shida ni serikali kwenda kuzikomboa mbona ile ya kwanza huko huko Canada walimalizana tena kimya kimya?Ni vyema kumalizana na mkulima kuliko serikali kuendelea kuvutana na huyo mkulima,ni kulifedhehesha taifa.
 
Back
Top Bottom