TTCL lipeni wafanyakazi wenu, wanaadhirika mitaani

Mambo ya Udini mimi sikuwa nayajua, ni wenyewe kwa wenyewe walikuwa wanaongea. Siwezi kuthibitisha mimi nimenukuu maongezi yao

Sina uhakika na taarifa yako.

Na sioni ni kwa jinsi gani mtu atampigia mwenzake ili kukuhakikishieni nyie kwamba hajalipwa na waongee mengi hivyo.
 
Kwa kawaida mshahara wa kumi na tatu ( nauli ya likizo) hulipwa mwezi December Mara tu baada ya x mass. Ikumbukwe mshahara wa December hulipwa na ulilipwa kabla ya Xmas.

Kilichotokea mwaka huu ni uchelewesho wa malipo hayo na wafanyakazi walijulishwa kuhusu hali hiyo.

Nasikia yalikuwa maelekezo kutoka serikalini na kwamba wafanyakazi wangelipwa Mara tu watakapopata "mwongozo" toka serikalini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee! Kwaiyo huo mshahara wameshalipwa? Maana lingekuwa ni jambo lake tu ningemkomalia lakini kawapigia wenzie na wote wanalia vilio vinavyofanana...kuweni na huruma jamani
 
Mleta mada una lako jambo. Tatizo lako liweke wazi tu. Ni dini ya huyo bosi na mdhahara wake kuwa million saba. Kwani wa dini hiyo awe analipwa zaidi, au siyo?

Hilo la baba'ko na kodi umezuga tu.

Unakuwa zaidi ya Pascal Mayalla kwa ufataani. Post ya kwa na ufataani. Kwankni usije na id yako tu.

Halafu tazama bichwa lako la habari unavyoharibu Kiswahili. Ni wale wale tu, hakuna zaidi.
kWANI HUYO KIONGOZI NI DINI GANI?
 
Nimesoma Comments zote, sijaona hata Comment moja ya mtu anayeonyesha ni mfanyakazi wa TTCL au Mke au Mume wa mfanyakazi wa TTCL anayeweza kuthibitisha kuwa WAMELIPWA. Lakini mimi ninachokisemea ni huruma tu ya watu hawa ambao wanaaibika mitaani wakati tunaona kampuni inatoa MABILIONI serikalini.
Masuala ya Udini na mengineo ya upendeleo yanaweza yakaonekana madogo lakini je, WAMELIPWA? na hili jambo lisichukuliwe kishabiki watu wanashindwa kusomesha watoto wala kulipa kodi za nyumba watu mnaleta utani?
 
Hilo la dini si umeandika wewe post yako ya kwanza, au umeshasahau?

Ungekuwa haufahamu ilihusu nini wewe kuandika kuhusu dini?
Kumbuka mimi sio mfanyakazi wa hiyo kampuni mimi nimempangisha mfanyakazi wao, na nimenukuu maneno waliyokuwa wakiongea mpangaji wangu na mmoja wa aliokuwa akiongea nae huku laud speaker ikiwa on
 
Nimesoma Comments zote, sijaona hata Comment moja ya mtu anayeonyesha ni mfanyakazi wa TTCL au Mke au Mume wa mfanyakazi wa TTCL anayeweza kuthibitisha kuwa WAMELIPWA. Lakini mimi ninachokisemea ni huruma tu ya watu hawa ambao wanaaibika mitaani wakati tunaona kampuni inatoa MABILIONI serikalini.
Masuala ya Udini na mengineo ya upendeleo yanaweza yakaonekana madogo lakini je, WAMELIPWA? na hili jambo lisichukuliwe kishabiki watu wanashindwa kusomesha watoto wala kulipa kodi za nyumba watu mnaleta utani?
Tuondolee ujinga humu. Kama una malalamiko peleka TTCL.
 
Kumbuka mimi sio mfanyakazi wa hiyo kampuni mimi nimempangisha mfanyakazi wao, na nimenukuu maneno waliyokuwa wakiongea mpangaji wangu na mmoja wa aliokuwa akiongea nae huku laud speaker ikiwa on
Sasa mpangaji wa babako anahusiana nini na dini ya viongozi wa TTCL? Kama babako hajalipwa ni yeye na babako siyo TTCL wenye shida.

Huu ujinga mwengine muwe wa wazi tu.

Fumbo mfumbie mjinga.

Wewe ni nyoka tu ambae unachuki binafsi hauna cha mpangaji wala kodi.
 
We jamaa Muongo Sana.
Hakuna uwongo hata kidogo. Kuwa na uchungu na maisha ya watu

Sasa Kwa mfano ni kweli, huyo mpangaji wenu anapata mshahara shilingi ngapi? Maana umesema anasubiri mshahara wa December huo huo awapeleke watoto wake shule (Ada na mahitaji yote ya shule) alafu mshahara huo huo awalipe Kodi yenu ya mwaka (umesema analipaga December miaka yote).
Unajua analipwa kiasi gani na kodi yetu ya pango ni kiasi gani? Unajua ana akiba kiasi gani au ameahidiwa kusaidiwa kiasi gani akiongeza na mshahara wake atafanikisha kiasi gani? Kuwa na huruma

Hapa kuna kitu hakiko Sawa, eiza kuwachafua TTCL au kuingiza udini bila sababu..
Ili nipate nini? Sina hata line yao wala situmii huduma yao hata moja, nawachafua ili iweje? Uliza, wamelipwa? Iwapo hawajalipwa, wanajichafua wenyewe

Mwisho kabisa, tukiashumu ni kweli jamaa hajalipa Kodi, hebu kuwa kijana. Mzee wako alihangaika katika umri wako akajenga nyumba anapangisha watu wewe unaamka asubuhi unasubiria TTCL walipe mshahara nawe ukinge kupitia mgongo wa Mzee. Mnaipigia hesabu hela ya mzee Hadi senti tano ya mwisho, Mzee anashindwa hata kununua suruali au kumpa mchepuko wake

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante kwa ushauri
 
Sasa mpangaji wa babako anahusiana nini na dini ya viongozi wa TTCL? Kama babako hajalipwa ni yeye na babako siyo TTCL wenye shida.

Huu ujinga mwengine muwe wa wazi tu.

Fumbo mfumbie mjinga.

Wewe ni nyoka tu ambae unachuki binafsi hauna cha mpangaji wala kodi.
Asante kwa maoni yako, nayaheshimu pia
 
Mzee wangu amempangisha Mfanyakazi wa TTCL anayefanyia tawi la jirani na Kiwanda cha Sigara ambaye kila Mwaka ikifika December hulipa kodi yake bila usumbufu kwa miaka mitatu aliyokaa na sisi huku akiendelea na ujenzi wa nyumba yake huko mbagala Kongowe.

Tangu tarehe ya kodi ilipofika mpangaji wetu amekuwa na sound nyingi mara atalipa mwisho wa mwezi mara mwanzoni mwa Januari lakini hadi leo watoto wake wamfungua shule ameshindwa kuwapleka shule na hana dalili yopyote ya kuwapeleka shule.

Lakini jana jumapili tarehe 5 mzee na mimi tuliwendea na notice ya kutaka atuachie nyumba yetu maana mzee nae anategemea kodi hiyo hiyo ili apelike madogo shule lakini tulichokutana nacho kimetushangaza sana.

Mpangaji wetu alisema hawajalipwa MSHAHARA na mimi na mzee tulimbishia sana kwamba haiwezekani kampuni ya simu inatowa gawio hadi la shilingi Bilioni Mbili lishindwe kuwalipa mishahara.

Kwa kututhibitishia aliwapigia wafanyakazi wenzie kama watano kwa kuweka LOUD SPEAKER na wote hao kwa masikio yetu tulisikia wakiwa na malalamiko yanayofanana wakilaumu uongozi wa kampuni hiyo kuwatendea unyama kwa kutowalipa mishahara.

Wafanyakazi hao wengine walionekana ni wau wazima walikuwa wanalalamikia boss mmoja (jina kapuni kwa sasa) kuwa ni dikteta, hana utu na ana upendeleo wa kidini na ndiye anayefanya wafanyakazi wadhalilike mitaani.

Wafanyakazi hao kila mmoja kwa namna yake walilalamika kushindwa kuwapeleka watoto wao mashuleni, wengine kushindwa kulipa madeni wengine kodi za nyumba ilimradi kila mmoja na manung'uniko yake.

Kampuni ya simu inakumbushwa kuwa Wafanyakazi wanaishi kwenye jamii na hivyo wanajikuta wanapata usumbufu kutokana na kushindwa klipa madeni muhimu.

Isingekuwa huyu mpangaji kuwapigia wenzie hadi wa mikoani jana ilikuwa ni siku ya mwisho kukaa na sisi maana tulishamwambia dalali atutafutie mpangaji mwingine.

Mimi siamini kama TTCL inaweza kuwakalisha wafayakazi wake muda mrefu bila kuwalipa mishahara isipokuwa ni management kupuuza mchango wa wafanyakazi na kama walivyokuwa wakiongea kwenye simu kuwa wenyewe wanalipana mishahara mikubwa ya hadi shilingi Milioni saba kwa mwezi hawawezi kujali shida za wafanyakazi wanaopata shilingi laki saba kwa mwezi.

Mpangaji wetu leo hii watoto wake wawili wamshindwa kwenda shule hawana ada.

TTCL LPENI MISHAHARA WAFANYAKAZI WENU WANAADHIRIKA HUKU MITAANI.
Mbona wamelipa Gawio bilioni na Haku mambo sio mazuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom