TTCL lipeni wafanyakazi wenu, wanaadhirika mitaani

vitz14

Senior Member
Dec 27, 2013
114
250
Kwa kawaida mshahara wa kumi na tatu ( nauli ya likizo) hulipwa mwezi December Mara tu baada ya x mass. Ikumbukwe mshahara wa December hulipwa na ulilipwa kabla ya Xmas.

Kilichotokea mwaka huu ni uchelewesho wa malipo hayo na wafanyakazi walijulishwa kuhusu hali hiyo.

Nasikia yalikuwa maelekezo kutoka serikalini na kwamba wafanyakazi wangelipwa Mara tu watakapopata "mwongozo" toka serikalini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu mwenzetu alikuwa keshapanga mshahara wa 13 aende beach kidimbwi kitu kimegoma anasingizia hawajalipwa mshahara,TTCL tarehe 15 nauli kapaa,tar 20 advance kapaa tar 25 mzigo mzima unaingia mtu anasema hawalipwi mshahara,huyo mpangaji wenu anafanya kazi labda chemichotex

Sent using Jamii Forums mobile app
 

vitz14

Senior Member
Dec 27, 2013
114
250
Kaswali kazuri sana...huyo mtu watu wa dini yake anawapandelea wapi directors ni dini wote wa dini yake mmoja tena mama wa watu ana acting,meneja wote wa makao makuu dini yake mmoja tena ana act.watu watufe madhaifu ya bosi wao waseme sio kuzunguka tu.come back home kumeswiting
Kwahiyo huyo mkuu watu wa dini yake anaowapendelea washalipwa ila hawa wadini nyingine ndio bado wanaisoma namba!

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
17,671
2,000
Mzee wangu amempangisha Mfanyakazi wa TTCL anayefanyia tawi la jirani na Kiwanda cha Sigara ambaye kila Mwaka ikifika December hulipa kodi yake bila usumbufu kwa miaka mitatu aliyokaa na sisi huku akiendelea na ujenzi wa nyumba yake huko mbagala Kongowe.

Tangu tarehe ya kodi ilipofika mpangaji wetu amekuwa na sound nyingi mara atalipa mwisho wa mwezi mara mwanzoni mwa Januari lakini hadi leo watoto wake wamfungua shule ameshindwa kuwapleka shule na hana dalili yopyote ya kuwapeleka shule.

Lakini jana jumapili tarehe 5 mzee na mimi tuliwendea na notice ya kutaka atuachie nyumba yetu maana mzee nae anategemea kodi hiyo hiyo ili apelike madogo shule lakini tulichokutana nacho kimetushangaza sana.

Mpangaji wetu alisema hawajalipwa MSHAHARA na mimi na mzee tulimbishia sana kwamba haiwezekani kampuni ya simu inatowa gawio hadi la shilingi Bilioni Mbili lishindwe kuwalipa mishahara.

Kwa kututhibitishia aliwapigia wafanyakazi wenzie kama watano kwa kuweka LOUD SPEAKER na wote hao kwa masikio yetu tulisikia wakiwa na malalamiko yanayofanana wakilaumu uongozi wa kampuni hiyo kuwatendea unyama kwa kutowalipa mishahara.

Wafanyakazi hao wengine walionekana ni wau wazima walikuwa wanalalamikia boss mmoja (jina kapuni kwa sasa) kuwa ni dikteta, hana utu na ana upendeleo wa kidini na ndiye anayefanya wafanyakazi wadhalilike mitaani.

Wafanyakazi hao kila mmoja kwa namna yake walilalamika kushindwa kuwapeleka watoto wao mashuleni, wengine kushindwa kulipa madeni wengine kodi za nyumba ilimradi kila mmoja na manung'uniko yake.

Kampuni ya simu inakumbushwa kuwa Wafanyakazi wanaishi kwenye jamii na hivyo wanajikuta wanapata usumbufu kutokana na kushindwa klipa madeni muhimu.

Isingekuwa huyu mpangaji kuwapigia wenzie hadi wa mikoani jana ilikuwa ni siku ya mwisho kukaa na sisi maana tulishamwambia dalali atutafutie mpangaji mwingine.

Mimi siamini kama TTCL inaweza kuwakalisha wafayakazi wake muda mrefu bila kuwalipa mishahara isipokuwa ni management kupuuza mchango wa wafanyakazi na kama walivyokuwa wakiongea kwenye simu kuwa wenyewe wanalipana mishahara mikubwa ya hadi shilingi Milioni saba kwa mwezi hawawezi kujali shida za wafanyakazi wanaopata shilingi laki saba kwa mwezi.

Mpangaji wetu leo hii watoto wake wawili wamshindwa kwenda shule hawana ada.

TTCL LPENI MISHAHARA WAFANYAKAZI WENU WANAADHIRIKA HUKU MITAANI.
Wameshalipwa.
*Thread closed*
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom