TTCL kupata fursa ya kupeleka internet nchini Burundi, wewe kama mtumiaji wa internet unaonaje huduma hapa nchini?

Oct 12, 2019
28
15
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) na Kampuni ya Mkongo wa Taifa ya Burundi (BBS) wamesaini mkataba wa miaka 10 wenye thamani ya TZS Bil. 13.8.

Burundi sasa itaanza kunufaika kwa mawasiliano ya uhakika ya simu kwa kushirikiana na Tanzania.
 
Hapa nyumbani sijaona faida ya moja kwa moja kwa mimi mchumia tumbo ila sijui kwa mabepali hapo juu..!
 
Kuna utofauti wa huduma za data( internet) zitolewazo kati TTCL na NICTBB, ingawaje wote ni kitu kimoja...

TTCL kama kampuni ya simu wao wanatoa huduma za mobile data kupitia line za simu na minara ya simu. Hapa wanafanana sawa tu na Tigo, Airtel n.k

NICTBB almaarufu kama mkongo wa Taifa wa mawasiliano, huu ni mfumo wa mawasiliano wenye mtandao uliounganishwa kupitia fibre, na kazi kubwa ni ubebaji wa mawasiliano ikiwemo internet...

Hivyo basi bila shaka, Warundi watakuwa wameungwa kwenye NICTBB ili waweze unganishwa na Internet Cloud toka nje, maana yake hapa TTCL/NICTBB atakuwa kama mbebaji na hiyo ni biashara...

Back
Top Bottom