TTCL fungueni official account JamiiForums

TTCL fungueni official account JamiiForums

Wasipokuwa makini watapata hasara maana kuingia saturated market inabidi uwe na kitu kipya tofauti na waliokutangulia
Mfano wale wazee wawatoe kabisa waweke vijana

Waondoe uccm waweke watu wenye taaluma zao
 
Wapo vizuri kwa kweli! kifurushi chao cha 290000 per month kipo poa, ila tu waache kutuhujumu kwa kupunguza speed kikikaribia kuisha!
 
Wafufue zile call booth zao kwenye shule za sekondari vyuoni na mitaani
 
Inavoonekana mitambo hii ya GSM 'area coverage' yake ni fupi ukilinganisha na ile ya CDMA. Hapa nilipo Tabora sehemu ya Ipuli CDMA haikuwa na shida hata kidogo, sasa hii GSM 'signal' wakati mwengine sipati kabisa na bahati mbaya nina kifurushi cha wiki nilichojiunga nikiwa Dar. Tafadhari tatueni tatizo hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Natumia hii line takribani ni miezi 2 tatizo kubwa/kero ni sisi tunaoishi maeneo ya nje mwa mji hapa dar.
Nawaomba ttcl wafanye coverage kubwa kwa hapa dar kwanza ndipo waanze huko mikoani
 
Gharama za kutuma na kupokea pesa kulinganisha na mitandao mingine ziwe chini...hii itasaidia kuwavutia wateja wengi kwani makato ya sasa ni kilio kwa wateja sema hakuna altenatives ukizingatia watz wengi hawaamini katika kuweka fedha benki...

wajitahidi pia kuwa na marketing team kubwa kuwashawishi wateja wengi hasa vijijini ambapo watu ni rigid kuswitch kwenda huduma nyingine toka huduma moja.....huwezi amini kuna watu mpaka leo hawajui kwamba TTCL wanahusika na nini...

juzi nipo maeneo fulani ndani ya DSM nikaulizia vocha za TTCL kwenye vibanda vya vocha wananishangaa...hawaelewi chochote kuhusu huduma za TTCL....Waandae marketing strategy ya kuwafikia walengwa kwakweli la sivyo itaendelea kuwa sleeping giant...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Panahitajika wataalamu wa Marketing ili kuvutia wateja maana siku hizi hii mitandao mengine wanafata mpka majumbani kusajili watu laini nadhani na wao TTCL inawabidi wabadilike wasisubiri wateja wawafate kwenye ofisi zao
 
Panahitajika wataalamu wa Marketing ili kuvutia wateja maana siku hizi hii mitandao mengine wanafata mpka majumbani kusajili watu laini nadhani na wao TTCL inawabidi wabadilike wasisubiri wateja wawafate kwenye ofisi zao
Kuna wengine wanasimama na mabango asubuhi kiukweli sijisikiagi vizuri kuona vijana wenzangu wakifanya vile..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Awali ya yote kwa hili la kuinunua na kuifanya % ya serikali/wananchi. Wakifanya na Haya Pía yatasaidia kuikuza tena hio kampuni.
1--- wasilazimishe kujenga minara yao kila sehemu, waingie ubia / wakodi minara ya kampuni nyengine ili mtandao wao uwepo nchi nzima ( Zantel na Tigo, haidhuru Zantel ni ya Tigo). Wajipange ili nao wapate minara yao.
2--- mawakala, waweke huduma karibu na wananchi, wapate mawakala wa huduma zao kila sehemu, washirikiane na kampuni za huduma za jamii, Tanesco, kulipia Ada za sehemu mbali mbali n.k
3----Wajitangaze Sana, redioni, TV na hata matamasha na mijumuiko mbali mbali.
4--- waweke Bei rahisi ( iwe ya kudumu lakini ) kwa maana wao ni wwuzaji wa jumla wa mawasiliano ya fibre / mkonga.
5 --- mengi yamesemwa na wadau hapo juu.
 
Wapo vizuri kwa kweli! kifurushi chao cha 290000 per month kipo poa, ila tu waache kutuhujumu kwa kupunguza speed kikikaribia kuisha!
Vifurushi vyao vipo bomba sana, hawaibi bundle(ukipewa 6GB utazitumia na hutojuta coz hauhisi kama zinaisha bila sababu)

Binafsi nimependa speed yao, hata ukuingia YouTube unatizama video bila buffering za kijinga.

Wajitahidi kusambaa maeneo yote nchini (wana mkongo wa taifa so it's easy), watoe promotion kila mara ili kuvutia wateja, wajitahidi kusambaza vocha zao maeneo yote(sasa hivi nikitaka vocha hadi maxmalipo au mpesa)

Binafsi nimesharudi nyumbani[emoji12]
 
Kwanza wangeanza kuhamsisha watu watumie line zao kwa sababu mpaka sasa katika ya watumiaji wa simu 50 labda unaweza kukuta 2 ndio wanatumia ttcl,utaanzisha huduma ya pesa kwenda kwa nani? Wanatakiwa waanzie chini sio juu kama walipo sasa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom