TTCL bado mnarudia makosa, tatizo ni nini?

TTCL bado mnarudia makosa, tatizo ni nini?

Hakuna kitu kinaniuma kama kuona mashirika ya umma yanashidwa kushindana na mashirika binafsi. Serikali imeonekana inania nzuri yakufufua hili shirika ila ndani yashirika nahisi kunawatu hawataki kubadilika pengine kwa manufaa yao binafsi. Shirika linahtaji mawazo mapya ili liweze kushindana na mashirika binafsi, kwa waliowahi kufanya IPT zao TTCL watakubaliana na mimi.
Mkuu unawaza kwa uyakinifu sana.
Ujue nchi hii ni ya ajabu sana.
Juzi tu serikali imewafurusha menejimenti nzima baada ya kuona mdororo wa kiuendeshaji usio na tija.

Cha kushangaza hawa waliowekwa sasa ni bora hata waliotimuliwa maana hawana jipya.

Kwa utendaji wa kibiashara za kusuasua namna hii, hata tunajiuliza hilo gawio walilojipretend kwa mh. Magufuli walichomoa mifukoni mwao kama shoo ili wajilipe baadaye?

Kampuni kubwa namna hiyo linashindwaje ubunifu na vijikampuni vidogovidogo vya binafsi?
Hapo lazima kunabgenge la walaji linaloendeleza umumiani wao.
 
Nakumbuka Mh. Pro. Mbarawa aliwaambia wawekeze kwenye data, ni ukweli usiopingika mahitaji ya data kwa sasa ni makubwa sana kwenye duniaa hii ya technolojia hivyo ni rahisi kutengeneza faida kubwa kwa mda mfupi, kinachotakiwa ni efficiciency and realiability ya huduma zao, soko bado lipo kubwa sana maana hawa wengine nao hawapo sawa sana kwenye hii nyanja.
 
Back
Top Bottom