Sakasaka Mao
JF-Expert Member
- Sep 29, 2016
- 15,963
- 23,264
Mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu, kumekuwa na taarifa za kibiashara toka kampuni ya Ttcl za kuvutia wateja kwenye mitandao ya mawasiliano nchini, kwa kauli mbiu yao ya "rudi nyumbani kumenoga".
Kumevunjwa bodi, kupinduliwa menejimenti, kuua matumizi ya vifaa vya mawasiliano vya analogia bila kutoa fidia kwa wateja katika shirika hilo la mawasiliano la umma kwa muktadha wa kuboresha na kuleta madiliko chanya kwenye sekta hii, lakini mambo ndivyo sivyo.
Mambo ni ya hovyo, upatikanaji wa huduma ni wa hovyo hovyo.
Walianza kwa ahadi za kuboresha na kusimika minara ya kuongeza nguvu ya masafa ya mawasiliano nchi nzima, lakini hadi leo ni miji michache sana yenye 'coverage' ya Ttcl.
Maeneo ya 'mikoani' ni maeneo machache sana kutoka zilipo 'installations' zao unaweza ukatumia mawasiliano ya Ttcl.
Huyo mdudu anayelibungua shirika hili la mawasiliano ya taifa anaonekana kuwa ana nguvu mno,sazingine kuliko hata serikali, maana hawajamgundua na wala hawajihangaishi kumtafuta, ni kwa nini?
Tuseme hawaielewi 'challange' hii, hapana kuna kitu nyuma ya pazia.
Kutokuwa wabunifu wa kibiashara na kuendeleza ukiritimba wa kuleta line zenye kubagua simu za 3g, pamoja na kushindwa kusimika minara ya kuboost mawasilano ni aina ya uhujumu uchumi mamboleo, unaofanywa kijanja kwa makusudi na menejimenti kwa kijifanya hawaelewi, kwa manufaa yao binafsi.
Nyumbani kunanogeshwaje bila ya kuondoa ukiritimba wa ovyo na uboreshwaji wa huduma?
Kiuhalisia mambo yalivyo ni tofauti na propaganda zao wanazotulisha wananchi kila uchao!
Nadhani serikali inatakiwa kuangazia jicho lake la tatu katika kampuni hii ya umma, kuna matatizo.