Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Hii ishu imekuwa kubwa mpaka taasisi ya Serikali inatoa tamko ni udhaifu mkubwa sana kwa upande wetu kama nchi kisa Mwanamke mmoja hata asiyekuwa na jina kasema kwamba Olduvai Gorge iko Kenya, tumewekeza siku ya tatu leo tunalia kila mahali kulalamika kana kwamba akirudisha kauli yake huyo mdada kuna chochote kitakachobadilika!
Hivi tunvyoongea Kisiwa chetu kimeuzwa kinyume na sheria zetu za nchi na Maliasili kwa Mzungu wa AK na kufika huko unahitaji Milioni 20/ siku na ni wazi hakuna Mtz atakayekwenda huko, Madini yetu kama Dhahabu, Shaba, Makaa ya Mawe yanaibiwa kila siku na Wazungu na Wachina yenye dhamani ya mabilioni ya shilingi ambayo yangeweza kutumika kutupunguzia ukali ya Maisha kwa kiasi kikubwa sana, Mwarabu wa Uarabuni kakabidhiwa ardhi kubwa sana inajulikana kama Loliondo na ukifika huko simu yako inakwambia kwamba karibu UAE, ukienda Serengeti kuna Uwanja wa ndege umejengwa na Wazungu Kinyume na sheria zetu za nchi na haumsaidii Mtz wa kawaida kwa chochote hivyo laiti kama tungewekeza hata tu sehemu ya nguvu tunazowekeza kwenye kumshambulia huyu dada na nchi ya Kenya kwenye kutetea Rasilimali zetu hakika tungefika mbali!
Hivyo narudia tena tuache upuuzi Kenya siyo adui wa TZ na wala nchi ya Kenya siyo ambayo inaiibia TanZania bali wanaoiibia TZ ni Wazungu, Waarabu, Wachina na wanasiasa wetu, kuchukia Wakenya ni kuendeleza ujinga wetu kama Waafrika kwani hata Wakenya nao ni victim wa ubebari kama sisi vile vile na tunachopaswa kufanya ni kuungana kwa pmj kushirikiana kwa manufaa ya Afrika yetu na siyo kubomoana, wengine wote wanajengana Waasia, Wazungu, hata Waarabu sisi tumekazana kuchukiana!
Narudia tena TTB acheni utoto kuna mambo muhimu ya kutetea kama Kisiwa chetu kuuziwa Mzungu, Loliondo yetu kupewa Mwarabu na siyo sijui dada gani wa Kenya kasema Olduvai iko Kenya!!