Fixed Point
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 11,304
- 12,753
Poleni na majukumu wanaMMU...
Leo hili jambo la trust kwenye mahusiano limekuwa likijirudiarudia sana katika kichwa changu. Mahusiano mengi sana yanavunjika sababu ya kukosa uaminifu. Kuna vitu vingi nimekuwa nikijiuliza na kujijibu na vingine kukosa kabisa majibu. Kwa mtazamo wangu UAMINIFU ni jambo muhimu sana katika mahusiano. Mara nyingi napenda sana niwe katika hali ambayo namuamini mpenzi wangu, pia napenda sana kwa gharama yoyote ile kumfanya mpenzi wangu aniamini. Kama nikigundua ana wasiwasi na kitu ninachomwambia huwa najitahidi kumwuliza aniambie nifanye nini ili aniamini sababu sipendi akae akiwa na wasiwasi, na ukweli nitafanya hicho kitu ili tu aridhike.
Inawezekana mimi nipo complicated kidogo, huwa napenda sana mtu aniambie ukweli hata kama ni mbaya kiasi gani. Kwa kuujua ukweli nakuwa na uhuru wa nini la kufanya baada ya hapo.... kukusamehe na kuendelea na mahusiano au kukusamehe na kusitisha mahusiano (kusamehe kwangu huwa siyo option, lazima nisamehe ili niweze kuendelea na mambo yangu mengine).
Katika huu uzi nitazungumzia sana uaminifu wa mambo ya kawaida tu, siyo kutoka nje ya mahusiano (cheating). Utakuta sometimes mtu anaamua tu kudanganya kwa sababu yoyote anayoijua. Kwa mfano mtu anamwambia mpenzi wake naenda sokoni wakati anaenda salon, au naenda kwa dada wakati anaenda kwa shangazi.
Hivi ikatokea ndo upo kwa shangazi halafu dada akaja nyumbani kukuulizia wakati wewe uliaga kwenda kwa dada itakuwaje? hata kama kweli mpenzi ataamini kuwa ulikuwa kwa shangazi, utakuwa umejenga hisia gani kwake kuhusu wewe? kwa nini umdanganye?
Wenzangu mnalizungumziaje hili?
Karibuni kwa mjadala