Trump tested positive for Coronavirus

Mkuu andika kwa utulivu tuelewe
Habari ndiyo hiyo.
Kwamba Trump, mdharau corona, sasa naye ni mhanga wa corona. Aombe sana isiwe na nguvu na kumtenda, kama ilivyowatenda raia zake zaidi ya laki mbili sasa.
 
Rais Donald Trump wa Marekani amesema kwamba yeye na mke wake Melania Trump wamepatikana na virusi vya corona na wako kwenye karantini.

Ametoa tangazo hilo kwenye mtandao wa Twitter.

Tangazo hilo linawadia baada ya Bwana Trump na wasaidizi wake wawili kuthibitishwa kuambukizwa virusi vya corona.

Hope Hicks, 31, mshauri wa rais amekuwa msaidizi wa karibu wa Bwana Trump kupatikana na virusi vya corona hadi hivi sasa.

Bi. Hicks alisafiri na Bwana Trump kwa ndege ya kijeshi kwenda kwenye mdahalo wa Televisheni alipokabiliana na mpinzani wake Joe Biden Jumanne.

Baadhi ya familia ya Trump ilihudhuria mdahalo huo walionekana wakiwa bila barakoa.


•Tonight, @FLOTUS and I tested positive for COVID-19. We will begin our quarantine and recovery process immediately. We will get through this TOGETHER!•


Bado haijafahamika vile kuthibitishwa kwa Bwana Trump kutaathiri maandalizi ya mdahalo wa pili wa urais, ambao umepagwa kufanyika Oktoba 15 huko Miami, Florida.


Bwana Trump mara nyingi huwa havai barakoa na amekuwa akipigwa picha akiwa hazingatii hatua ya kutokaribiana akiwa na wasaidizi wake au watu wengine wakati wa ziara zake rasmi.

Daktari wa Bwana Trump Sean Conley, alitoa taarifa ikisema rais na mke wake wote wanaendelea vizuri na wanapanga kusalia nyumbani ndani ya Ikulu wakati wa kipindi chao cha kuendelea kupona.

"Muwe na uhakika natarajia Rais aendelee kutekeleza majukumu yake bila matatizo yoyote wakati anaendelea kupata afueni, na nitaendelea kuwafahamisha matukio yoyote ya siku za usoni," taarifa hiyo imesema.

Bwana Trump sio Raisi wa kwanza duniani kukutwa na virusi vya corona. Mapema mwaka huu, Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson na Jair Bolsonaro wa BrazilView attachment 1587834
 
Sasa Trump akiwa na Covid-19 na umri umeenda vile hata asipokufa, itamtesa sana.
 
Hiyo ni taarifa kutoka Marekani. Mungu awaponye na kuwarejeshea afya zao. Tuwaombee ili Mungu aingilie kati
 
Alisema ni Virus vya Kichana . hahahah! Trump get a strap!
 
Wewe kweli una matatizo kichwani,Covid-19 haichagui.
 
Pole yao



Wasirudie kuifatilia (kudukua)Tanzania
 
Kwani whats so special kwa Trump mpaka iwe ajabu akipata corona. Nani kakwambia corona ni adhabu, mfano au somo. Nyinyi ndio uwa mnashangilia mtu akipata HIV kwamba alikuwa mzuri ila kaupata.
 
Pona Yao ni pale watakapoacha kumwona Magufuli ni adui Wao Kwa kuwa tu analinda maslahi ya nchi yake

Pona Yao, waache kuitisha TANZANIA kuhusu mambo yake yenyewe

Wakizidisha kuitishia Tanzania kuhusu Magufuli hasa wakilenga wizi wa madini yetu kupitia mtu Fulani, na huyo OmpePo atawekwa karantini Kwa korona, na huyo ziloba Wao hapa nchini itampata Corona

Uonevu Wao Kwa kisingizio cha demokrasia huku Wao wakionesha dhahili demokrasia imewashinda, watajuta kuifahamu TANZANIA,

Mungu atawaadhibu
 

Baadhi ya watu wachache humu jukwaani tayari walikuwa wameshatoa mapendekezo kwamba Marekani wanatakiwa waahirishe uchaguzi Korona ipite kwanza halafu ndiyo waendelee na mchakato huo hapo baadaye. Kuna mambo mengi yanachangia kwenye hili kubwa ikiwa ni afya za watu pamoja na uwezekano wa uwepo wa wizi wa kura usiotarajiwa, kama wataamuua kupiga kura kwa njia ya Posta. Mh. Rais Trump mwenyewe ameonyesha wazi kabisa kuwa haridhiki na utaratibu wa kupiga kura kwa njia ya posta na kwa hili yuko sahihi kabisa kwa upande wangu mimi, lakini watu hawamwelewi, nadhani pengine labda mahasimu wake wa kisiasa wanaona atafaidika sana kupata muda wa nyongeza Ikulu akiwa anasubiria korona iishe halafu ndiyo uchaguzi ufanyike.
Mimi ningependa tu kuwashauri hawa ndugu zetu mambo kadhaa kama yafuatavyo hapa chini. Ni kwa sababu ninaipenda Marekani na wa-Marekani pia

MOJA: Korona ni janga la asili na analoli-control Mungu kwa kiasi kikubwa sana na hivyo ningewaomba sana walipishe janga hili lipite kwanza halafu ndiyo warudi tena kwenye utaratibu mwingine wa kawaida, zikiwemo pilika pilika za uchaguzi

MBILI: Kama utaratibu wa Katiba yao unaruhusu, basi nashauri watengeneze kama Serikali ya mpito wakiwa bado wanasubiria uchaguzi, iwapo tu hawaridhiki na swala la kumuongezea muda Rais Trump aliyepo madarakani kwa sasa

TATU: Korona ni janga la dunia, pamoja na kwamba kuna baadhi ya sehemu limeshaisha. Naomba watu waendelee kukumbuka hili ili wanapokuwa wanafanya mambo yao, waendelee kuyafanya kwa tahadhari hiyo. Wasipofanya hivyo, kuna uwezekano likaja likatugharimu tena maisha ya watu wengine tofauti na matarajio na makisio yetu na tuliyokuwa nayo hapo awali wakati janga hili linaingia. Yaani itakula kwetu zaidi ya tulivyotarajia. Marekani ipo mpaka siku Yesu anarudi, haraka ya uchaguzi ya nini wakati mchakato huo kwa sasa unahatarisha afya za watu?

Hiki kilichotokea kwa sasa ni warning kutoka kwa Mungu kuwa hapendi uchaguzi huo ufanyike wakati huu wa Korona. Ni ushauri tu lakini

Nawatakia uponyaji wa haraka Mh. Rais Trump na mke wake. Mungu awafunike kwa ulinzi wake ulio mkuu mno, kama alivyowahi kumfunika Mh. Borris Johnson alipokuwa amepatwa na janga hili

MUNGU AWALINDE NA KUWABARIKI, WAPONE HARAKA
 
KARMA is always a BITCH.

 
Propaganda hiyo anakimbia mdahalo huyo ili ajiandae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…