Trump: Historia Moja ya Ubaguzi

hukumundo

JF-Expert Member
Oct 8, 2011
849
435
Watu wengi hapa Bongo wanamshabikia Trump na kuona kwamba madai juu ubaguzi wake ni ya kampeni tu. Kwa wale tunaomjua Trump toka siku nyingi tunadhani kwamba Wabongo wanaomshabikia Trump wanafanya hivyo kwa kufuata hadithi moja tu.

Mwandishi Chimamanda Ngozi Adichie ameandika na kufanya kampeni dhidi ya kuiangalia dunia na mazingira kwa kufuata hadithi moja tu. Nami nawaasa msimwangalie Trump kwa jambo moja tu. Ila hapa nawaletea simulizi za kweli kuhusu ubaguzi wake na mkakati anaoutumia mara nyingi kupata wafuasi.

Mnamo tarehe 19 Aprili 1989, jioni, giza likiwa limeshaingia, Mwanadada mzungu Trisha Meili (28) akiwa ana-jog katika Central Park jijini New York, alivashambuliwa, akabakwa, akapigwa vibaya na mtesi wake akakimbia akiamini amekufa labda.Usiku huo huo mwanamke mwingine mweusi alibakwa na kutupwa kutoka ghorofani sehemu hizo hizo.

Ulikuwa pia usiku wa vurugu karibu na hapo. Vijana hasa weusi na Walatino walikuwa wakirusha mawe na kupiga kelele. Wakakamatwa vijana weusi wanne na mlatino mmoja wakidaiwa kuwa ndiyo waliombaka Bi Meili.

Vijana hao walikuwa na miaka 14-16. Wakiwa rumande walibanwa vibaya na mateso kiasi kwamba kila mmoja akajionea kwamba akikiri kwamba aliwaona wenzie, atasalimika. Kwa njia hiyo wakajikuta wote wamekiri kuhusika kwa namna fulani.

Wiki mbili baada ya tukio hilo, na baada ya habari za kukiri kwao kujulikana, Trump alinunua ukurasa mmoja wa gazeti maarufu la New York Daily News na kuanza kampeni za kudai hukumu ya kifo kwa vijana wakatili na washenzi hao.

Mpaka hapo huwezi kuona dalili za ubaguzi wake, mpaka nikuambie kwamba halikusemwa jambo lolote kuhusu mwanamke mweusi ambaye aliuawa usiku ule na katika mazingira yale. Trump alitoa maneno makali ambayo yalichochea hali mbaya na vitisho kwa familia za vijana hao. Sitakuwa na muda wa kuelezea jinsi ambavyo mfumo wa kisheria unavyowakandamiza watu wa matabaka fulani huko Marekani.

Mwaka 2002, jambazi na mbakaji sugu Matias Reyes akakiri kwamba ndiye hasa aliyembaka na kumpiga Bi Meili. Baadaye uchunguzi wa DNA ulifanywa na vizibiti vilivyokusanywa wakati ule na ikathibitika kwamba ndiye mbakaji aliyehusika na tukio lile baya. Hakuna hata mmoja katika wale wavulana watano aliyehusika. Na mwishoni mwa mwaka huo vijana wale wote walifunguliwa na kesi yao kufutwa. Waliishtaki serikali ya jiji la New York na mwaka 2014l walishinda $41 milioni kwa kufanya njama za kuwakuta na hatia na kuwafunga kinyume cha sheria na haki.

Kila mtu aliona ni utovu wa haki na unyama waliofanyiwa vijana hao. Watu walioamini kwamba vijana hao ndiyo wakosaji kwa sababu ya uendeshaji mbaya wa shauri hili walikiri kwamba vijana hawakutendewa haki. Na Trump je, ambaye alifanya kampeni akidai vijana hao wanyongwe? Utadhani kwamba kama ni mtu wa kusema ukweli na kufuata ukweli angesema sawa, ushahidi umeonesha hawana kosa.

Tumewakosea. NOOOO! Trump aling’aka akidai vijana wale ndiyo wenye hatia, na wametolewa tu kwa technicality. Alidai kwamba wale vijana watakuwa wanawacheka watu wote wa New York kwani wamebaka na sasa wamelipwa donge nono kwa ubakaji huo.

Na hapo ndipo tunapoona hatari ya uraisi wa Trump, kutopenda kujua na kuutambua ukweli wa mambo. Watu wanadhani “anasema kweli bila kupindisha maneno.” Kwa hakika ni ukweli anavyouona yeye na anaoutaka yeye.

Watu wa namna hii ni hatari sana duniani. Hitler alikuwa anauona ukweli kwa namna yake na hata ilivyokuwa dhahiri kwamba Wajerumani wako matatani, hakuona ukweli huo. Kwa maoni yangu yuko katika Republican Party kwa sababu kwa miaka ya karibuni chama hicho kimejitoa ufahamu na kuukataa ukweli ambao hawaupendi. Tulishuhudia hilo mwaka 2012 wakati watu wote walipokuwa wanaona kwamba Obama anakubalika sana, Romney na wakuu wa Republican Party walianza sherehe kabla ya siku ya uchaguzi wakidai kwamba dalili zote ni za ushindi ilhali polls zote zilikuwa zinasema mambo mengine kabisa.

Hivi sasa, wanasayansi wanazungumzia mabadiliko ya tabianchi, lakini kuna wasomi wengi ndani ya chama hicho wanadai hakuna kitu kama hicho.Wachunguzi kadha wa maisha ya Trump wanasema anajua sana kutumia lugha yenye undertones za ubaguzi wa rangi ili kuhamasisha mgongano baini ya watu.

Ndipo nikasema, Republican Party si walijidai wao ni zaidi katika kuukataa ukweli, basi sasa wamempata mtu ambaye ndiyo mnafiki mkubwa anayeweza kuukataa ukweli kushinda wao. Ashakum si matusi: Republican establishment imejamba sasa wananusa wenyewe, wasishangae.
 
Nadhani tuwaachie wamarekani wenyewe waamue, maana wenzetu wana uwezo mkubwa sana wa kipima na kujua ni nani anafaa kuiongoza Marekani, sio kama sisi huku tunaochagua kwa kuangalia uwezo wa kupiga push-ups jukwaani. Wakiona Trump hafai naamini hawatamchagu.

Tusubiri tuone!!!
 
Siamimi kama wewe/sisi tunaathirika na ubaguzi wake, pili hiyo ni habari kama habari nyingine, yaweza kuwa kweli au si kweli, tatu tukimpenda au kumchukia trump hatutaleta athaari yoyote kwake, nne Trump ndio atapeperusha bebdera ya Republican(mtazamo wangu, neno langu sio sheria)
 
Siamimi kama wewe/sisi tunaathirika na ubaguzi wake, pili hiyo ni habari kama habari nyingine, yaweza kuwa kweli au si kweli, tatu tukimpenda au kumchukia trump hatutaleta athaari yoyote kwake, nne Trump ndio atapeperusha bebdera ya Republican(mtazamo wangu, neno langu sio sheria)
Hoja yangu kubwa katika nyuzi hizi za Trump ni kuwaasa watu kuwa critical zaidi katika kupata habari. Inakupasa kutafuta ukweli na si kushabikia tu. Na unapouona ukweli, uukubali. Na hilo ndilo nililolisema juu ya Trump na Republicans, wanapenda kuukataa ukweli hata ukiwa dhahiri kiasi gani. Ushahidi upo wa kisayansi kwamba vijana hawakufanya hayo mambo, na mtu mwingine kapatikana kwamba ndiyo katenda, na ushahidi wa kisayansi unamwonyesha ndiye, lakini Trump anasema, ni upuuzi. Ni kuukataa ukweli. Habari nilizokupa hapa si za kusema "yaweza kuwa kweli au si kweli." Mambo hayo yalitokea kabisa. Ninakupa links za sources usome wewe mwenyewe ujiridhishe. Ukiukataa ukweli ndipo utang'ang'ania na kudai wanamwonea ilhali mambo yako dhahiri kabisa. Hata kama labda haituhusu Watanzania, usomaji wetu wa habari lazima uwe informed. Kuwa informed inatakiwa kuwa ndiyo desturi yetu, la sivyo hata mambo yetu ya hapa Bongo hatutayachukulia kwa makini na kufanya ushabiki tu.


Donald Trump and the Central Park Five: the racially charged rise of a demagogue


Donald Trump and the Central Park Five - The New Yorker


Central Park jogger case - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Trump kashawasema Africa iz are lazy poor and thief
ImageUploadedByJamiiForums1458508207.357598.jpg
 
Watu wengi hapa Bongo wanamshabikia Trump na kuona kwamba madai juu ubaguzi wake ni ya kampeni tu. Kwa wale tunaomjua Trump toka siku nyingi tunadhani kwamba Wabongo wanaomshabikia Trump wanafanya hivyo kwa kufuata hadithi moja tu. Mwandishi Chimamanda Ngozi Adichie ameandika na kufanya kampeni dhidi ya kuiangalia dunia na mazingira kwa kufuata hadithi moja tu. Nami nawaasa msimwangalie Trump kwa jambo moja tu. Ila hapa nawaletea simulizi za kweli kuhusu ubaguzi wake na mkakati anaoutumia mara nyingi kupata wafuasi.
Mnamo tarehe 19 Aprili 1989, jioni, giza likiwa limeshaingia, Mwanadada mzungu Trisha Meili (28) akiwa ana-jog katika Central Park jijini New York, alivashambuliwa, akabakwa, akapigwa vibaya na mtesi wake akakimbia akiamini amekufa labda.Usiku huo huo mwanamke mwingine mweusi alibakwa na kutupwa kutoka ghorofani sehemu hizo hizo. Ulikuwa pia usiku wa vurugu karibu na hapo. Vijana hasa weusi na Walatino walikuwa wakirusha mawe na kupiga kelele. Wakakamatwa vijana weusi wanne na mlatino mmoja wakidaiwa kuwa ndiyo waliombaka Bi Meili. Vijana hao walikuwa na miaka 14-16. Wakiwa rumande walibanwa vibaya na mateso kiasi kwamba kila mmoja akajionea kwamba akikiri kwamba aliwaona wenzie, atasalimika. Kwa njia hiyo wakajikuta wote wamekiri kuhusika kwa namna fulani.
Wiki mbili baada ya tukio hilo, na baada ya habari za kukiri kwao kujulikana, Trump alinunua ukurasa mmoja wa gazeti maarufu la New York Daily News na kuanza kampeni za kudai hukumu ya kifo kwa vijana wakatili na washenzi hao. Mpaka hapo huwezi kuona dalili za ubaguzi wake, mpaka nikuambie kwamba halikusemwa jambo lolote kuhusu mwanamke mweusi ambaye aliuawa usiku ule na katika mazingira yale. Trump alitoa maneno makali ambayo yalichochea hali mbaya na vitisho kwa familia za vijana hao. Sitakuwa na muda wa kuelezea jinsi ambavyo mfumo wa kisheria unavyowakandamiza watu wa matabaka fulani huko Marekani.

Mwaka 2002, jambazi na mbakaji sugu Matias Reyes akakiri kwamba ndiye hasa aliyembaka na kumpiga Bi Meili. Baadaye uchunguzi wa DNA ulifanywa na vizibiti vilivyokusanywa wakati ule na ikathibitika kwamba ndiye mbakaji aliyehusika na tukio lile baya. Hakuna hata mmoja katika wale wavulana watano aliyehusika. Na mwishoni mwa mwaka huo vijana wale wote walifunguliwa na kesi yao kufutwa. Waliishtaki serikali ya jiji la New York na mwaka 2014l walishinda $41 milioni kwa kufanya njama za kuwakuta na hatia na kuwafunga kinyume cha sheria na haki.

Kila mtu aliona ni utovu wa haki na unyama waliofanyiwa vijana hao. Watu walioamini kwamba vijana hao ndiyo wakosaji kwa sababu ya uendeshaji mbaya wa shauri hili walikiri kwamba vijana hawakutendewa haki. Na Trump je, ambaye alifanya kampeni akidai vijana hao wanyongwe? Utadhani kwamba kama ni mtu wa kusema ukweli na kufuata ukweli angesema sawa, ushahidi umeonesha hawana kosa. Tumewakosea. NOOOO! Trump aling’aka akidai vijana wale ndiyo wenye hatia, na wametolewa tu kwa technicality. Alidai kwamba wale vijana watakuwa wanawacheka watu wote wa New York kwani wamebaka na sasa wamelipwa donge nono kwa ubakaji huo.

Na hapo ndipo tunapoona hatari ya uraisi wa Trump, kutopenda kujua na kuutambua ukweli wa mambo. Watu wanadhani “anasema kweli bila kupindisha maneno.” Kwa hakika ni ukweli anavyouona yeye na anaoutaka yeye. Watu wa namna hii ni hatari sana duniani. Hitler alikuwa anauona ukweli kwa namna yake na hata ilivyokuwa dhahiri kwamba Wajerumani wako matatani, hakuona ukweli huo. Kwa maoni yangu yuko katika Republican Party kwa sababu kwa miaka ya karibuni chama hicho kimejitoa ufahamu na kuukataa ukweli ambao hawaupendi. Tulishuhudia hilo mwaka 2012 wakati watu wote walipokuwa wanaona kwamba Obama anakubalika sana, Romney na wakuu wa Republican Party walianza sherehe kabla ya siku ya uchaguzi wakidai kwamba dalili zote ni za ushindi ilhali polls zote zilikuwa zinasema mambo mengine kabisa. Hivi sasa, wanasayansi wanazungumzia mabadiliko ya tabianchi, lakini kuna wasomi wengi ndani ya chama hicho wanadai hakuna kitu kama hicho.Wachunguzi kadha wa maisha ya Trump wanasema anajua sana kutumia lugha yenye undertones za ubaguzi wa rangi ili kuhamasisha mgongano baini ya watu.

Ndipo nikasema, Republican Party si walijidai wao ni zaidi katika kuukataa ukweli, basi sasa wamempata mtu ambaye ndiyo mnafiki mkubwa anayeweza kuukataa ukweli kushinda wao. Ashakum si matusi: Republican establishment imejamba sasa wananusa wenyewe, wasishangae.

1. Hakuna hats sehemu Mona inayoonyesha alitenda hivyo kwa sababu vijana wale ni weusi.

2. Zungumzia tabia za baadhi ya wamarekani weusi yuko US.
 
1. Hakuna hats sehemu Mona inayoonyesha alitenda hivyo kwa sababu vijana wale ni weusi.

2. Zungumzia tabia za baadhi ya wamarekani weusi yuko US.
In fact, sidhani hata kama aliwataja wale vijana watano, if you must know. Lakini siku zote unaposoma habari yoyote soma na subtext. Kuna mambo huwezi kuyasema kwa sababu kisheria unaweza kujikuta matatani. Lakini the subtext may be very clear. Na hasa unapoona 2014 anawaona hao vijana kwamba wana hatia.
Juu ya Wamarekani Weusi, wataka niseme nini? Tabia gani wataka niizungumzie? Ni topic pana mno. Na hawapo monolithic. Wako wa namna tofauti tofauti, na mitazamo tofauti tofauti. Kwa mfano, wako wanaomuunga mkono Obama na kumwona ni pragmatic na wako wanaomlaani sana na kumwona ameshindwa kazi. They are just as diverse.
 
Nadhani tuwaachie wamarekani wenyewe waamue, maana wenzetu wana uwezo mkubwa sana wa kipima na kujua ni nani anafaa kuiongoza Marekani, sio kama sisi huku tunaochagua kwa kuangalia uwezo wa kupiga push-ups jukwaani. Wakiona Trump hafai naamini hawatamchagu.

Tusubiri tuone!!!


Really? Unaamini kuwa Wamarekani wana uwezo mkubwa wa kujua viongozi wazuri? Hawa ni watu waliomchagua George W Bush twice!!
 
Inakuwa ngumu kuziamini habari kama hizi kwa kipindi kama hiki. Ambacho trump anamaadui wengi sana ndani ya chama chake na. Nje ya
Chama chake. Yatasemwa mengi sana. ila mm ninamtakia trump aishi maisha marefu.
Kwasababu.
 
Inakuwa ngumu kuziamini habari kama hizi kwa kipindi kama hiki. Ambacho trump anamaadui wengi sana ndani ya chama chake na. Nje ya
Chama chake. Yatasemwa mengi sana. ila mm ninamtakia trump aishi maisha marefu.
Kwasababu.
Na hicho ndicho ninachokisema juu ya hatari ya kutokuwa makini na kutokuwa critical. Wakiamua watu kushabikia basi hata uwape ushahidi kwamba si hivyo, wanasema "inakuwa ngumu kuziamini habari hizi kwa kipindi kama hiki." Hii ni tabia iliyosambaa ya kukataa ushahidi na kurukia mambo yasiyo na ushahidi wa kutosha. Ndiyo maana kila kona ukienda unaambiwa vitu kama Freemason hata kama hakuna ushahidi wowote.
Nasema ni lazima tujifunze kuwa critical na kuchunguza habari kwa makini si kishabiki tu. Hiyo habari nimeileta na nimeweka links. Na utaona kwenye links hizo habari hizi si mpya. Unaitilia mashaka kwa misingi gani?
 
Na hicho ndicho ninachokisema juu ya hatari ya kutokuwa makini na kutokuwa critical. Wakiamua watu kushabikia basi hata uwape ushahidi kwamba si hivyo, wanasema "inakuwa ngumu kuziamini habari hizi kwa kipindi kama hiki." Hii ni tabia iliyosambaa ya kukataa ushahidi na kurukia mambo yasiyo na ushahidi wa kutosha. Ndiyo maana kila kona ukienda unaambiwa vitu kama Freemason hata kama hakuna ushahidi wowote.
Nasema ni lazima tujifunze kuwa critical na kuchunguza habari kwa makini si kishabiki tu. Hiyo habari nimeileta na nimeweka links. Na utaona kwenue links hizo habari hizi si mpya. Unaitilia mashaka kwa misingi gani?
Hata wewe mwemyewe ukiingia kwenye siasa lazima yatajitokeza maneno kama hayo lakini yeye trump amesema siasa hataki kwasababu siku zote siasa ndio zinazo leta matatizo.
 
Hata wewe mwemyewe ukiingia kwenye siasa lazima yatajitokeza maneno kama hayo lakini yeye trump amesema siasa hataki kwasababu siku zote siasa ndio zinazo leta matatizo.
Ninachosema ni kwamba ukweli uko wazi. Kama tu ni mahaba niue sawa. Lakini ni tabia hii ya kutotaka kuyatafakari mambo kwa makini na kuchukulia kiushabiki tu ndiko kunakotuponza hata kwenye siasa zetu na maisha yetu pia. Tu wepesi wa kuamini stori za vijiweni na hatutaki kuhakiki ukweli wake. Na mtazamo wako ni evidence.
 
  • Thanks
Reactions: kui
Hapo hujaweka maneno yake machafu anayoo ngea kuhusu wanawake.

Juzi tena kapishana maneno na Fox News wakamtolea uvivu. (A Republican VS Fox news)?!!

Kuna mvurugano sasa Republicans (they don't know what to do with him)
Kama ni kuungana na kum support, watafanya hivyo kwa ajili ya kukiokoa Chama chao. Ni mbaya kiasi kwamba kuna rumors za kuanzisha third party, kitu ambacho kitasambaratisha The Grand Old Party.
 
Mike Tyson says it’s ‘a pretty awesome thing’ that Donald Trump is ‘doing so well’

imrs.php

Donald Trump is shown with Mike Tyson in 1988. (Richard Drew/Associated Press)

Donald Trump certainly has his share of detractors, but Mike Tyson is not one of them. The ex-boxer, who has previously expressed support for the Republican presidential candidate, recently said that Trump has gotten an idea of what Tyson himself once went through, and that “it’s a pretty awesome thing” that Trump is “doing so well.”
Mike Tyson says it’s ‘a pretty awesome thing’ that Donald Trump is ‘doing so well’
 

Attachments

  • upload_2016-3-22_5-36-0.jpeg
    upload_2016-3-22_5-36-0.jpeg
    4.8 KB · Views: 74
  • upload_2016-3-22_5-36-23.jpeg
    upload_2016-3-22_5-36-23.jpeg
    3.2 KB · Views: 74
Back
Top Bottom