Watu wengi hapa Bongo wanamshabikia Trump na kuona kwamba madai juu ubaguzi wake ni ya kampeni tu. Kwa wale tunaomjua Trump toka siku nyingi tunadhani kwamba Wabongo wanaomshabikia Trump wanafanya hivyo kwa kufuata hadithi moja tu.
Mwandishi Chimamanda Ngozi Adichie ameandika na kufanya kampeni dhidi ya kuiangalia dunia na mazingira kwa kufuata hadithi moja tu. Nami nawaasa msimwangalie Trump kwa jambo moja tu. Ila hapa nawaletea simulizi za kweli kuhusu ubaguzi wake na mkakati anaoutumia mara nyingi kupata wafuasi.
Mnamo tarehe 19 Aprili 1989, jioni, giza likiwa limeshaingia, Mwanadada mzungu Trisha Meili (28) akiwa ana-jog katika Central Park jijini New York, alivashambuliwa, akabakwa, akapigwa vibaya na mtesi wake akakimbia akiamini amekufa labda.Usiku huo huo mwanamke mwingine mweusi alibakwa na kutupwa kutoka ghorofani sehemu hizo hizo.
Ulikuwa pia usiku wa vurugu karibu na hapo. Vijana hasa weusi na Walatino walikuwa wakirusha mawe na kupiga kelele. Wakakamatwa vijana weusi wanne na mlatino mmoja wakidaiwa kuwa ndiyo waliombaka Bi Meili.
Vijana hao walikuwa na miaka 14-16. Wakiwa rumande walibanwa vibaya na mateso kiasi kwamba kila mmoja akajionea kwamba akikiri kwamba aliwaona wenzie, atasalimika. Kwa njia hiyo wakajikuta wote wamekiri kuhusika kwa namna fulani.
Wiki mbili baada ya tukio hilo, na baada ya habari za kukiri kwao kujulikana, Trump alinunua ukurasa mmoja wa gazeti maarufu la New York Daily News na kuanza kampeni za kudai hukumu ya kifo kwa vijana wakatili na washenzi hao.
Mpaka hapo huwezi kuona dalili za ubaguzi wake, mpaka nikuambie kwamba halikusemwa jambo lolote kuhusu mwanamke mweusi ambaye aliuawa usiku ule na katika mazingira yale. Trump alitoa maneno makali ambayo yalichochea hali mbaya na vitisho kwa familia za vijana hao. Sitakuwa na muda wa kuelezea jinsi ambavyo mfumo wa kisheria unavyowakandamiza watu wa matabaka fulani huko Marekani.
Mwaka 2002, jambazi na mbakaji sugu Matias Reyes akakiri kwamba ndiye hasa aliyembaka na kumpiga Bi Meili. Baadaye uchunguzi wa DNA ulifanywa na vizibiti vilivyokusanywa wakati ule na ikathibitika kwamba ndiye mbakaji aliyehusika na tukio lile baya. Hakuna hata mmoja katika wale wavulana watano aliyehusika. Na mwishoni mwa mwaka huo vijana wale wote walifunguliwa na kesi yao kufutwa. Waliishtaki serikali ya jiji la New York na mwaka 2014l walishinda $41 milioni kwa kufanya njama za kuwakuta na hatia na kuwafunga kinyume cha sheria na haki.
Kila mtu aliona ni utovu wa haki na unyama waliofanyiwa vijana hao. Watu walioamini kwamba vijana hao ndiyo wakosaji kwa sababu ya uendeshaji mbaya wa shauri hili walikiri kwamba vijana hawakutendewa haki. Na Trump je, ambaye alifanya kampeni akidai vijana hao wanyongwe? Utadhani kwamba kama ni mtu wa kusema ukweli na kufuata ukweli angesema sawa, ushahidi umeonesha hawana kosa.
Tumewakosea. NOOOO! Trump aling’aka akidai vijana wale ndiyo wenye hatia, na wametolewa tu kwa technicality. Alidai kwamba wale vijana watakuwa wanawacheka watu wote wa New York kwani wamebaka na sasa wamelipwa donge nono kwa ubakaji huo.
Na hapo ndipo tunapoona hatari ya uraisi wa Trump, kutopenda kujua na kuutambua ukweli wa mambo. Watu wanadhani “anasema kweli bila kupindisha maneno.” Kwa hakika ni ukweli anavyouona yeye na anaoutaka yeye.
Watu wa namna hii ni hatari sana duniani. Hitler alikuwa anauona ukweli kwa namna yake na hata ilivyokuwa dhahiri kwamba Wajerumani wako matatani, hakuona ukweli huo. Kwa maoni yangu yuko katika Republican Party kwa sababu kwa miaka ya karibuni chama hicho kimejitoa ufahamu na kuukataa ukweli ambao hawaupendi. Tulishuhudia hilo mwaka 2012 wakati watu wote walipokuwa wanaona kwamba Obama anakubalika sana, Romney na wakuu wa Republican Party walianza sherehe kabla ya siku ya uchaguzi wakidai kwamba dalili zote ni za ushindi ilhali polls zote zilikuwa zinasema mambo mengine kabisa.
Hivi sasa, wanasayansi wanazungumzia mabadiliko ya tabianchi, lakini kuna wasomi wengi ndani ya chama hicho wanadai hakuna kitu kama hicho.Wachunguzi kadha wa maisha ya Trump wanasema anajua sana kutumia lugha yenye undertones za ubaguzi wa rangi ili kuhamasisha mgongano baini ya watu.
Ndipo nikasema, Republican Party si walijidai wao ni zaidi katika kuukataa ukweli, basi sasa wamempata mtu ambaye ndiyo mnafiki mkubwa anayeweza kuukataa ukweli kushinda wao. Ashakum si matusi: Republican establishment imejamba sasa wananusa wenyewe, wasishangae.