Trump hakuitaja Tanzania kuwa ni miongoni mwa Nchi zitakazoongezwa kwenye travel ban

Shigganza

Senior Member
May 24, 2018
160
412
Nimeona vijana wengi hasa wa Upinzani kwa maksudi kutokana na Chuki binafsi, ushabiki wa vyama na ufahamu hafifu wanapotosha kwambaTRUMP ameitaja rasmi Tanzania miongoni mwa Nchi saba zitakazo wekewa vikwazo kwa Raia wake kuingia Nchini humo.

Usahihi wa habari:
Rais wa Marekani DONALD TRUMP akiwa katika Kongamano la Kiuchumi huko Davos Switerland alifanya mahojiano na gazeti la Wall Street, ambapo pamoja na mambo mengine alidokeza Nchi hiyo inatarajia kuongeza Nchi saba (MAJINA HAKUZITAJA) ambazo Raia wake watawekewa vikwazo vya kuingia Nchini humo.

Kufuatia habari hiyo tovuti ya Marekani ya Politico inayojihusisha na masuala ya Sera za Ndani na Nje ya Marekani INADHANI Nchi hizo zinaweza kuwa ni Nigeria, Sudani, Beralus, Mynmar, Tanzania, Kyrgyztan na Eriteria.

Sababu gani husababisha Nchi husika kuingizwa kwenye zuio hilo?
Hapa napo nimeona wanaharakati wanapuyanga, mara Serikali ina vunja haki za binadamu ndio sababu! Ukweli ni kwamba Miongoni mwa Sababu Kuu ambazo zimekuwa zikitumiwa na Marekani kwa Nchi fulani kuingizwa katika orodha ya travel ban ni Nchi husika kuwa na rekodi za kuwa na raia/ vikundi vya kigaidi pamoja na Serikali ya Nchi husika kutoshirikiana na Marekani kwenye kuzuia ugaidi (rejea mifano ya Nchi ambazo tayari zipo kwenye zuio)

Us Travel ban ina maanisha nini?
Ni vikwazo vya kuingia Marekani ambavyo hutolewa kwa Raia wa Taifa fulani lililoko kwenye orodha. Vikwazo hivyo hujumuisha pamoja na mambo mengne nyongeza ya ukaguzi wa taarifa binafsi za waombaji wà visa, ambao hubainika kuwa na rekodi za kujihusisha au kuhusishwa na matukio ya kihalifu huzuiliwa kuingia.

Rai kwa vyombo vya habari
Ni vyema Vyombo vya habari vikaripoti taarifa husika kwa usahihi ili kuondoa taharuki isiyokuwa ya lazima inayoweza kutokea. Aidha tuendelee kusubiri Taarifa Rasmi ya Marekani itakayoonesha orodha ya Nchi hizo.

Aidan Meziwa
Diaspora - US.
 
Screenshot_20200122-231833.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uchambuzi wa BBC juu ya maana ya katazo

Katazo linalotarajiwa kutangazwa Jumatatu tarehe 27 January 2020

Habari juu ya katazo litakalohusu nchi kadhaa ikiwemo Tanzania zilizozagaa ktk miji yenye habari za uhakika kama Davos Uswiss, Washington DC na magazeti yenye heshima kwa majina Politico, New York Times,The Economist na Wall Street Journal

 
Viherehere walioitaja Tanzania ilhali Trump mwenyewe hajaitaja, aibu kwenu, mijitu mumekosa uzalendo, hamfai kupewa hifadhi kwenye nchi yoyote Afrika, nyie ni vibaraka mtalegea tu.
Magufuli endelea baba, pambana na mafisadi, endelea kuwekeza kwenye miundo mbinu, Afrika itakukumbuka.
 
Back
Top Bottom