Trump awaonya Iran wasicheze na Moto

Uchumi wa Texas ni zaidi ya uchumi wa Ufaransa miongoni mwa mataifa yenye nguvu kubwa za kiuchumi duniani. Sasa huyo Irani na US wapi na wapi? Sana sana janja yake ni kufadhili vikundi vya kigaidi kufanya hujuma; na Trump kawapiga ban imewauma hapana mchezo.
Sio uchumi pekee unaopigana vita. Hata uchumi wa Vietnam ulikuwa mdogo sana, lakini USA walikubali kichapo, tena hadharani. Hata huko Afghanistan na Irak kumewashinda.
 
Wamarekani wanazionea nchi za kiarabu. Koroa ya kaskazini mbona inatesti siraha mbona haichukui hatua....?
 
Trump awambia Iran wanacheza na moto, na yeye hatakuwa mwema sana kama alivyokuwa Obama.
View attachment 466802

Iran kupitia waziri wa ulinzi Javaz Zarif yajibu, Pasipo kuendeshwa na Vitisho vya Mmarekani haiwezi kuanzisha vita.

View attachment 466805

Sasa sijui kwanini Trump inamuuma hawa jama wakifanya kile yeye anachokifanya

UPDATE
Just an update, Marekani muda mfupi uliopita wameongeza vikwazo zidi ya Iran. Hivi vimetarget baadhi ya watu kwenye uongozi wa Iran, lakini bado haijajulikana how far America is ready to go. Maana inavyosemekana vikwazo hivyo vinavyunja makubaliano ya UN ya nuclear kati ya Obama (Marekani na Iran.

Treasury Dept. hits Iran with new sanctions for testing ballistic missile

Iran
wanamjaribu Trump... Trump kawapa onyo, anacheza na FIRE..!! Trump hajaribiwagi..Ooh
 
US asipomnyamazisha Iran asahau kuhusu ushawishi middle East kijeshi na kisiasa. Sasa hivi Iran anatengeneza ushawishi Syria, Lebanon na Iraq pia. Lakini kwa mtazamo wangu ni sawa tu kujenga undugu na majirani. Iran hana kosa hapo. Lakini US anajua huyu mpersia haitaishia hapo.....anajua Iran atataka kutawala middle East kiuchumi na kisiasa. Israel anawasisiwasi. Anataka ajilinde kwa kumuhujumu Iran. Na anayosababu nzito kufanya hivi. Hapo mambo moto. Iran anamambo mawili kuchaguwa. Kujiaandaa na vita au kulegeza msimamo. Najua Iran atachagua bora kuingia vitani si kufa kikondoo. Hawa Wairan wana-historia ndefu katika taifa lao. Wamamisimamo yao na utu wao. Wataingia vitani. Ni suala la muda tu.

Nani atashinda vita?? Wamarekani na Israel watashinda kwa hakika. Lakini hii haitaishia hapo. Makundi mapya ya kigaidi yataibuka. Mbinu mpya kukabiliana nazo zitawekwa.
Mkuu ilani hawezi pigana vita na USA alafu urusi akae tu haiwezekani,kwanza itakuwa advantage kwa Murusi ili urudi kwenye usupa power...kwa maneno mengine USA hawezi pigana na Irani,ingekuwa rahisi hivyo irani ingekuwa tayari majivu
 
Putin atagombana na Trump siku si nyingi mana Trump kumbe ujinga wake ni mwingi sana akitaka kuipiga Iran naamini itazusha mambo makubwa sana sawa atashinda lakini je Mrusi ataacha hiv hivi???
 
Mkuu ilani hawezi pigana vita na USA alafu urusi akae tu haiwezekani,kwanza itakuwa advantage kwa Murusi ili urudi kwenye usupa power...kwa maneno mengine USA hawezi pigana na Irani,ingekuwa rahisi hivyo irani ingekuwa tayari majivu
Vita inawezekana tu. Kifupi hadi sasa Israel ipo kwenye war na Iran. Mipango hii niyasiku nyingi. Subi uone vile Mambo yanaenda
 
So Trump amegwaya kuanzisha vita kaishia kuweka vikwazo uchwara kwa vikampuni vya wairan,
hajui kuwa jamaa wamehitimu katika kuanzisha kampuni hewa kwa ajili ya kuruka viunzi vikwazo.

Kawaida iran sera yake ni kutokua nchi ya kwanza kuanzisha vita,ndo maana haijawahi anzisha vita kwa miaka mingi sana,
majaribio ya makombora yataendelea tena mwezi ujao wanarusha satelite 2
 
Uchumi na vita vinaweza visishabiane sana,, maana kama Iran ana Nuclear weapons,, then hakuna janja ya mmarekani kuretaliate.
Haya zombi ongezea na hii, Uchumi wa Iringa ni zaidi ya uchumi wa Poland.
Teheheheheheheheh......
 
Trump awambia Iran wanacheza na moto, na yeye hatakuwa mwema sana kama alivyokuwa Obama.
View attachment 466802

Iran kupitia waziri wa ulinzi Javaz Zarif yajibu, Pasipo kuendeshwa na Vitisho vya Mmarekani haiwezi kuanzisha vita.

View attachment 466805

Sasa sijui kwanini Trump inamuuma hawa jama wakifanya kile yeye anachokifanya

UPDATE
Just an update, Marekani muda mfupi uliopita wameongeza vikwazo zidi ya Iran. Hivi vimetarget baadhi ya watu kwenye uongozi wa Iran, lakini bado haijajulikana how far America is ready to go. Maana inavyosemekana vikwazo hivyo vinavyunja makubaliano ya UN ya nuclear kati ya Obama (Marekani na Iran.

Treasury Dept. hits Iran with new sanctions for testing ballistic missile
Iran nikweli anacheza na moto.
Note
Yupo on list ya nchi zakuwa hit muda mrefu. Israel ndio eng yani itakuwa majivu. Usa wanakisasi kikali na hwa jammaa yan full hatar
 
Back
Top Bottom