Trump awaonya Iran wasicheze na Moto

LOSEJMASAI

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
332
856
Trump awambia Iran wanacheza na moto, na yeye hatakuwa mwema sana kama alivyokuwa Obama.
upload_2017-2-3_14-16-55.png


Iran kupitia waziri wa ulinzi Javaz Zarif yajibu, Pasipo kuendeshwa na Vitisho vya Mmarekani haiwezi kuanzisha vita.

upload_2017-2-3_14-19-12.png


Sasa sijui kwanini Trump inamuuma hawa jama wakifanya kile yeye anachokifanya

UPDATE
Just an update, Marekani muda mfupi uliopita wameongeza vikwazo zidi ya Iran. Hivi vimetarget baadhi ya watu kwenye uongozi wa Iran, lakini bado haijajulikana how far America is ready to go. Maana inavyosemekana vikwazo hivyo vinavyunja makubaliano ya UN ya nuclear kati ya Obama (Marekani na Iran.

Treasury Dept. hits Iran with new sanctions for testing ballistic missile
 
"We'll never initiate war" hii kauli ya woga sana na Israel itavimba kichwa sana hapo mashariki ya Kati.....hebu tungoje
Mbwa koko kachomeka mkia katikati ya miguu yake ya nyuma; chezea kumwona simba mbele wewe; lazima akimbie upande upande kama amekata "cetre-bolt". Huyo waziri ni wa kufukuza mara moja; kaitia aibu nchi hata kama alichoongea ni ukweli.
 
Iran bado ni taifa dogo sana kijeshi.Jimbo la Texas peke yake linatosha kuipiga Iran
Uchumi wa Texas ni zaidi ya uchumi wa Ufaransa miongoni mwa mataifa yenye nguvu kubwa za kiuchumi duniani. Sasa huyo Irani na US wapi na wapi? Sana sana janja yake ni kufadhili vikundi vya kigaidi kufanya hujuma; na Trump kawapiga ban imewauma hapana mchezo.
 
Uchumi wa Texas ni zaidi ya uchumi wa Ufaransa miongoni mwa mataifa yenye nguvu kubwa za kiuchumi duniani. Sasa huyo Irani na US wapi na wapi? Sana sana janja yake ni kufadhili vikundi vya kigaidi kufanya hujuma; na Trump kawapiga ban imewauma hapana mchezo.

Uchumi na vita vinaweza visishabiane sana,, maana kama Iran ana Nuclear weapons,, then hakuna janja ya mmarekani kuretaliate.
 
Mimi huwa sipendi mipasho si watwangane tu ajulikane na mkubwa sasa vitisho tu mpaka lini wafanye tu hata pambano la kirafiki
 
US asipomnyamazisha Iran asahau kuhusu ushawishi middle East kijeshi na kisiasa. Sasa hivi Iran anatengeneza ushawishi Syria, Lebanon na Iraq pia. Lakini kwa mtazamo wangu ni sawa tu kujenga undugu na majirani. Iran hana kosa hapo. Lakini US anajua huyu mpersia haitaishia hapo.....anajua Iran atataka kutawala middle East kiuchumi na kisiasa. Israel anawasisiwasi. Anataka ajilinde kwa kumuhujumu Iran. Na anayosababu nzito kufanya hivi. Hapo mambo moto. Iran anamambo mawili kuchaguwa. Kujiaandaa na vita au kulegeza msimamo. Najua Iran atachagua bora kuingia vitani si kufa kikondoo. Hawa Wairan wana-historia ndefu katika taifa lao. Wamamisimamo yao na utu wao. Wataingia vitani. Ni suala la muda tu.

Nani atashinda vita?? Wamarekani na Israel watashinda kwa hakika. Lakini hii haitaishia hapo. Makundi mapya ya kigaidi yataibuka. Mbinu mpya kukabiliana nazo zitawekwa.
 
Naona mapicha picha.tangu kuwepo kwa mataifa ulimwenguni,amani haijawahi kutokea.mimi madhani huyu trump ndo atazalisha makundi kibao ya kigaidi.hata huku afrika hatupo salama sana
 
Back
Top Bottom