True Story

Mungi

JF Gold Member
Joined
Sep 23, 2010
Posts
16,975
Reaction score
9,580
[h=5]Hii nimeinyaka mahali:

Juzi wakati naelekea home nilipita pale Salenda bridge nikaona mfuko umetupwa kando ya barabara,nikasogea nikaangalia ndani nikakuta millioni 5 na vitu vyingine kibao...

Moyo ukanidunda,nikashikwa na woga.Nikaangalia kushoto na kulia nikaona watu hawanioni....nikaokota ule mfuko na kwenda haraka home...

Nilipofika home nikamwaga kila kitu,nikakuta;vitambulisho,kadi za ATM,iPhone na certificates kibao...kwa tamaa niliokuwa nayo nilitaka nitoe sim card ktk iphone lakini nikaacha,roho ikanisuta kuwa mwenye mali hii atanipigia!!!

Ni kweli baada ya muda si mrefu simu iliita ..nikapokea(alikuwa Mwanamke) na kwa maelezo aliyotoa ikawa wazi kuwa zile mali ni za aliyenipigia... Nikamwelezea kule niliko.

Baada ya muda huyo mama akaja kuchukua mzigo wake na kila kitu lakini akanipa zile millioni 5 nichukue...

Nikakataa kiistaarabu...ingawa alinilazimisha na kunisihi sana,nilimwambia,'Malipo ni kwa mungu'....Mwishowe yule mama akachukua namba yangu ya simu akaondoka...

Jana akanipigia simu kuwa yuko nje nyumba yangu...nilipotoka nikakuta amekuja na RANGE ROVER SPORT mpyaaa!! akanipa ufunguo akaniambia ni yangu na kuna nyumba ya kifahari MBEZI ...akanipa briefcase imejaa pesa kwa ajili ya kufungua biashara!!

Daah,kwa furaha nikaingia kwenye ile gari nilitest...ile nawasha tu nikasikia,"Anko...Ankooo,amka chakula tayari!"

''MTOTO WA BRO ANANIAMSHA GETO!!!! Kumbe muda wote nlikuwa naotaaaa bana!!!![/h]
 
Na anko mwenyewe ni Preta! Mungi wataalamu wataalamu wake hawapo tena! Wewe ndio wamekurithisha mikoba nini mkuu? BTW Ilikuwa ndoto tamu kichizi.
 
Last edited by a moderator:
Na anko mwenyewe ni Preta! Mungi wataalamu wataalamu wake hawapo tena! Wewe ndio wamekurithisha mikoba nini mkuu? BTW Ilikuwa ndoto tamu kichizi.

afu inatia hasira kichizi unapogundua ni ndoto
 
Last edited by a moderator:
Umeifanya siku yangu kuwa yenye furaha kwa story yako ya ndoto ya mchana.
 
umenikumbusha siku nilipoibiwa gari nikatamani iwe ndoto na kumbe kweli ilikuwa ndoto!
 
aaah kumbe ndoto je ingekuwa kweli ungerudisha kweli lile fuko kwa usawa huu?swali hili alijibu mzee wa kidonge na wakeze maana maisha yao,mmmmh utata kwa kweliii a
 
Hii kama nimeiona kwa Emmanuel Masanja Mkandamizaji...
 
ndoto bwana me kuna wakati naota naokota hela kila navyotembea, nakuwa na hela nyingii nikishtuka kumbe ndoto
 
Dah,nilishakutamani kinoma nikatamani na mm ningepata hilo zali halafu kumbe ndoto dah hongera mkuu ndoto zako nzuri si wengine mara nyingi huwa tunaota zakukimbizwa tu na watu wakutisha!....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…