True story ya Martha

True story ya Martha

Vituka

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2011
Posts
2,269
Reaction score
1,269
Wakati ninakua na kupata akili, pale kijijini kwetu alikuwepo mama mmoja kichaa, jina lake halisi aliitwa Martha na jina alilojitungia baada ya kuchizika ni 'SHOGA'.

Mama huyo alikuwa mzuri sana jamani, na ukweli ni kwamba alikuwa ana watoto wakubwa tu wakike na wa kiume. Kuna wakati alikuwa anapiga pamba za ukweli hadi tunamsahau ingawa ukichaa wake ulikuwa palepale.Alikuwa hajui kumpiga mtu ila vituko vyake tu viliwaacha watu hoi. Anaweza kutana na wewe halafu kwa upole anakuita pembeni na kukwambia kuwa mama yako kafariki. Kwa waliokuwa wanamfahamu haikuwapa shida ila kwa wageni mh, wengi walilizwa. Nilikuwa nikijiuliza sababu za yule mama kuwa kichaa pasopo kupata jibu. Kila niliyemuuliza hakunipa jibu la kueleweka.

Siku moja bibi yangu akanisimulia sababu ya Martha kuwa kichaa. anasema she was married to a certain man ambae pale kwetu anaheshimika sana na ndiye aliyezaa nae watoto3. Waliishi na mama mkwe wa Martha na walipendana sana. Martha hakuwaji kushuhudia ubaya wa mama wakwe na hata wanawake wenzie walipokuwa wakisimuliana mabaya ya mama wakwe aliwashangaa.

Anasema martha alikuwa mama wa nyumbani tu, na alijishughulisha na upikaji wa pombe za kienyeji akishirikiana na mama mkwe wake. Siku moja mama mkwe akamshauri waende kwa mganga kutafta dawa ili wauze izo pombe zao vizuri, yani kila wakipika basi wauze yote. Martha kwa kumuamini mama mkwe wake akakubali ila hakumshirikisha mumewe na hilo likiwa ni agizo toka kwa huyo mama mkwe.

Walifanikiwa kupata iyo dawa na mganga akawapa maagizo kuwa iyo dawa ifunikwe chini ya kitanda cha Martha na cha mama mkwe. Walipofika nyumbani Martha akafanya kama alivyoambiwaa, ila hakuhakikisha kama mamaa mkwe nae alifanya kama alivyoagizwa. Siku moja Martha alishangaa kumuona muweze akija nyumbani na kuanza kupekua uvungu wa kitanda chao! Hamadi!!akatoka na ile midawa!! martha hakuogopa sana akamwambia mumewe ukweli wote.

Mumewe akamuita mama yake na kumuuliza, ajabu mama alikana na kuruka futi mia!!!Anadai hajui chochote. Martha akamwambia mbona hata wewe mama ulipewa iyo dawa uweke uvunguni mwa kitanda chako?Mama akakana na kusema ili kupata ushahidi basi waende chumbani kwake. Mume wa Martha alipekua ule uvungu na hakukuwa na kitu chochote!!Mwisho wa siku Martha akaonekana kuwa alikuwa na nia ya kumloga mumewe!! martha hakuamini kile alichofanyiwa na mama mkwe wake.

Kama kawaida vikao vya wazee vilikaa kuwasuluhisha, mume akasema hana shida yeye alitaka tu kujua izo dawa za nini na kwamba ameamini alichosema mkewe. Tatizo lilikuwa kwa Martha, yeye alitakaa mama mkwe wake akiri ukweli na amuomba msamaha kwa vile amemsingizia kitu kibaya sana na mbele ya jamii ameonekana sio mke mwema. Mama mkwe aliendelea kushikilia msimamo wake, na akadai hata kitendo cha mwanae (mume wa Martha) kuamini maneno ya Martha ni uthibitisho tosha kuwa hiyo dawa sasa inafanya kazi.

Wazee walishindwa kusuluhisha kwa sababu Martha alikuwa hataki kurudi nyumbani kwake mpaka pale mama mkwe atakapokiri kosa lake na pia ahaame hapo nyumbani akaishi sehemu nyingine.Kesi ikaenda kanisani walipofungia ndoa Martha na mumewe. Alikuwepo Padri mmoja mzungu, very famous aliyeanzisha kanisa eneo hilo (Fr. John). Father alimshauri sana Martha amsamehe mama mkwe na arudi nyumbani kulea familia yake lakini Martha alishikilia msimamo wake ule ule kwamba mamaa mkwe ahame na aombe msamaha lasivyo yeye harudi kwa mumewe.

Padri huyo aliendesha vikao vya usuluhishi zaidi ya mara tano kumsihi Martha ila Martha alikataa. Mwisho padri akachukua Bible, akaweka kichwani mwa Martha akamwambia kama wewe ni Mkristo na mtoto wa Mungu samehe na urudi kwako. Martha aliendelea na msimamo wake huo huo na Padri akasema basi yeye hana kingine cha kufanya. Kila mtu akaondoka, na siku hiyo hiyo Martha ALICHIZIKA!

Baada ya kuchizika mumewe alioa tena kwa harusi kanisani (kwa vile kisheria inaruhusiwa) na hadi leo muwe wa Martha yupo hai na huyo mkewe na Martha alishafariki miaka ya 2000 au 2001.
 
mama mkwe....haya, asante kwa simulizi na angalizo kwa wengine
 
Mh! Kwahiyo inatufundisha tusiwaamini wamama wakwe c ndiyo??
 
But sijaelewa huo ukichaa wa martha umetokana na nini?
 
But sijaelewa huo ukichaa wa martha umetokana na nini?

Hata mimi nimepata wakati mgumu kuelewa kama wewe...

Sasa sijajua ni kwa sababu ya masharti ya mganga kukiukwa au ni kutokana na apizo la Biblia...
 
Huyu mume alioa lakini mkewe alikuwa hai hajafa,na ninavyojua kwa wakristo huwezi kuoa mpaka mwenzio afariki dunia.

Kweli hakuna mama mkwe mzuri.
Labda ni 10 kati ya 100
 
Hata mimi nimepata wakati mgumu kuelewa kama wewe...

Sasa sijajua ni kwa sababu ya masharti ya mganga kukiukwa au ni kutokana na apizo la Biblia...

yani nimeshndwaa kabisaa! Mashart y mganga hapana mbona imeonesha hapo kuwa alifanya kama alivyoagizwa,labda bible ya faza kwakuwa aligoma kabsa kutoa msamaha.ila ameonewa mana kumsamehe mtu ni hiari na c lazima!!
 
hadi leo muwe wa Martha yupo hai na huyo mkewe na Martha alishafariki miaka ya 2000 au 2001.

sijaelewa..........huyo mkewe na Martha aliyefariki ni nani.......?
 
WALIMWEUSI tunashukuru kwa hadithi nzuri jamani.

Sasa nafikiri itawafundisha wana wa jukwaa hili wawe makini na mama mkwe zao maana Mi naona ina somo fulani.
 
Last edited by a moderator:
Preta Mi naona aliyekufa kwa hadithi ya WALIMWEUSI ni yule ambaye ameghairi kumsamehe mama mkwe mbele ya Kanisa.

Preta A town wanasemaje?
 
Last edited by a moderator:
Preta Mi naona aliyekufa kwa hadithi ya WALIMWEUSI ni yule ambaye ameghairi kumsamehe mama mkwe mbele ya Kanisa.

Preta A town wanasemaje?

oooh.....asante kwa kunielewesha......japo bado story yenyewe ni tata kwangu.........

A-Town nadhani kutakuwa poa.....nilishahama siku hizi nipo Mongolia........
 
Hata mimi nimepata wakati mgumu kuelewa kama wewe...

Sasa sijajua ni kwa sababu ya masharti ya mganga kukiukwa au ni kutokana na apizo la Biblia...

Ni mchanganyiko wa vyote bila kusahau Msongo wa mawazo baada ya mama mkwe kumgeuka.
 
hadi leo muwe wa Martha yupo hai na huyo mkewe na Martha alishafariki miaka ya 2000 au 2001.

sijaelewa..........huyo mkewe na Martha aliyefariki ni nani.......?
hata mimi hapo mwisho sijaelewa kabisa.
 
Nadhani ilikuwa ni msongo wa mawazo ndio ulisababisha huo ukichaa.
 
Back
Top Bottom