True story: Ushuhuda wa ndoa yangu

True story: Ushuhuda wa ndoa yangu

Kaka, hii story sio ya kutunga, sina sababu ya kumpa Mungu utukufu kwa kitu ambacho hakukifanya kwenye maisha yangu, ujue Mungu hajibembelezi tumtungie sifa na utukufu, na ni dhihaka mbele za Mungu ambayo siwezi kuifanya, Mungu hadhhakiwi wala hahitaji msaada wa wanadamu kupata utukufu, na katu hawezi kuruhusu wala kukubali icho kitu. story hii imenitokea maishani mwangu. vilevile, nawaonya wale ambao hawajaoa au kuolewa, muwe makini sana na zawazi wanazoleta watu, muwe makini na vyakula na kila kitu wakati wa sherehe, muwe makini na ndugu...sio wote wanakuja kwenye ndoa wanawapenda, wengine wanawaonea wivu....kuna mengi huwa yanatokea, niliandika tu harakaharaka nikitoa kichwani yale yaliyotokea, na sijaandika yote, ningeandika yote hapa na kuweka mifano yote, kuna watu hapa wangeshataja hadi jina langu hapa...yapo kadhaa nimeyaacha, nitasimulia siku nyingine, lakini Mungu ni shahidi yangu, haya maisha nimeyapitia kabisa.

Ashukuriwe Mungu atufanyiaye njia pale pasipokua na njia. Mungu hufungua milango iliyofungwa na adui. Yeye ndiye mwenye ufunguo wa Daudi, yeye afunguaye na hapana afungaye. Wao walipokuvuruga walijua wamekuweza, hawakujua Mungu atakukumbuka na kuwaumbua siku moja.
 
wandugu, Mungu anaweza yote. unaweza kupitia janga moja hivi, ukalia hadi machozi ukayazoea, moyo ukaumia hadi mwisho, uso ukawa frustrated hadi mwisho, na kwetu sisi wanaume, unajazwa maneno rundo na ndugu zako, mara umeoa mwenye mkosi, mara umeoa tasa, mara tulikushauri haukusikia, maneno yoote wanaongea, halafu ukiwa umeshazoea umefika mwisho umesema sasa basi kama kudharauliwa nimeshadharauliwa, kama kutukanwa nimeshatukanwa, nimeshajulikana mimi ni mufilisi na tasa....hapohapo Mungu anaituka, anairudisha miaka yote iliyoliwa na nzige madumadu na parare. mimi wakati nafunga ndoa wale tuliofunga pamoja walizaa mwaka unaofuata, wakafululiza kuzaa watoto rundo, lakini mimi nimekuja kujazwa mapacha nimewazidi watoto kwa miaka mifupi tu, wao walienda moja moja mimi dabodabo...hahaaha. Mungu anajua kaibisha adui. however, of all you can do, unatakiwa kusamehe wote waliokukosea na kumwachia Mungu, kisasi ni cha Mungu, na ukifanya hivyo hakika Mungu hujitwalia utukufu. sifa na utukufu kwa Mungu.
 
Ukimtumaini mungu akuangushi nimeona mengi ata mm mwezi mmoja baada yakufunga ndoa tukasema tutafute mtoto aisee mwezi ulio fuata baada yakuona period nilifathaika sana niliumia sana akuna nilicho kiwaza katika akiliyangu zaidi ya mtoto niliwakumbuka watu wote ambao hawana watoto nikasema ili jaribu naona lanipata ntafanya nn
Niliumia yaani naelewa kaka siku moja mume akasema mkewangu ili swala tuache mungu amue ikishindikana tutaasili mtoto mchanga tumlee ila ndugu zangu ntawambia umezaa iliuma mno mno yaani kila wiki napima mimba

Mungu mwema now na mtoto wakike .
Na mama angu anajaribu Ilo mwaka 15 katika ndoa sasa mwaka Jana akapata rehema akapata ujauzito ila mimba kufika miezi sita ikatoka kwa uzembe wa dokta alie Fanya majaribio kwa mwanamke mwenye huitaji wa watoto kwa miaka 15 mama angu akapoteza mapacha 4 na wote walikuwa wakiume
Yaani ilituuma sana tulilia kama msiba wa mtu mzima
Ila atukati tamaa kumwombea mama angu mdogo na yy ni mama mwokovu anae jua mipango ya mungu tuna imani mungu wetu atampa mtoto ata kama mmoja.
So sad habari hii, lakini Bwana wa majeshi hajawahi kushindwa
 
Read Responsibly!!!! mm ilikuwa kidogo tu niingie mkenge nilipokuja kushituka kumbe huwa wanaandaa hata waumin washuhudie uongo kuwahadaa waumin....ila nasema huyu wanayemzushiia atawahukumu kadiri wanavyostahiri
Bado humjui Mungu wa kweli alivyo, ukimjua hutosema hayo. Tena kama kuna watu uliowaona wanaandaa watu ili washuhudie ipo siku Mungu wa kweli atawaaibisha na kuwaweka peupeee maana yeye huwa hadhihakiwi
 
Read Responsibly!!!! mm ilikuwa kidogo tu niingie mkenge nilipokuja kushituka kumbe huwa wanaandaa hata waumin washuhudie uongo kuwahadaa waumin....ila nasema huyu wanayemzushiia atawahukumu kadiri wanavyostahiri
kuna wakati unaweza kung'antwa na nyoka baadaye kila unyasi unaouona unakimbia unahisi ni nyoka, kumbe wakati mwingine sio nyoka, ni kipande cha dhahabu. kuna manabii wa uongo wengi sana siku hizi, wanatafuta pesa tu, na mahubiri yao sio ya utakatifu, ni pesa na miujiza, kupaka mafuta na chochote wanachohisi wanafanya kwa maslahi yao. lakini hapohapo katikati yao wapo watumishi waliitwa na Mungu na wanafanya kazi wakiongozwa na Mungu kabisa. nimezunguka sana makanisa hapo dsm, nimesali makanisa ambayo baadaye nastuka na kukimbia, hiyo yote ni kutafuta mahali sahihi, kwasababu kuna wezi na waongo haimaanishi sasa tubaki tu mahali pasipo salama....tafuta Mungu hadi umwone, ukiona kanisa halieleweki achana nalo nenda lingine, hayo ni mashirika tu ya dini Mungu hatambui dini anaangalia utakatifu hivyo utaenda pale panapokusaidia upata utakatifu. pesa na vitu vingine vyote vitakuja baadaye na havitakiwi kutangulia kuliko kutafuta utakatifu wa Mungu. and as for this testimony, natamani ungekuwa unanifahamu, kwasababu huu ushuhuda nisingeandika mimi, wewe ndio ungeandika badala yangu kwasababu kwa wote wanaonifahamu hakuna asiyeyajua haya niliyoyaandika kwa walau 50% of it. mengine ni ya familia, ila la kufulia, kukosa watoto na yote ambayo hata usipoyatoa nje ya ndoa walioko nje watayajua tu kwa kuwaangalia, yote hayo watu wanayajua. sihitaji kuongea sana hili, Mungu anajua, na sina haja ya kumpa Mungu utukufu kitu ambacho hajafanya. Mungu wa mbinguni atukuzwe milele.
 
ni jambo ambalo limetokea kwenye maisha yangu, ni hakika na kweli. Mungu ndiye shahidi wa kwanza katika hili. nitamshukuru Mungu maisha yangu yote, kwasababu alinikumbuka kipindi cha dhidi yangu. Mungu nakupa utukufu wote, Utukufu wako hatochukua mwanadmau yeyote.

nimewashauri watu wachague makanisa ya kwenda, mimi nilipitia makanis amengi, nilitangatanga sana kutafuta msaada, ajabu yake mambo yalipobadilika, wachungaji kadhaa hasa wa makanisa ambayo niliyastukia nikayakimbia, wakaanza kujitangaza kuwa wao ndio wameniombea mimi na mke wangu hadi tukafunguliwa....wengine wakawa wanataka nikatoe sadaka....sasa wachungaji zaidi ya watatu wote kila mtu anavutia kwake kwamba yeye ndiye aliomba nami...ajabu yake wote hao niliwastukia nikawakimbia. kuna imani nyingi sana siku hizi, wengine wamejificha kwenye makanisa ya kilokole kumbe watafuta pesa tu na wanaiba utukufu wa Mungu. nilienda kuwaambia mimi sitoi sadaka kwasababu wao wamesema, nikakata na mawasiliano yao, niliwaambia siwezi kumpa utukufu mwanadamu wakati Mungu amefanya. kamwe sitaiba utukufu wa Mungu kumpa mwanadamu. ndio maana nawaambia chunguzeni pa kwenda, hasa kwa nyakati hizi.

however, ukweli upo palepale, imani yenye wokovu ni imani ya Kilokole tu, na huko ndiko nilitafuta Mungu nikampata. nilitangatanga mwanzoni, lakini nilipopata kanisa halisi, ndipo hapo nilipata nguvu za Roho Mtakatifu mimi na mke wangu na maisha yakabadilika.
Nimebarikiwa sna na story yko, Hakika hakuna Mungu anaepaswa kuabudiwa ktk roho na kweli zaidi ya Mungu wa bwana wetu Yesu kristo.
Hakika ndugu zangu kama mnataka kuingia mbinguni mpokee huyu Yesu. Atakuweka huru
 
Nimebarikiwa sna na story yko, Hakika hakuna Mungu anaepaswa kuabudiwa ktk roho na kweli zaidi ya Mungu wa bwana wetu Yesu kristo.
Hakika ndugu zangu kama mnataka kuingia mbinguni mpokee huyu Yesu. Atakuweka huru
Ni Mungu wa Ibrahim Isaka na Yakobo mwenye kuhurumia, ndio maana alifanyika mwili afanane na sisi, akazaliwa na kutukomboa toka kwenye maangamizi yote. Uchawi na uganga hauna nguvu dhidi ya Nguvu ya Damu/Jina la Yesu Kristo, alilipa garama yote, alisema yamekwisha, mkuu wa ulimwengu huu ameshashindwa, na kwa Jina lake kila goti litapigwa na kila ulimi utamkiri kuwa yeye ni Bwana, ameinuliwa juu sana, juu kuliko falme zote, hapana Jina lingine tulilopewa sisi wanadamu litupasalo kuokolewa kwalo, kwa Jina hilo kila goti litapigwa la vitu vilivyoko juu mbinguni, vilivyoko duniani na hata chini ya nchi(kuzimu).

laiti kama ningekuwa vizuri kiroho nikawa na Yesu moyoni mwangu, hakika mtego wa mwindaji hata usingeninasa nikateseka na mke wangu kwa miaka 5. wapo watu ambao hawaamini nisemalo, ni kwasababu hayajawakuta, na ninawaombea yasiwakute kabisa, kwasababu ni moto mkali sana.
 
Unashuhudia kwa hamasa mpk mtu anasisimka!
MUNGU WETU NI MWEMA SANA!
 
Unashuhudia kwa hamasa mpk mtu anasisimka!
MUNGU WETU NI MWEMA SANA!
cha ajabu ni kwamba, hayo niliyoongea na mengine ambayo sijayaandika hapa (pangejaa sana) yametokea kwenye maisha yangu halisi kabisa. hadi nikijiangalia leo huw anajishangaa mwenyewe kwasababu usifanye mchezo kupita kwenye kipindi cha miaka 5 mtu mzima umefungwa mikono na miguu, ndoa yako imefungwa mikono, miguu, vizazi everything....Mungu anaweza yote dada. Mwacheni Mungu aitwe Mungu.
 
cha ajabu ni kwamba, hayo niliyoongea na mengine ambayo sijayaandika hapa (pangejaa sana) yametokea kwenye maisha yangu halisi kabisa. hadi nikijiangalia leo huw anajishangaa mwenyewe kwasababu usifanye mchezo kupita kwenye kipindi cha miaka 5 mtu mzima umefungwa mikono na miguu, ndoa yako imefungwa mikono, miguu, vizazi everything....Mungu anaweza yote dada. Mwacheni Mungu aitwe Mungu.
NAKUELEWA!
WALA USISEME ZAIDI!
yani nakuelewaaaaa kabisa kabisa!
 
Back
Top Bottom