True story: Ushuhuda wa ndoa yangu

True story: Ushuhuda wa ndoa yangu

Ukimtumaini mungu akuangushi nimeona mengi ata mm mwezi mmoja baada yakufunga ndoa tukasema tutafute mtoto aisee mwezi ulio fuata baada yakuona period nilifathaika sana niliumia sana akuna nilicho kiwaza katika akiliyangu zaidi ya mtoto niliwakumbuka watu wote ambao hawana watoto nikasema ili jaribu naona lanipata ntafanya nn
Niliumia yaani naelewa kaka siku moja mume akasema mkewangu ili swala tuache mungu amue ikishindikana tutaasili mtoto mchanga tumlee ila ndugu zangu ntawambia umezaa iliuma mno mno yaani kila wiki napima mimba

Mungu mwema now na mtoto wakike .
Na mama angu anajaribu Ilo mwaka 15 katika ndoa sasa mwaka Jana akapata rehema akapata ujauzito ila mimba kufika miezi sita ikatoka kwa uzembe wa dokta alie Fanya majaribio kwa mwanamke mwenye huitaji wa watoto kwa miaka 15 mama angu akapoteza mapacha 4 na wote walikuwa wakiume
Yaani ilituuma sana tulilia kama msiba wa mtu mzima
Ila atukati tamaa kumwombea mama angu mdogo na yy ni mama mwokovu anae jua mipango ya mungu tuna imani mungu wetu atampa mtoto ata kama mmoja.
 
mmmmh nilianza kukuelew ulivyo ingiza mambo ya kanisa tena ukanichosha ata kusoma

by the way pole kwa matatizo hii ndo dunia things change
 
So inspirational and educative spiritual...hakika Mungu ni mwema na ni kweli yote yanaezekana kwa yeye atupaye nguvu na tunaishi kwa neema. Mungu ni mwema maana tushapata ushuhuda au fundosho....mwenye macho na aone mwenye sikio asikie. Ubarikiwe sana mtumishi
 
Mhhhh bado kidogo muanze kunena kwa roho maana naona kila mchangiaji anazidi kupandwa mzuka
 
Ni Miaka mingi kidogo, nawasimulia watakaokuwa wanapitia kadhia ya kutopata watoto katika ndoa, mimi pia yalinikuta, pengine mtajifunza kitu. Kila jambo lina mwisho wake, hakuna jambo lisilo na mwisho. mambo yenye furaha huwa na mwisho pia, mambo yenye huzuni huwa na mwisho pia. Mshukuru Mungu sana kama hujapitia jaribuhili na uwaombee wanaopitia kadhia hii. hii habari ni ya kweli, na inahusu maisha yangu mimi. Nampa Mungu shukrani, sifa na utukufu.

Nilifunga ndoa na mke wangu mpenzi miaka mingi iliyopita, ndoa yetu ilikuwa kubwa na bora...nilikuwa mtu maarufu kidogo, binafsi nilikuwa najiweza kipesa. ndugu wengi waliniganda kwasababu ya pesa tu, hata watu wasio ndugu waliniganda. nilisaidia watu wengi sana, pamoja na kwamba nilikuwa duniani/misri.

Tulipomaliza tu sherehe za ukumbini, ndugu wa pande zote mbili walianza kugombana, kila mtu anataka awe karibu na ndoa yetu zaidi kwa maslahi yake, hatukuwa tunamjua Mungu, tuliishi tu maisha ya kisasa. hatukujua kilichokuwa kinaendelea chini kwa chini kwasababu wote wakifika kwetu hawaonyeshi hiyo na ni wachache wenye ujasiri walitung'ata sikio....tukapuuzia, kumbe ugomvi ule uliendelea hadi kutuchukia mimi na mke wangu.

Tuliishi mwaka wa kwanza, hakuna cha mimba wala dalili, mke wangu magonjwa yalianza mfululizo yasiyoisha, mimi pia biashara na kila nilichokuwa nacho vikaanza kupukutika kimoja baada ya kingine, ndugu wakaanza kudai mtoto wa ndoa, hatukuwa na la kufanya hatujui tutamtoa wapi, na hapohapo tunatamani tungekuwa na uwezo tufanye lolote tupate mtoto ili tusionekana wagumba na matasa. hali ilipoendelea sana, ndugu wangu waliona aibu ya ukoo au familia, watu waliohudhuria ndoa watasema either nimeoa tasa, au mimi mwenyewe sioi, ili kuficha aibu walitaka kulazimisha wamchukue mke wangu wampeleke kijijini kwetu wakamfanyie madawa ya kienyeji, na matambiko, nikagoma. nashukuru Mungu na mke wangu hakukubali. ndugu walinitukana, tuligombana nao waliniona sina akili, na nimekataa msaada wao.wote wakanichukia, tukabaki kama tulivyo, mimi na mke wangu tu. hakuna aliye hata pembeni yetu. tukasonga mbele.

Tulikaa miaka mitatu hakuna mtoto, biashara zote zimesambaratika, viwanja tulivyokuwa navyo prime area tumeuza vyote na hela imepukutikia kwenye matibu, na vitu ambavyo kila tukianzisha vinakufa bila hata kujua vinakufaje. ni kama mkosi uliingia...waliosema mengi walisema, mara wengine wakasema fulani katuloga, wengine wakasema upande huu umetuloga kulipiza kisasi....pamoja na yooote, ni kweli kuna kitu kilifanywa juu yetu katika ulimwengu wa roho ambacho kilitutesa na kutuweka vidonda vilivyotuumiza maumivi ambayo yatakuwa ushuhuda wa maisha yetu hadi siku ya mwisho.

Mhhhh, chakuka kikaanza kuwa cha shida nyumbani kwangu, nilikuwa na maisha mazuri nikafikia kupanga chumba kuishi na mke wa ndoa. tukipanga hapa tunakaa kidogo tunahama ili watu wasijue tunapoishi, wapunguze kusambaza uvumi wa kufilisika na kutozaa...maisha ya shida na hofu, aibu na kudharauliwa hadi na mtoto mdogo. ilifika kipindi hatuna hela ya kula kabisaaa, ndani tupo wawili tu, unakuwa na mia mbili unanunua mihogo ya kukaanga unampa mke aishi, mimi mwanaume najifanya nimeshiba..mia mbili iliyobaki unaiacha ya kesho. tulilala njaa siku nyingi sana na miezi mingi sana, tulikunywa uji kama dinner mara nyingi sana, hatukuijua nyama wala ubwabwa kwa muda mrefu sana, hatuna hela na hakuna hata cha kufanya upate, chochote utakachokifanya hakifaniniwi kabisaa, na yeyote utakayemsogelea hata kibarua kidogo tu, anakukimbia...hapohapo elewa mimi ni graduate wa marks nzuri....lakini hata kibarua hupati.....usifanye mchezo na nuksi....ikikupata hadi nnzi anakukimbia... lakini cha kushukuru Mungu, tulikuwa pamoja ajabu na tulikuwa tunapendana kuliko hata awali.

Mke wangu alifadhaika kupita kiasi, tulikuwa frustrated sana, stress ilikuwa maisha yetu......mwaka wa nne huo hakuna mtoto, magonjwa yamepona, ila hospitali wanasema hatuna shida, mke wangu alikunywa dawa za kila aina za hospitali apate mtoto..tulitembea sana sana, tulienda hospitali za kila aina, na hizo ndizo zilizotufisili sana. Mimi moyoni mwangu nilidhamiria hata tukiishi hivihivi bila mtoto hadi kufa hakuna shida, maadamu tunaishi na mke wangu bila kuachana, nilimpenda sana mke wangu, alinipenda sana pia, nilimkuta mke wangu Bikira, msomi mwenye bikra? ndio inayonifanya nimheshimu sana hadi leo hii.....ni wasomi wachache wenye hiyo.....huwezi kuwaza labda alitumia vidonge au alitoa mimba, yote hayo nilifutilia mbali hayakuwepo kwasababu mimi ndiye nilikata utepe.

wanawake ni wepesi sana kudanganyika....tulikubaliana na mke wangu hatutakwenda kwa waganga wa kienyeji kutafuta mtoto kwasababu kuna mtu tulikuwa tunamjua alipata mtoto kwa mganga wa kienyeji, siku ameingia chumbani akakuta yule mtoto amegeuka nyoka, na ghafla akarudi kuwa mtoto wake........lakini Mke wangu ilifika kipindi alijaribiwa, wakati wa likizo nikamruhusu akaenda kwa wazazi wake mkoa fulani, amerudi na chale nyingi ajabu mbichi, kumbe wazazi wake wameenda kumpeleka kwa waganga wa kienyeji, madawa mengi amekula,..alikiri kwangu yote yaliyotendeka huko kwa uchungu,....tuligombana sana.lakini hakuna kilichobadilika, maisha yalikuwa magumu zaidi. tuligombana sana, ndoa ilikuwa chungu, lakini nilikuja kumsamehe kwasababu niliona sio yeye, alikuwa moja wapo wa wanadamu ambao hata ukiangalia sura tu ni frustrated kabisa, upande wangu mimi ndugu zangu walimsambaratisha na kumsimanga hadi mwisho, nilijua hakuna na nia mbaya, ni kwasababu tu alitaka tupate watoto though kwa njia mbaya ambayo sikuiafiki..nilimuonya asirudie tena na nilimuweka under surveillance.

niligombana na ndugu zangu karibia wote kwaajili ya mke wangu. Wengi walisema nimeoa mtu mwenye mkosi, wengine wakasema nimeoa tasa, kila mtu aliongea lake....ndugu wale wote waliokuwa wanafuata hela walipoona zimeisha waligeuka mabosi wangu wa kunisengenya, kuna watu nimewasaidia hadi kusacrifice vitu vyangu lakini walikuwa ndio wasengenyaji wangu,wanyanyasaji wangu, wamesahau yote. USISAHAU ULIKOTOKA EE MWANADAMU...tujifunze kugeuka nyuma kuangalia waliotufikisha tulipo. watu walikauka nyumbani kwangu, unakaa mwaka mzima hakuna hata anayekupigia simu wala kukusalimia, ukiwatembelea wanajihami wanaona kama unataka kuwakopa hela. nilipita maisha magumu ambayo ni watu wachache sana hupita. tulikuwa tunaumia kuona watu wengine wana watoto wameongozana nao, mke wangu ametukanwa sana na watu kwamba ni tasa, hata mbele za watu, siku moja mtoto wa jirani amevurugavuruga vitu vya mke wangu, alipojaribu kumukanya, mamake alikuja kwa sauti ya uswahilini,....'' WAZAZI TUZAE, WAGUMBE WALEE.."...hahaha, nashukuru Mungu sikurusha ngumi.

tuliamua kwenda kuokoka, Tulimpokea Yesu akawa Mwokozi wa maisha yetu, hakuna jinsi, kwasababu kama maisha ya dunia tumepitia yote, madawa ya kienyeji tumepitia vya kutosha tangu utoto wetu hadi utu uzima....mke wangu alishachanjwa machale ajabu....sasa si bora tuokoke tu tujaribishe na upande mwingine wa shilingi (tulijiuliza)...pale kanisani tukaanza mafunzo ya awali, tulijazwa Roho Mtakatifu, tukawa watu wa kanisani tu, kusali sana, kufunga sana, tulikondaaa sana kwasababu ya kufunga, tulilia machozi hadi ya mwisho....kanisani ilikuwa ni sehemu yetu ya faraja, tukiumia moyo wee tunaenda church tunaliaaa na kumwomba Mungu. Mhhh, Mwaka wa Tano huo, mambo yakaanza kubadilika, tulishasahau kabisa kama tunatafuta mtoto, tunaishi tu kawaida kama watu wengine....kumbe muujiza huja wakati ule umesahau na usiotarajia....Mhhhhh. Mke wangu alikuja kuwa wa kiroho sana, ni mtu wa Maombi sana, sote ilikuwa tunapiga maombi sana, nguvu za Mungu zilianza kujidhihirisha kwetu, hatuna hofu tena, tuna amani na furaha ya Bwana Yesu, furaha na amani isiyopimika.....Asante sana Yesu.....akiwa katika maombi, wife alifunuliwa kama maono mtoto anashushwa amevalishwa nguo nyeupe, ni mtoto anayefanana sana na mimi, Mhhhh, tulimshukuru Mungu na kujitia imani ya Yesu.

tumekaa kidogo, siku nyingine akaona maono wakati wa maombi, watoto wawili wanashushwa na kukabidhiwa mikononi mwake. Oh my God! Mungu anaweza,hakuna jambo lililo gumu kumshinda yeye. mimi Mungu alikuja kunibariki na shirika moja kubwa sana, maisha ya fedha yakabadilika, tukawa watu wenye pesa, waleee waliokuwa wametukimbia waliosema hatuna akili, hatujui kufanya madili, hatujui kuishi mjini, tumefilisika...wakaanza kujikusanya mmoja baada ya mwingine wanakuja kutusalimia....hahahha, kweli Mungu humwondoa mnyonge toka mavumbini, na masikini toka jaani, amkalishe pamoja na wakuu, akakirithi kiti chake cha enzi....nilikuwa ni mtu wa kukaa vikao na watu wakubwa wa dunia hii, nikawa mtu mwenye access ya mambo ya hali ya juu. mke wangu anaanza kujiendeleza zaidi kimasomo, tulikuwa tunaishi kama mapacha....sijui upendo ule ulitoka wapi? Asante Yesu.

imefika kipindi....mke wangu akakosa period, akaanza kuhisi kuumwa, tukaenda hospitali , doctor alitoka pale kwasababu aliona ameongozana na mimi, aliongea kama kukomoa vile".....majibu haya naomba muyapokee kama yalivyo....mkeo ana mimba........"...Ohhh Mungu wangu, niseme nini mimi mwenye dhambi. Doctor alijua labda mimi nina wasiwasi mke wangu kachepuka, sasa nimekuja kuthibitisha kama ana mimba au la ili tugombane vizuri, kumbe tumekuja pale kuthibitisha ile period iliyokosekana ndio majibu ya Mungu au tuendelee kuishi kwa imani kama tulivyozoea, hakujua kama tumetafuta mimba kwa miaka 5, usoni aliongea akidhihirisha kabisa anatarajia tutagombana na alikuwa anajilinda tusianze kugombania pale. hahahaha. Nilimwambia Asante.

Tulishusha pumzi, tukaenda nyumbani, tukamshukuru Mungu. sikuamini, kwasababu nilikuwa kijana na sikuwa nilishazaa au kuexperience icho kitu, ikafika miezi kadhaa, tumbo likawa kubwa, akajifungua mtoto wa kwanza, ni mtoto anayefanana na mimi hadi naogopa. vilevile kama mke wangu alivyoonyeshwa. tulikaa miaka miwili na nusu, tukapata watoto Mapacha wazuri ajabu. sawasawa na vile mke wangu alivyoonyeshwa akishushiwa watoto wawili pamoja alipokuwa kwenye maono. tumeendelea, imekuwa ni kuzaa mapacha tu tena na tena hadi tumefika kipindi tumesema kuzaa sasa basi. hahaha, jamani kila jambo lina mwisho wake, hakuna shida isiyokuwa na mwisho, na hakika watoto ni zawadi toka kwa Mungu, na Mungu hufungua matumbo ya watu wasiozaa, na vizazi visivyozaa.

Neno la Mungu linasema Watoto ni zawadi toka kwa Mungu. Mungu ndiye anatoa watoto, sio waganga wa kienyeji au yeyote yule. na watoto walioletwa na Mungu huwa ni Baraka, hao wanaozaliwa kwa waganga ni uchungu na shida tupu. Asante Yesu.

Zaburi 128:3, yeyote amchaye Bwana, mkewe atakuwa kama mzabibu uzaao nyumbani mwake. Wanawe watachipua kama miche ya mizeituni wakiizunguka meza yake.

Galatia 4:27,
imeandikwa; furahi wewe uliye tasa, usiyezaa, paza sauti ulie, wewe usiye na utungu; maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi kuliko wa huyo aliye na mume.

Walawi 26: 9
, kama tukiyashika maagizo ya Mungu, ataongeza uzao wetu. Tutakuwa na uzazi mwingi, na Mungu atalithibitisha hili agano lake analoliweka nasi kwetu.

Mungu alibadilisha maisha yangu kifedha, Nina furaha, tunacho chakula kingi nyumbani, tumejenga, tuna pesa, tunacho kila tunachohitaji, hakuna majonzi tena, hakuna frustration tena, ukituangalia hautaamini kama tulishakuwa frustrated hadi kutaka kuokota makopo..hahaha watoto wetu wengi wanazunguka meza yetu wakila chakula na kucheza kwa furaha, watoto wamesoma shule bora hapa nchini, wana akili ajabu, ni watoto wa Baraka. Asante sana Mungu wangu kunifuta machozi na kutuondolea aibu ya utasa.

Nikikumbuka nilikotoka Ee Bwana Mungu wa Ibrahimu Isaka na Yakobo, kule ulikonitoa, kwenye aibu kuonekana tasa, umenifuta machozi yangu, umeificha aibu yangu. Asante Mungu wangu.

Kama upo unayepitia kadhia hi, ninaielewa jangwa unalopitia, ni maumivu yasiyopimika. wewe uliyezaa bila tatizo huwezi kuyajua haya ninayoongea, wale walioko kwenye jangwa hilo ndio wanajua maumivu. waombeeni watu wa aina hiyo. Mungu atawabariki. Mlilie Mungu,

Mwombeni Mungu, yeye ndiye atawapatia watoto. fanyeni maombi hata ya kufunga. Mungu atajibu maombi yenu.

Psalms 109:24 24I have gone without eating,b until my knees are weak, and my body is bony. 25When my enemies see me, they say cruel things and shake their heads. 26Please help me, LORD God! Come and save me because of your love. 27 Let others know that you alone have saved me. 28I don't care if they curse me, as long as you bless me. You will make my enemies fail when they attack, and you will make me glad to be your servant. 29You will cover them with shame, just as their bodies are covered with clothes. Magoti yangu yamedhoofu kwa kufunga, na mwili wangu umekonda kw akukosa mafuta, name nalikuwalaumu kwao, wanionapo hutikisa vichwa vyao. Ee Bwana, Mungu wangu, unisaidie, uniokoe sawasawa na fadhili zako, nao wakajue ya kuwa ndio mkono wako, wewe Bwana umeyafanya hayo. Wao walaani basi wewe wabariki, wameondoka wao wakaaibishwa, bali mtumishi wako atafurahi. Washitaki wangu watavikwa fedheha, watajivika aibu yao kama joho.

MWOMBE MUNGU AFANYE KITU ILI WATU WOTE WALIOKUZUNGUKA WAJUE NA KUSEMA NI MUNGU PEKE YAKE AMEFANYA HILI,HAKIKA HUU NI MUUJIZA WA MUNGU NA SI MWINGINE. UKIOMBA MAOMBI YA NAMNA HII,KWA KUFUNGA KWA IMANI YAKO YOTE, UTAFUNGULIWA. VUMILIA, USIKATE TAMAA NA KUGEUKIA NJIA MBAYA.

Only God, can save you, only him and no body else. wanawake ni wepesi wa moyo, msijaribiwe kwenda kwa waganga wa kienyeji, Mkimbilieni Mungu atawaponya. na usiende tu kila kanisa la kilokole, mengine hayana Mungu, tafiti, fanya utafiti uende kanisa gani la wokovu, ukifika hapo tulia mtafute Mungu ataonekana. usihangaikie dunia, tafuta kwanza utakatifu, ukipata utakatifu mambo mengine yote yatakuja kwa ziada. Bali utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na mengine yote mtazidishwa.
Nashukuru kwa ujumbe wako. Nimesoma hadi mwisho.
Ila nina maswali haya
1. Mke wako alikuwa anafanya kazi gani?? Coz Wakati mko nyumba ya kupanga mkiwa bado hamjaokoka umesema mke wako alikwenda likizo kwa wazazi wake na akachanjwa chale huko.
2. Umesema mke wako ni graduate na baada ya wewe kufanikiwa kupata kazi ukaamua akajiendeleze alikwenda kujiendeleza level gani??
3. Kama MKEO alikuwa anafanya kazi na alikuwa anapata mshahara hadi wa kwenda likizo Ilikuwaje muwe hamna hela hadi kushindia uji, mihogo shilling 200 n.k
4. Namwamini sana Mungu naamini sana katika imani yangu. Mungu kanitendea mambo makuu sana maishani mwangu. Naomba majibu ya maswala hayo matatu afu nikwambie kitu
 
Mungu anaweza zaidi ya haya ulioandika hapa mkuu ila punguza drama na simulizi zako.
 
ni jambo ambalo limetokea kwenye maisha yangu, ni hakika na kweli. Mungu ndiye shahidi wa kwanza katika hili. nitamshukuru Mungu maisha yangu yote, kwasababu alinikumbuka kipindi cha dhidi yangu. Mungu nakupa utukufu wote, Utukufu wako hatochukua mwanadmau yeyote.

nimewashauri watu wachague makanisa ya kwenda, mimi nilipitia makanis amengi, nilitangatanga sana kutafuta msaada, ajabu yake mambo yalipobadilika, wachungaji kadhaa hasa wa makanisa ambayo niliyastukia nikayakimbia, wakaanza kujitangaza kuwa wao ndio wameniombea mimi na mke wangu hadi tukafunguliwa....wengine wakawa wanataka nikatoe sadaka....sasa wachungaji zaidi ya watatu wote kila mtu anavutia kwake kwamba yeye ndiye aliomba nami...ajabu yake wote hao niliwastukia nikawakimbia. kuna imani nyingi sana siku hizi, wengine wamejificha kwenye makanisa ya kilokole kumbe watafuta pesa tu na wanaiba utukufu wa Mungu. nilienda kuwaambia mimi sitoi sadaka kwasababu wao wamesema, nikakata na mawasiliano yao, niliwaambia siwezi kumpa utukufu mwanadamu wakati Mungu amefanya. kamwe sitaiba utukufu wa Mungu kumpa mwanadamu. ndio maana nawaambia chunguzeni pa kwenda, hasa kwa nyakati hizi.

however, ukweli upo palepale, imani yenye wokovu ni imani ya Kilokole tu, na huko ndiko nilitafuta Mungu nikampata. nilitangatanga mwanzoni, lakini nilipopata kanisa halisi, ndipo hapo nilipata nguvu za Roho Mtakatifu mimi na mke wangu na maisha yakabadilika.
Mwenyezi MUNGU hayupo kanisani wala kwa mchungaji; bali Mwenyezi MUNGU yupo karibu nawe kuliko mshipa wa shingoni mwako. Ili kumwabudu Mwenyezi MUNGU si lazima kwenda kanisani bali hata chumbani kwako hata msituni hata mtoni. Mche Mwenyezi MUNGU kwa roho na kweli, hakika popote ulipo utamwona. Kikubwa zaidi, tii sheria zake, zidisha mema na ondosha mabaya maishani mwako, Mwenyezi MUNGU atajidhihirisha maishani mwako.
 
kaka wala usisumbuke kufikiri hayo, huyo unayemsema hajawahi kuhubiri haya. sitaki nimseme, ila shuhuda wa hili jambo ni Mungu aliye juu. nimeishi maisha magumu ya kudharauliwa hadi na mtoto mdogo. nuksi ni kitu hatari sana, pamoja na kuwa graduate, niliandika barua za kuomba kazi si chini ya mia moja, na zingine niliitwa interview, lakini ukifika pale, wanakuona kama mavi. ajabu yake, maisha yalipobadilika, everything has changed. Mungu anatakasa ndugu, hauna haja kwenda kuogeshwa kwa mganga, Damu ya Yesu inatosha, inasafisha kabisa mwili nafsi na roho.
Kwanini unasema ni nuksi? Huoni kama unajiingiza kwenye kuhukumu? Kwanini usiamini kuwa yote uliyopitia ulikuwa tu ni mtihani tu maishani mwako?
Kumbuka kupata na kukosa vyote ni mtihani na ni neema. Sasa umepata, hiyo ni neema lkn pia ni mtihani kwako, basi usikufuru.
 
mmmmh nilianza kukuelew ulivyo ingiza mambo ya kanisa tena ukanichosha ata kusoma

by the way pole kwa matatizo hii ndo dunia things change
ndio maana ya ushuhuda, naongea kile kilichotokea kwangu, kama kingetokea kwa mganga wa kienyeji ningesimulia kilivyo, kama kingetokea msikitini ningesimulia kilivyo, kama kingetokea kokote kule, ningesimulia kilivyo....amini usiamini maisha haya nimeyaishi, na ni kwasababu tu yapo mambo nimeyasema kwaajili ya mke wangu kwa ushuhuda wanawake wengine wajifunze, isingekuwa hivyo ningeweka identity yangu hapa, kuna watu humu wangenifahamu na wameshuhudia yaliyotokea maishani mwangu. mwenye kuamini na aamini, asiyeamini basi Mungu amsaidie.
 
Mwenyezi MUNGU hayupo kanisani wala kwa mchungaji; bali Mwenyezi MUNGU yupo karibu nawe kuliko mshipa wa shingoni mwako. Ili kumwabudu Mwenyezi MUNGU si lazima kwenda kanisani bali hata chumbani kwako hata msituni hata mtoni. Mche Mwenyezi MUNGU kwa roho na kweli, hakika popote ulipo utamwona. Kikubwa zaidi, tii sheria zake, zidisha mema na ondosha mabaya maishani mwako, Mwenyezi MUNGU atajidhihirisha maishani mwako.
Natamani nikupe like 10000..

Mleta mada alianza vizuri, lkn alivoanza kuweka sijui Kanisa Fulani ndo nimepata muujiza kanikata stimu, kama promo flani hivi amazing!

God's everywhere...
 
Binafsi nimeliona hilo, ni hadithi tu ya kutunga, ili kulifanyia promo kanisa lake, usikute ni mchungaji kabisa
Kaka, hii story sio ya kutunga, sina sababu ya kumpa Mungu utukufu kwa kitu ambacho hakukifanya kwenye maisha yangu, ujue Mungu hajibembelezi tumtungie sifa na utukufu, na ni dhihaka mbele za Mungu ambayo siwezi kuifanya, Mungu hadhhakiwi wala hahitaji msaada wa wanadamu kupata utukufu, na katu hawezi kuruhusu wala kukubali icho kitu. story hii imenitokea maishani mwangu. vilevile, nawaonya wale ambao hawajaoa au kuolewa, muwe makini sana na zawazi wanazoleta watu, muwe makini na vyakula na kila kitu wakati wa sherehe, muwe makini na ndugu...sio wote wanakuja kwenye ndoa wanawapenda, wengine wanawaonea wivu....kuna mengi huwa yanatokea, niliandika tu harakaharaka nikitoa kichwani yale yaliyotokea, na sijaandika yote, ningeandika yote hapa na kuweka mifano yote, kuna watu hapa wangeshataja hadi jina langu hapa...yapo kadhaa nimeyaacha, nitasimulia siku nyingine, lakini Mungu ni shahidi yangu, haya maisha nimeyapitia kabisa.
 
Back
Top Bottom