True story: Ushuhuda wa ndoa yangu

True story: Ushuhuda wa ndoa yangu

Huu ni uongo mtupu, imani yoyote inayotanguliza tu-miujiza-miujiza kama hiyo ya kwako siyo imani dhabiti na ni imani ya uongo. Ukisoma Mathayo 16:21-26 hata Yesu alikataa mambo ya kujitia ujinga kwamba ukiwa mfuasi wake basi huwezi kupatwa na taabu za hapa duniani. Inaonyesha wazi wewe shida yako ni faraja za kidunia kama watoto, mali n.k ndiyo maana umekuwa ukihama-hama madhehebu/makanisa. Yaani ni kama unamlazimisha Mungu ajibu hayo maombi yako na usipojibiwa unavyotaka imani yako kwa Mungu inapungua/inaisha!! Hii imani yako haina tofauti na wanaofanya ushirikina maana wao utafuta kwa kubadiri waganga mbalimbali mpaka wapate mganga atakayewapatia wanachotaka (mara nyingi mali, watoto au tiba yaani exactly kama yale uliyoyaandika kwenye hadithi yako). Hivyo, Imani ya kweli ni pale utakapo kubali ya kuwa katika hali yoyote ile iwe ya taabu na dhiki (umasikini, ugonjwa, n.k) au faraja (amani, ukwasi, n.k.) Mungu ataendelea kuwa Mungu na watu waambiwe ukweli ya kuwa hapa duniani kuna kupata na kupatwa hata kama ni mfuasi mwaminifu wa Mungu kupitia Yesu. Na siyo hayo majina mnayojibatiza ya ulokole na kuanza kuwadanganya watu eti wakijiunga na imani yenu basi shida zao zitaisha - dhubutu.
binafsi huwa siendi kanisa lolote linalohubiri tu miujiza. ila utakatifu, kujwazwa Roho na kunena kwa lugha, kuishi kwa utakatifu etc. hata Yesu alisema miujiza ni chakula cha watoto ambao hawajamjua yeye. lakini haimaaishi kwamba miujiza haipo, Mungu wetu anafanya miujiza hata leo hii. kuna vitu vingine katika maisha yetu haviwezi kutendeka hadi kwa miujiza, binafsi kwa hali niliyokuwa nayo nilihitaji muujiza wa Mungu kwakweli, na niiliupata and through that imani yangu iliongezeka sana na kilio na majonzi katika ndoa vikakoma. namshukuru Mungu.

kuhusu kuhama kanisa, ndugu yangu, kanisa halimfikishi mtu mbinguni, hayo ni makusanyiko ya watu tu ambo wanampango wa kwenda mbinguni, kusanyiko lingine linaweza kuwa na nia ya kwenda mbinguni lakini wamefuata njia isiyo sahihi, ukigundua sio dhambi kuhama la sivo utakuwa unapoteza muda. Neno la Mungu linasema nanyi mtanitafuta na kuniona mtakaponitafuta kwa mioyo yenu yote. as long as unatumia njia sahihi, tafuta Mungu hadi umpate. ni kweli Mungu ni wa muhimu kuliko muujiza, lakini haimaanishi kwamba muujiza ni dhambi as long as ni Mungu anaufanya. na wakati mwingine huwa ni mpango wa Mungu ajitukuze.
 
Back
Top Bottom