True Story: Nikiwa natafuta kazi nikadondokea mikononi mwa waganga

Kweli maisha si lelemama
Hii Leo Hadi ndoa zinatafutwa kwa waganga,Biashara ili iende lazima umuone Ostazi akusaidie,

Kuna watu wamezikamata familia zao kishirikina yaani akiongea yeye hata kama Mawazo kandamizi ukoo mzima unaafiki
Kiufupi kunawatu wamezishika familia zao kishirikina yaani power ya kifamilia, wanataka waabudiwe kuanzia kazini Hadi mtaani kwa nguvu za Giza walizokuwa nazo
 
Nina mwaka wa nne naenda kwa waganga sasa hivi hapa nina hirizi 23 na chale 50.

Nikipiga hesabu pesa niliyotumia kuzunguka kwa waganga ingetosha kua mtaji kama ningesave ila ndiyo mambo si mambo. Ijumaa naenda kwa mganga wa kimasai nikamsikilize aniambie nakwama wapi.
 
🤣🤣🤣🤣🤣 Pole sana.
 
Hatari hii, sijui nimshukuru nani...Mungu au wazazi! Labda huko mbeleni coz huwezi jua, ila watu wanaishi maisha ya ajabu sana kwa kutegemea mambo ya kichawi na kishirikina.
 
🤣🤣🤣🤣 acha nicheke kwanza.

Lengo la uzi sio kutumia uganga katika kupambana ma maisha bali ni kuwaonyesha madogo na mabro wanaopambana kutoka,mafanikio sio rahisi. Fomula ya mafanikio ni ndefu sana na sio lelemama.

Nilipohitimu chuo kikuu 2011 nikaingia mtaani kutafuta kazi. Hali ilikuwa tait sana maana mpaka hela ya daladala Dar es Salaam ikawa taabu. Sikuwa napenda sana kujiombeleza kwa ndugu,mategemeo yangu makubwa ilikuwa kwa class mates wangu ambao wengi walikuwa wanafunzi wangu.

Nikiwa na ufaulu mzuri wa GPA 4.2 niliamini sistahili kubaki mtaani bali natakiwa kuwa ofisi kali. Sambaza CV kila kona lakini wapi hata interview tu siitwi. Nikaachana na maofisi nikahamia kwenye vyuo vya kati labda wataelewa GPA yangu,lakini wapi.

Jamaa yangu Imma alikuwa msaada sana kwangu,kunitoa nauli na kunifariji. Yeye alipata kazi mapema sana. Kwa sababu alikuwa ni mtu wa karibu sana ikabidi anichane kwamba yeye alienda kwa mganga Bagamoyo akampika.

Imma akanipeleka kwa mganga na kunilipia kila kitu. Nikajikuta Bagamoyo kwa mzee Tupatupa. Sijui kama yupo hai huyu nguli maana ni kitambo sana 2012. Nikamuomba asinichanje maana mimi ni msomi itakuwaje huko mtaani. Basi pale zikapigwa ndumba nyingi. Yule mtaalamu hakuwa na mambo mengi Mwisho nikavua nguo nikajifunga shuka jeupe nikapewa maji kwenye ndoo nikaenda njia panda kuoga. 🤣🤣🤣🤣🤣.

Akaniambia ndani ya mwezi huu nitapata kazi. Kusema kweli nikawa na imani kubwa sana. Katika mwezi huo hali ikawa ngumu tu. Nikaenda kwa baba yangu mdogo vijijini Mtwara kupumzisha akili. Baba mdogo ni mtu wa migodini akanishauri twende kwa mtaalamu. Sikumwambia kama nimeshapikwa tayari.

Basi kule Mtwara nikaenda kwa mtaalam,siyakumbuki vizuri maeneo. Nikakutana na mzee mmoja mlemavu anaganga kwa kutumia koran. Naye pia hakuwa na mambo mengi. Akanifukia vitu vyake na kunipatia hirizi iliyotakiwa kuwa nayo nikienda interview.

Nikaona isiwe taabu nikachagua boxer moja nikaishonelea ile hirizi. Nikaendelea na michakato ya kusaka kazi.

Kufupisha stori baada ya miezi mitatu nikapata ajira safi na mshahara sio haba. Haikuwa rahisi kujua kama waganga walinisaidia au vipi..Haikua rahisi kujua ni mganga yupi aliyenisaidia, ni Tupatupa au mzee wa Mtwara? Sikujua.

Wale wazee wote walinitaka nikifanikiwa nikatoe shukrani. Kusema kweli sikurudi kutoa shukrani zaidi ya kumshukuru Mungu kwa yote.

Sasa imepita miaka 9 nimewakumbuka wale wazee na fighting nzima ya kutafuta ajira. Kama wapo hi nawatakia maisha marefu. Kama walifariki Mungu awarehemu. Ila hirizi ya mzee wa Mtwara ninayo kama kumbukumbu tu huwa nimeiweka kwenye bahasha ngumu na kuifadhi kwenye droo.

Mwisho
Mafanikio hayaji kirahisi. Tufanye kazi na kutafuta mafanikio bila kuchoka bila kukata tamaa. Ikumbukwe sijakuhamasisha uende kwa mganga,nimekuhamisisha upambane
Katoe Shukurani kwa Wazee.

Ni hayo tu
 
acha nicheke kwanza.

Lengo la uzi sio kutumia uganga katika kupambana ma maisha bali ni kuwaonyesha madogo na mabro wanaopambana kutoka,mafanikio sio rahisi. Fomula ya mafanikio ni ndefu sana na sio lelemama.

Nilipohitimu chuo kikuu 2011 nikaingia mtaani kutafuta kazi. Hali ilikuwa tait sana maana mpaka hela ya daladala Dar es Salaam ikawa taabu. Sikuwa napenda sana kujiombeleza kwa ndugu,mategemeo yangu makubwa ilikuwa kwa class mates wangu ambao wengi walikuwa wanafunzi wangu.

Nikiwa na ufaulu mzuri wa GPA 4.2 niliamini sistahili kubaki mtaani bali natakiwa kuwa ofisi kali. Sambaza CV kila kona lakini wapi hata interview tu siitwi. Nikaachana na maofisi nikahamia kwenye vyuo vya kati labda wataelewa GPA yangu,lakini wapi.

Jamaa yangu Imma alikuwa msaada sana kwangu,kunitoa nauli na kunifariji. Yeye alipata kazi mapema sana. Kwa sababu alikuwa ni mtu wa karibu sana ikabidi anichane kwamba yeye alienda kwa mganga Bagamoyo akampika.

Imma akanipeleka kwa mganga na kunilipia kila kitu. Nikajikuta Bagamoyo kwa mzee Tupatupa. Sijui kama yupo hai huyu nguli maana ni kitambo sana 2012. Nikamuomba asinichanje maana mimi ni msomi itakuwaje huko mtaani. Basi pale zikapigwa ndumba nyingi. Yule mtaalamu hakuwa na mambo mengi Mwisho nikavua nguo nikajifunga shuka jeupe nikapewa maji kwenye ndoo nikaenda njia panda kuoga. .

Akaniambia ndani ya mwezi huu nitapata kazi. Kusema kweli nikawa na imani kubwa sana. Katika mwezi huo hali ikawa ngumu tu. Nikaenda kwa baba yangu mdogo vijijini Mtwara kupumzisha akili. Baba mdogo ni mtu wa migodini akanishauri twende kwa mtaalamu. Sikumwambia kama nimeshapikwa tayari.

Basi kule Mtwara nikaenda kwa mtaalam,siyakumbuki vizuri maeneo. Nikakutana na mzee mmoja mlemavu anaganga kwa kutumia koran. Naye pia hakuwa na mambo mengi. Akanifukia vitu vyake na kunipatia hirizi iliyotakiwa kuwa nayo nikienda interview.

Nikaona isiwe taabu nikachagua boxer moja nikaishonelea ile hirizi. Nikaendelea na michakato ya kusaka kazi.

Kufupisha stori baada ya miezi mitatu nikapata ajira safi na mshahara sio haba. Haikuwa rahisi kujua kama waganga walinisaidia au vipi..Haikua rahisi kujua ni mganga yupi aliyenisaidia, ni Tupatupa au mzee wa Mtwara? Sikujua.

Wale wazee wote walinitaka nikifanikiwa nikatoe shukrani. Kusema kweli sikurudi kutoa shukrani zaidi ya kumshukuru Mungu kwa yote.

Sasa imepita miaka 9 nimewakumbuka wale wazee na fighting nzima ya kutafuta ajira. Kama wapo hi nawatakia maisha marefu. Kama walifariki Mungu awarehemu. Ila hirizi ya mzee wa Mtwara ninayo kama kumbukumbu tu huwa nimeiweka kwenye bahasha ngumu na kuifadhi kwenye droo.

Mwisho
Mafanikio hayaji kirahisi. Tufanye kazi na kutafuta mafanikio bila kuchoka bila kukata tamaa. Ikumbukwe sijakuhamasisha uende kwa mganga,nimekuhamisisha upambane
Poa tumekusoma mkuu

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom