True story: Kosa ni la nani?

kibebi

Senior Member
Feb 22, 2013
111
267
sehemu ya 1

“hiyo mimba utailea mwenyewe…mimi sihitaji mtoto kwa sasa na hasa siwezi kuzaa na wewe” yalikuwa ni maneno ya Millard kwa Sarah. Millard na Sara ni waaafrika waliokutana Denmark kila mmoja akiwa nchini humo kwa ajili ya masomo. Millard ni raia wa Siera Leone na Sarah ni raia wa Tanzania. Wawili hawa walikutana kwa mara ya kwanza kwenye treni wakielekea chuoni Upsala kwa ajili ya usaili wa kufungua mhula mpya wa masomo (semester). Kwa Sarah hii ilikuwa ni mara yake ya kwanza kwenda chuoni hapo kwa ajili ya programu yake ya pili baada ya ile ya kwanza ambayo aliichukulia kwenye chuo cha Stockholm nchini Sweden. Akiwa ndani ya treni Sarah alivutiwa kuona mtu anamkazia macho na uso wake umejazwa na tabasamu bashasha na bila hiyana Sarah naye akajibu kwa tabasamu kubwa kabisa na hivyo kumfanya Millard ahame kiti alichokuwa amekalia na kuhamia upande wa pili alipokuwa amekaa Sarah.

“Hello my name is Millard from Siera leone…and you” Ilikuwa ni sauti ya Millard akijitambulisha kwa Sarah mara baada ya kukaa vizuri kwenye kiti kilichoambatana na kiti alichokuwa amekalia Sarah. Sarah akajibu “my name is Sarah from Tanzania… nice to meet you Millard”. Sarah hakuishia hapo aliendelea na mazungumzo na wote walijikuta wamezoeana kama vile walifahamiana miaka 10 iliyopita. “ For how long have you been living here?” aliuliza Sarah akiwa na shauku ya kumfahamu zaidi rafiki huyu ambaye walikutana dakika chache zilizopita. Millard alijibu “Ohhh about 7 years ….infact I relocated from Goteborg to Upsala two years ago”. Kabla Millard hajamaliza Sarah alidakia “I have been living here for two years now but I can not imagine living here for all those years … this place is quite boring. Have you been studying all those years? “Of course yes… what else?” Saraha aliendelea na maswali yake kama vile polisi anavyomhoji mtuhumiwa wa ugaidi.. “do you have a job? Aliuliza Sarah. “Yes I am employed by two companies Milama cleaning company and Sverige cleaning company. I clean shops, and government offices”. alijibu Millard kwa kujiamini. Kwa upande wa Sarah ilikuwa ni kama amepata nafasi ya dhahabu kukutana na mtu ambaye ana uzoefu nchini Sweden angalau kwa muda mrefu na aliwaza huenda Millard atamsaidia kupata kazi jambo ambalo lilikuwa gumu sana kwa wageni. “ I wish it was me…I have been looking for a cleaning job since when I stepped into this country but no where to find one. Can you recommend me to your boss?” aliuliza Sarah kwa sauti iliyoonesha kukata tamaa. “nästa stopp är Upsala” ni sauti iliyokuwa ikiwajulisha kwamba kituo kinachofuata ni Upsala . Hivyo wote walijiandaa na treni iliposimama wote walishuka.

Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Sarah kufika chuoni Upsala hivyo basi Millard alimuongoza Sarah hadi kwenye ofisi ya huduma za wanafunzi ili kupata maelekezo muhimu kuhusiana na programu yake. Baadaye Millard na Sarah walibadilishana namba kwa makubaliano kwamba watatafutana baadaye jioni kwani Millard alikuwa amekuja tu mara moja chuoni hapo na hivyo saa tisa kamili alitakiwa kwenda kusafisha jengo la taasisi ya makosa ya jinai mjini humo.

Baada ya kumaliza taratibu zilizompeleka chuoni Sarah alirudi kwenye hostel za wanafunzi ambapo alipasha mkate wake akaupaka siagi na kasha akajibweteka kwenye kiti akaula taratibu kwa kushushia na chai na rangi. Akiwa katikati mlo wake simu yake ikaita ngriiiii ngriiiiii ngriiii …akabonyeza kitufe cha kupokelea simu. “Hello” Sarah aliitika baada ya kupokea simu ile. “Hello Sarah…this is Millard… how is your evening?” Sarah alistuka kidogo kusikia sauti ya Millard na kukumbuka kuwa alikuwa hajasave ile namba baada ya Millard kumbip wakati alipompatia namba yake. Alichelewa kidogo kujibu na hivyo Millard ilibidi arudie tena kumuuliza kama ni mzima. Sara alimjibu kuwa hakukuwa na tatizo lolote na alikuwa amerudi hostel salama. Waliongea mambo mengi sana usiku ule na Millard alimuahidi Sarah kwamba atamsaidia kupata kazi ya usafi kwenye kampuni ile. Sarah alifurahi sana kusikia kwamba angepatiwa kazi kwenye kampuni mojawapo alizokuwa anafanyia Millard. Muda ulivyozidi kwenda ndipo wawili hawa walizidi kuzoeana na kuwa karibu. Ilifikia kipindi Sarah akawa anamtembelea Millard karibia kila siku muda kwa muda ambao Millard alikuwa amemaliza kazi zake za usafi.

Ilikuwa ni jumapili tulivu iliyokuwa na upepo uliombatana na baridi kali Sarah na Millard walikuwa chumbani kwa Millard wakiangalia movie ya never been kissed. Wote walionekana kuifurahia movie hii na taratibu Millard alijisogeza na kukaa karibu kabisa na Sarah. Wawili hawa walijikuta wamekumbatiana na kujifunika blaketi moja. “ooopssiiiiiii oyeeeahhhh no no no no no pleaseee” Je milio hii ni ya nini na nini kitaendelea?????????ungana nami mtunzi wako kwenye sehemu ya pili ya simulizi hii ya kweli itakayokufunza mikasa na mswaibu ya ughaibuni

Usikose sehemu ya pili ya true story hii jumanne ijay
 
Hahahaha we acha tu, wabeba mabox wanavituko! Ukiwaambia kurudi wanasema wanajipanga, ila Pole zake dada Sarah
Kitu cha kukomunika kwa dinner... halafu mtu yuko Africa anaitisha hela kama vile zinaanguka kwenye mti. Jamani tanzania bado kubwa inatutosha wote na kubaki. Rudini home
 
Kitu cha kukomunika kwa dinner... halafu mtu yuko Africa anaitisha hela kama vile zinaanguka kwenye mti. Jamani tanzania bado kubwa inatutosha wote na kubaki. Rudini home
...a.k.a mkate a.k.a komunio, siipendi kabisa hiyo kitu!
 
Mtunzi au msimuliaji?? Anyways ni nzuri though. Ila wiki hadi wiki mbona interval kubwa sana asee.
 
SEHEMU YA PILI

baada ya movie Milard alimpikia Sarah chakula cha kijapan kijulikanacho kwa jina la lasagne (lasanya). Walikula mlo ule kwa furaha na usiku sarah alilala pale pale ila alijizuia sana milard asimguse. usiku mzima ulikuwa bila bila...

Maisha yaliendela na baada ya miezi miwili Siku moja milard alimua kuongea na sarah kuhusu hisia zake za mapenzi kwa sarah. Sarah hakuonekana kuelewa na hivyo milard hakulazimisha sana. Alimhakikishia sarah kwamba hatajutia kuwa kwenye mahusiano na milard. Walianza kununuliana zawadi mbali mbali na kila mmoja alionekana kufurahia maisha yale. Milard aliongea na boss wake kuhusu swala la rafiki yake kukosa kazi ila boss alimwambia kwa muda ule hakuwa na nafasi yoyote hivyo awe anamkumbusha mara kwa mara ili kama itatokea nafasi aweze kumpatia.

Milard aliamua kumsurprise sarah kwa kumuandalia safari ya boat (cruising) kutoka sweden kwenda Copenhagen. Aliamua kufanya maandalizi kwa kulipia tiketi kupitia mtandaoni na kila kitu kilipokamilika alisubiria siku tatu kabla ya safari ili aweze kumsaprize Sarah. “baby” aliita milard… “ Yes darling” sarah alijibu kwa utii. “I have booked for a boat trip for two of us to Copenhagen, will you join me?” “oohh ofcourse, I have not been to Denmark … thank you milly” alijibu sarah na kumbusu milard kwa furaha. Walimalizia jioni ile kwa kupanga namna ambavyo wangesafiri na namna ambavyo wataifanya safari ile ya kukumbukwa na kila mmoja.

Ngriii ngrriiiii ilikuwa simu ya millard iliyokuwa inaita jioni sana baada ya millard kutoka kazini. Milard aliangalia namba na kugundua aliyekuwa anapiga alikuwa ni boss wake bwana Kristian. Milard alipokea simu ile kwa mashaka sana kwakuwa haikuwa kawaida kwa boss mzungu kumpigia mfanyakazi wake muda ambao sio wa kazi. Baada ya simu ile milard alimuambia sarah kwamba boss anamuomba (sarah) kumsaidia kusafisha duka la chakula asubuhi ya kesho yake kwani anayefanya kazi hiyo anaumwa. Na imebidi ampigie usiku kwani msimamizi wa duka lile huwa hataki masihara kabisa linapokuja swala la usafi dukani pale. Kuna wakati boss wa milard inambidi kusafisha maduka pale anapokosekana mtu wa kushika nafasi inapotokea dharura kwani wateja wao asilimia kubwa ni wakali sana. Na hawaelewi kitu dharura. Ilikuwa ni furaha kubwa kwa sarah kwani kupata kazi ya usafi eneo lile la upsala ilikuwa ni kazi kubwa. Basi sarah na milard walikubaliana walale pamoja ili asubuhi inayofuata waongozane wote ili akamfundishe namna ya kufanya kazi ile kwa ufasaha.

Kesho yake wote waliwahi na kazi ya kufundishana haikuwa ngumu sana. Japo ilikuwa ni siku ya kwanza pale dukani msimamizi wa duka lile alimkubali sana sarah hadi akampigia simu bwana kristian kwa namna alivyofurahia kazi ya msafishaji mpya (sarah). Jioni baada ya kazi sarah na milard walikaa na kujadili kuhusu safari yao ya Denmark. Wote waliafikiana kuwa kwakuwa ilikuwa mara ya kwanza kwa sarah kufanya kazi kwenye kampuni ile isingekuwa vizuri kwa yeye kuomba kuomba ruhusa siku moja tu baada ya yeye kuanza kazi. Hivyo basi waliamua kuvunja safari ile ya Denmark.

Baada ya kupatiwa kazi sarah alionekana kuanza kujenga imani na milard Basi ilifikia kipindi Sarah alihamia kwa milard na wakawa wanalala pamoja, wanapika pamoja na kupakua pamoja. Kwa kweli wawili hawa waliishi kwa furaha sana na kila mmoja alitamani kuwa karibu na mwenzake.
 
Basi maisha yaliendelea na sasa sarah alikuwa anafanya kazi japo ya muda. Ilikuwa ni vigumu sana kuhudhuria masomo kwakuwa wakati mwingine ratiba hasa ya vipindi vya asubuhi iligongana na ratiba ya kazi. Basi ilipotokea kwamba ratiba inagongana sarah hakuwa na namna nyingine zaidi ya kuamua kwenda kazini na kudoji shule.

Sarah kwa imani aliyojenga kwa milard aliamua kukubali ombi la milard. Wawili hawa wakawa wapenzi rasmi. Sarah hakusita kutumia utaalamu wake wa kitanga kumdatisha kijana wa watu. Alimfanyia masaji kila siku jioni, alimuogesha, alimpikia wali nazi, chapati, maandazi, na vyakula vingine vya kitanzania ambavyo sio vya kisieraleon. Kila siku ilikuwa ni ya mshangao kwa milard. Kweli waliridhishana sana hasa kwenye 6/6 na kwa mara ya kwanza kabisa sarah aliweza kufika kileleni. Wanafunzi wengine waliweza kutambua kwamba tayari wawili hawa walikuwa kwenye mahaba mazito.
 
Ni wazi kwamba milard alibadilisha maisha sarah na kumfungulia milango ya ajira kwani baada ya kuonesha ufanisi alizidi kuongezewa kazi zingine nyingi zilizomuwezesha kupata fedha ya kujikimu. Sarah aliendelea kumshukuru milard kwa ukarimu aliomuonesha kwa kuendelea kumpatia tunda lake bure kila iitwapo usiku na mchana wakati wa week end.

mikaka miwili nyuma huko siera leone kabla ya sarah kukutana na milard
Mwaka 2011 milard alijulishwa na mama yake kwamba arudi kwao kwani kuna jambo la muhimu la wao kuongea kama familia. basi bila hiyana milard alijipanga na mwaka huo huo alisafiri kutoka sweden hadi kwao ili kuweza kumsikiliza mama yake. Alipokelewa kwa furaha sana na baada ya siku mbili toka afike mama yake alimkalisha chini ili amwambie alichomuitia.
Mama yake alianza kwa kumpngeza mwanae kwa namna ambavyo mwanae huyo amekuwa akimsaidia tokea baba yake alivyokufa hadi muda ule na ambavyo ameweza kubadilisha maisha ya nyumbani kwao tangia alipoingia ulaya. Mama yake pia hakusita kumkumbusha kuhusu watoto wa ndugu zake ambao tayari walikuwa na familia japo ni rika moja na milard. Alisisitiza kuwa hata kama milard atakuwa tajiri namna gani ila kama hana familia basi heshima itashuka na zaidi ya hapo maisha ni mafupi hivyo ni vema afikirie swala la familia kwa haraka sana.

Milard alishangaa sana kwani kama ni swala la ndoa mama yake angeweza kuongea nae kwa simu hakukuwa na ulazima wa yeye kupanda ndege hadi Africa kwa ajili ya kuambiwa swala la ndoa. Kwa kuwa alimpenda sana mama yake hakuonesha kama amekereka Bali alimkubalia na mama yake na kumuahidi kwamba mwaka ule usingeisha bila kutambulishwa mkwe wake mtarajiwa.

Swala la mwanamke halikuwa tatizo kubwa kwa milard kwani tayari alikuwa na wanawake 3 wanaompenda sana na wote aliwaahidi ndoa. Kati ya hawa watatu wawili walikuwa wakiishi sieraleone na mmoja alikuwa anaishi Netherlands. Tatizo lilikuwa ni yupi kati ya hawa 3 angemchagua kuwa mke wake?. Ni baada ya mama yake kumkumbushia swala la ndoa (hasa kitendo cha kumtoa ulaya hadi Africa kwa swala hilo) kulikomfanya aanze kuwaza sana namna ya kuwakata waanawake wawili na kubaki na mmoja au kuwakata wote na kutafuta mwingine ili amuoe.

Wakati bado akiwa kijijini kwao milard alimua jumamosi moja kwenda kanisani kwa ajili ya ibada. Kwakuwa ni muda mrefu anakuwa mbali na familia yake alimua siku hiyo kuifanya special na kuongozana na mama yake pamoja na mdogo wake aliyeitwa derrick. Ibada ilipoisha mama yake alikuwa busy kusalimiana na wanafamilia wengine na hivyo vijana hawa waliungana na mama yao katika zoezi hili. Mama yao aliwatambulisha kwa wanae kwa washiriki mbali mbali ambao walikuwa hawawajui na kusisitiza kwamba mwanae mmoja alikuwa Sweden kwa ajili ya masomo pamoja na kazi na amekuwa msaada mkubwa kwa familia yake. Muda wa kusalimiana ulipoisha basi kila mshiriki alirudi nyumbani kwake.

“Hodi mama…..” ilikuwa ni suati ya binti iliyokuwa ikibisha nyumbani kwa mama milard. “karibuuuuuuu’ aliitika mama milard akielekea mlangoni kufungua mlango. “Oooh Elsieee karibuuu sana” mama milard alimkaribisha mgeni aliyekuwa anabisha. Wakati mama anelekea nje akagongana na milard ambaye naye wakati huo huo alikuwa anatoka nje kwa ajili ya kumsaidia mama yake kuchanja kuni kwa ajili ya kuandaa mlo wa siku hiyo mchana. Hivyo wote wawili walimpokea Elsie ambaye alikuwa amebeba magimbi ya Africa magharibi (yams) kwenye kapu kubwa na mafuta ya mawese (palm oil) kwenye dumu kubwa. Elsie alimmwambia mama milard kwamba mawese yale pamoja na magimbi ni zawadi ambazo mama yake alimtuma azilete kwa mama milard. Mama alishukuru sana na kumsisitiza Elsie akae ili amtengenezee chochote lakini elsie hakukubali. Alisisitiza kupewa kapu lake ili awahi nyumbani kwako akaandae mlo wa mchana kwani mama yake alikuwa ameenda kwenye shughuli za kanisa.
 
Baada ya Elsie kuondoka milard alimuuliza mama yake Yule binti alikuwa ni mtoto wa nani pale kijijini kwao na wana ukaribu gani hadi kufikia kumletea mama yake zawadi muhimu kama zile. Kwa watu wa Africa magharibi yams na palm oil ni bidhaa za heshima sana kumpelekea mtu. Hivyo mtu anapopelekewa zawadi ya namna ile huwa kunakuwa na jambo kubwa sana linaloendelea kati yao au huwa ni marafiki walioshibana sana. Mama milard alimuelezea mwanae kwamba mama Elsie ni rafiki yake sana na wamekuwa wakishirikiana kwa karibu sana na kwa mambo mengi. Aliendelea kuelezea kwamba zawadi zile zilikuwa ni kwa ajili ya Milard kwani ni muda kidogo tangu aondoke nyumbani hivyo ule ulikuwa ni ukaribisho. Milard alielewa na akakatisha mazungumzo yale kwa kuelekea zilipo kuni na kuanza kazi ya kuandaa kuni za kupikia mchana ule.

Je nini kitafuata? Usikose sehemu ya 3 ya simulizi hiii
 
SEHEMU YA TATU
Millard aliandaa kuni na kumpatia mama yake ambaye aliandaa supu ya bamia (maarufu Kama okra soup) pamoja na ugali kwa ustadi mkubwa. Baada ya mlo kuwa tayari basi akatenga meza na kumuita mwanae Huyu mpendwa ili waweze kujumuika pamoja. Mama Millard alikuwa ni mapishii mzuri wa vyakula vya asili na kamwe mlaji wa mlo wake asingeacha kusifia chakula chake baada ya kujiweka mdomoni. Hali haikuwa tofauti kwa Millard ambaye baada tu ya kupata ombi la chakula alimuangalia mama yake na kumpa sifa kem kem kwa kupika chakula Kitamu na chenye ladha.
Basi walikula wote kwa furaha na baada ya kumaliza kula Millard alimwambia mama yake apumzike Kwani yeye Ndio angetoa vyombo mezani na kuweka mazingira ya mesini kuwa sawa.
 
Back
Top Bottom